MJADALA WA KATIBA UNA MAANA YOYOTE KWA WATANZANIA WA KIJIJInI?

AMARIDONG

JF-Expert Member
Jun 24, 2010
2,502
180
Moto mkali wa madai ya Katiba mpya umeendelea kushika kasi baada ya wanazuoni, wasomi, wanasiasa na wanaharakati kukutana kwenye kongamano la Katiba lililoandaliwa na Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udasa) na kupendekeza namna ya mchakato wa kuiandika unapaswa kufanyika.
Hata hivyo, wabunge kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM), hawakuhudhuria kongamano hilo ambalo lilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo vijana wengi wa vyuo vikuu, wabunge wa Chadema, wahadhiri waandamizi na Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani.
Profesa Issah Shivji ambaye alikuwa mmoja wa watoa mada, alieleza kuwa wakati sasa umefika kwa wananchi wa Tanzania kuwa na katiba mpya ambayo itajumuisha misingi ya taifa itakayokuwa imelinda maslahi ya wananchi.
“Suala hili tusiliache likabebwa na wanasiasa hata kidogo. Kabla hatujaiandika katiba tuweke kwanza mjadala wa kuangalia mambo ambayo yana maslahi ya nchi na ambayo tungependa kuyaingiza ndani ya katiba,” alisema.
Alifafanua kwamba katiba mpya inapaswa iangalie maslahi ya walio wengi na hasa wanaoishi vijijini kwa kuangalia ardhi, madini, wanyama na maliasili nyingine, lakini pia mfumo mzima wa serikali kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi.
Profesa Shivji alisema haitakuwa sahihi suala la katiba likawa la Rais kama inavyoonekana sasa ambapo amekusudia kuunda tume itayoshughulikia mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya bila ya wananchi kuelezwa muundo wa namna tume hiyo itakavyokuwa, hadidu za rejea na baada ya kufanya kazi yake kitafuatia kitu gani.
Kwa upande wake, mwandishi wa habari mwandamizi hapa nchini, Jenerali Ulimwengu, alisema wakati umefika kwa wananchi kushiriki moja kwa moja kwenye mchakato wa kuandika katiba mpya kwa kuwa historia inaonyesha kwamba mabadiliko ya katiba yaliyofanywa huko nyuma hawakuyashirikisha.
“Wakati umefika kwa raia kuwa na nafasi juu ya serikali yao na siyo serikali kuwa na nafasi juu ya wananchi. Ni fursa ya kujiangalia upya na tusikubali kwenda haraka haraka; si zoezi la Rais, Bunge, vyama vya siasa, wanazuoni au waandishi wa habari, ni la Watanzania wote,” alisema.
Alipendekeza kwamba mjadala kuhusu mchakato wa katiba mpya uanze ndani ya vyama vya kiraia wa namna ya kuboresha misingi itakayolinda masilahi ya wananchi ili wawe na usemi kuhusu raslimali zao na serikali yao.
Ulimwengu alisema mchakato wa kuandika Katiba mpya utaisaidia Tanzania kujisanifu upya kwa kutambua rasilimali zote za taifa zilizo chini na juu ya ardhi na kuainisha umiliki na matumizi yake.
Alisema kwa usanifu huo, taifa litaweka bayana nani mwenye mamlaka ya kuruhusu matumizi ya rasilimali hizo na kwa wakati gani.
“Na kueleza rasilimali hizo ni mali ya nani, ni ya serikali, wawekezaji au wananchi…wananchi waliopo kwenye maeneo yenye rasilimali hizo wananufaika vipi? Mikataba iweje na mgawanyo wa mapato uweje kati ya serikali kuu na serikali za mitaa,” alisema Ulimwengu.
Bila kuonyesha kupinga nafasi ya wakuu wa wilaya au mikoa, alisema uteuzi wao umekuwa hauzingatii sifa wala vigezo vilivyowazi, akitolea mfano kwamba viongozi hao wamekuwa wakiteuliwa wenye elimu ya darasa la saba, sekondari, chuo kikuu, wastaafu wa majeshi wenye vyeo vya koplo au brigedia jenerali.
Ulimwengu alisema bila kuangalia uwezo na sifa za wakuu wa mikoa na wilaya, “eti wao ndio wanaujua zaidi siri za taifa ikiwemo hali ya usalama kuliko viongozi wengine wenye sifa kuliko wao.”
Alisema nafasi ya viongozi hao inapaswa kutazamwa upya na hilo linawezekana katika Katiba mpya.
Aliongeza kwamba ni vyema serikali ikalitazama suala la madai ya Katiba mpya wakati huu wa amani badala ya kusubiri machafuko.
Kwa upande wake, mbunge wa Iramba Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, alisema Katiba iliyopo hivi sasa haiwezi tena kutumika kwa kuwa ina makosa mengi ambayo hayawezi kuendelea kuvumiliwa.
“Tunahitaji Katiba mpya kwa sababu utaratibu uliotufikisha hapa hautatusogeza mbele, nchi haiwezi kuendelea kutawalika tena kwa sababu mfumo wa Katiba ya sasa unasimama katika nguzo tatu ambazo ni rais mfalme (mwenye madaraka makubwa), chama kimoja na muungano,” alisema Lissu na kuongeza kwamba “Muungano umeshabomoka kwa sababu Katiba mpya ya Zanzibar inaeleza kuwa Zanzibar ni nchi na Rais wake ni mkuu wa nchi…jambo ambalo halielezwi hivyo kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.” alisema Lissu na kushangiliwa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alisema mchakato wa mabadiliko hayo, unahitaji mshikamano mkubwa miongoni mwa wananchi na kwamba lizingatie misingi ya demokrasia.
Alimshauri Rais Kikwete, kufanyia kazi haraka ahadi yake ya kuunda tume ya kuratibu mchakato huo kwa kushirikisha kwanza chama chake (CCM), kwa kuwa suala hilo halikuwa kwenye ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010-2015.
Mwanataaluma, Renatus Mkinga, alisema mchakato wa kuandika Katiba mpya sio jukumu la Rais Kikwete, isipokuwa Bunge ndilo lenye mamlaka ya kutunga sheria itakayosimamia zoezi zima au kufanya mabadiliko ya katiba iliyopo ili kuruhusu kuandikwa nyingine mpya.
Alisema katiba ijayo inapaswa kuangalia maadili ya viongozi hususani wale wanaotumia vibaya madaraka yao mathalani kuiba mali ya umma au kujihusisha na rushwa.
“Sio kama ilivyo sasa hivi hata wezi ni wabunge na ni mawaziri, ndio wanaotamba,” alisema na kuwataja wabunge wenye kashfa za ubadhirifu wa mali za umma.
Mwanasheria maarufu nchini, Mabere Marando, alisema suala la Katiba mpya haliepukiki kwa sasa kwa kuwa kuna mambo ambayo yanasigina amani ya nchi ikiwemo kutokuwepo kwa tume huru ya uchaguzi.
Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika, alisema sio sahihi kwa Rais Kikwete kuunda tume ya kuratibu mchakato wa uchaguzi hivi sasa kwa kuwa Ibara ya 98 ya Katiba iliyopo inalipa Bunge mamlaka ya kutengeneza mfumo utakaoruhusu kuandikwa kwa Katiba mpya kwa kutunga sheria au kufanya mabadiliko ya katiba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa), Ananilea Nkya, alishauri kwamba kwa kuwa mchakato wa katiba mpya ni suala la muda mrefu, serikali inachotakiwa kufanya hivi sasa ni kutafiti kile ambacho wananchi wanataka kiwemo kwenye katiba na kutoa elimu kwa raia.
Waziri Kombani ambaye hakutoa mada yoyote kwenye kongamano hilo, alipotakiwa kutoa maoni yake, alisema asingeweza kusema chochote na badala yake, atawasilisha maoni yaliyotolewa wakati wa mdahalo kwa Rais Kikwete.
“Mimi nilikuwa msikilizaji tu hapa, nachoweza kusema ni kwam
 
Mfumo wa utawala kwa miaka 49 umekiuka katiba iliyopo kimsingi kwa kuifanya mali ya serikali na kuondoa haki ya wananchi kufahamu haki zao zilizopo kwenye katiba yenyewe.............wananchi walijengwa kuiogopa katiba na kuona yaliyomo ni 'matakatifu yanayohusu dola' na yasiyopaswa kuhojiwa na raia yeyote. Si ajabu kwa zaidi ya 95% ya watanzania kutojua kilichomo ndani ya 'katiba ya serikali yao' . Wanakijiji wanafahamu "kauli mbiu za Kilimo" na 'ahadi' nyingi wanazosikia wakati wa kampeni za uchaguzi bila kujua kwamba hizo si ahadi bali ni haki zao za msingi zinazopaswa kutajwa ndani ya "katiba ya watanzania". Mijadala ni muhimu zaidi kwao kwani ndio njia pekee inayowawezesha kufahamu nini umuhimu wa katiba mpya na kwamba wao ndio wadau wakuu.
 
Mbona meseji yako na haiendani ya kichwa cha habari?

Nilidhani baada ya kutoa muhtasari sasa utaonyesha hilo swali lako ktk kichwa cha habari!
 
Back
Top Bottom