Mjadala wa kujitenga kwa Zanzibar ni mgumu kuliko kujadili kuuimarisha muungano... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjadala wa kujitenga kwa Zanzibar ni mgumu kuliko kujadili kuuimarisha muungano...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwakajilae, Jul 2, 2012.

 1. m

  mwakajilae Member

  #1
  Jul 2, 2012
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati tukiendelea kuhakikisha haya mainteligensia yaliyokuwa na nia ya kumuua Ulimboka yanaanikwa na kuyashughulikia.

  Nawaomba wanajamvi tuweze kulitazama na kulitafakali suala hili la Muungano wetu kwa kina na tahadhari kubwa ikiwa si kwa kukomoana, kuoneshana bali kutazama kwa mbele na nyuma.

  Mjadala huu unapande mbili za mabishano, upande mmoja ukionesha kutokuridhishwa na upande mmoja ambao ni Tanganyika isiyokuwapo, inayojinufaisha kwa kujificha kwenye sura ya Muungano. Lakini wa upande wa bara wanashutumu juu ya hadhi iliyo nayo Zanzibar kwa maana ya utambulisho wake kama nchi.

  Kiufupi matatizo makubwa ya Muungano wetu siyo hayo kimtazamo wangu bali ni uhusiano wa Muungano na Maisha ya Watanzania kama yanaenda sambamba.

  Mfano: Wazanzibari na Waliokuwa Watanganyika wanatambuana kwamba ni wamoja? Wananufaika na Muungano? Au ni Muungano wa viongozi tuu kwamba ndiyo wanaofahamiana?

  Hoja ya Zanzibar kuwa nchi au siyo nchi, hoja ya Zanzibar kuwa na uwakilishi sawa na bara ninaona haina Mashiko zaidi ya hayo machache niliyoyainisha hapo. Kwani nchi haiwi nchi kutokana na uwingi wa watu au ukubwa wa eneo lake bali ni kutokana na historia yake ya Mapambano ya kuitafta ujitambulisho wa nchi hyo.

  Ndo maana japo Afrika ni bara kubwa lakini halina mwakilishi wa kura ya Veto umoja wa Mataifa, ndiyo maana nchi kama Nigeria ni kubwa kuliko Uingereza lakini Nigeria haina kura ya Veto nk.

  Nilichotaka kukizungumzia ni Matarajio yetu juu ya Mapambano dhidi ya Muungano na hoja ya Zanzibar kutamani kujitenga.

  Kihistoria kabisa hakuna mtu anayeetambulika kama ni Mzanzibari, matunda ya Muungano ni utambulisho wa uwepo wa Wazanzibari.

  Wazanzibari wanaitaka Zanzibar ipi?
  Kuna Zanzibar ya Mwarabu, Kuna Zanzibar ya Mwingereza, Kuna Zanzibar ya Sultan, Kuna Zanzibar ya Uhuru wa mwaka 1963, Kuna Zanziba ya Mapinduzi na kuna Zanzibar ya Muungano ambayo ndiyo hii. Hawa wanaitaka ipi?

  Ijulikane wazi kwamba kabla ya Muungano haya makundi yote hayakuwa mamoja, yalikuwa makundi hasimu wakubwa, Muungano umewafanya wawe wamoja hawa.

  Kiufupi, tujadili mstakabali wa Zanzibar nje ya Muungano kwa wanaoijua historia ya Visiwa hivi vikubwa vya Pemba na Unguja.

  Nilikuwa naona ni rahisi kuuboresha Muungano huu ukawa wa wananchi kuliko kuuvunja pasipo kuyatazama haya mbele na nyuma.

  Asante.
   
 2. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Duniani kuna nchi 196 zinazotambulika na Zanzibar si mojawapo. U.N. kuna nchi 193 zinazotambulika na Zanzibar si mojawapo. Afrika kuna nchi 54 zinazotambulika na Zanzibar si mojawapo...

  Find out what i mean...
   
 3. J

  John W. Mlacha Verified User

  #3
  Jul 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  usingeweka conclusion ya huo msimamo wako wa mwisho ungeacha mjadala uendelee bila ya kusema ulikuwa unaona......
   
 4. T

  Topical JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Same shi t different day..

  Zanzibar tunaitaka ni zanzbar ya leo; hizo propaganda za historia waeleza wale wajingawajinga mliozoewa kuwagawa..
   
 5. m

  mwakajilae Member

  #5
  Jul 2, 2012
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukisema hivyo maanake wewe ni miongoni mwa wananchi munaounga mkono uwepo wa Muungano ulioizaa uwepo wa Zanzibar,ukiikataa Zanzibar ya sasa utakuwa una taka unguja, au pemba,Sultan,au Mwarabu.Mjadala uendelee.
   
 6. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kumbuka kuna miungano miwili Tanzania,Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na Muungano wa Unguja na Pemba. Tofauti na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ule wa Unguja na Pemba haukuwa na makubaliano. Wazee wa Unguja wanasema Jamhuri ya Zanzibar ilikuwa inajumuisha kisiwa cha unguja, kisiwa cha mafia ,na kilwa. Pemba na Mombasa ilikuwa ni Jamhuri nyingine. Wazee wa unguja wanasema ni Ureno iliyokalia visiwa hivyo ndio waliojumuisha visiwa vya Pemba na unguja Kama nchi moja. Swali wanalojiuliza wazee wa unguja ipo wapi hati ya muungano ya unguja na Pemba. Ili kabla ya JMT haikavunjika waangalie mambo ya muungano ya unguja na pemba. Source: nimeongea na wazee wa zanzibar
   
 7. a

  abdy76 Member

  #7
  Jul 2, 2012
  Joined: May 29, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tunataka znz ya uamsho!!!!!!!!!!!!!!
   
 8. l

  lum JF-Expert Member

  #8
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 343
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  yanii uwepo wa zanzibar unatokana na muungano duhh.
  mkuu muungano unatokana na uwepo wa zanzibar na tanganyika hawa ndio wazazi wa mtoto muungano.
  hayo mambo ya unguja, upemba,usultani na uarabu mlifanikiwa kutugawa hapo nyuma sasa hivi tushalishtukia hilo mtengo huo mtanasa wenye watanganyika
  ''JAMUHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA''shengesha badaeee
   
 9. u

  ukweli utadhihirika Member

  #9
  Jul 2, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi naona kwanini usiseme zanzibar ya nyerere ya saivi
   
 10. m

  mzaire JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Ondoa upuuzi wako..., Zanzibar inataka kujitoa na sio kujitenga ktk muungano wacha kuongopea Watanganyika.

  Iliojitenga ni S.Sudan.


  Wee ni kilaza kwanini ukaitwa muungano wa Tanzania na sio Tanzania?
   
Loading...