Mjadala wa katiba live star tv toka ARUSHA

tusichoke

JF-Expert Member
Apr 2, 2011
1,316
216
Kwa wanaoweza kufuatilia hivi sasa mdahalo kuhusu mustakabali wa katiba mpya unaendelea star tv toka arusha
 
wachangiaji wanataka katiba mpya impunguzie rais madaraka,wabunge walioshindwa uchaguzi wasipewe ukuu wa mkoa au wilaya,idadi ya wabunge ipunguzwe,katiba itamke kiongozi mwenye kashfa ajiuzuru na mengine mengi
 
tuhabarishe huo mdahalo uko pande zipi bado wanaruhusu watu kuingia?
 
Inaonekana ni toka kumbi moja ya hotel za hapo Arusha,washiriki ni raia,wanachuo mount meru university, makumila na unaendeshwa na kituo cha sheria na haki za binadamu,mimi naangalia kupitia star tv sipo ukumbini ,naomba anayefahamu huo ukumbi atujuze
 
Vipi kuhusu suala la uwekezaji limegusiwa kwenye huo mdahalo?????? ukizingatia ya kwamba ni wanafunzi tena wa Vyuo ndiyo wako kwenye huo mdahalo. Mkuu tunaomba aliyeukumbini aendelee kutujuza, kwani sisi hapa tunajiandaa na MTANANGE kati ya MANI YU na LIVAPULI. Mimi nitakuwa nawajulisha mabao yatakavyokuwa yanapigwa.
 
Back
Top Bottom