Mjadala wa English ya Namba moja na wajibu wa UDSM Kama chuo alichosoma

pinno

JF-Expert Member
Jan 17, 2013
1,213
1,228
Kama Mtanzania yeyote, na Muafrika yeyote ambae anafuatilia habari mbalimbali , Nimejikuta sijapitwa na hizi habari na mijadala inayoendelea kuwa Namba moja ameshindwa kuzungumza lugha ya Kiingereza huko south

Tofauti na watu wengine, wanaoshadadia, mimi nina baki kuwa positive kuwa Mheshimiwa hajashidwa, bali ameamua kwa utashi wake na mapenzi yake kwa Lugha yetu adhimu ya kiswahili

Raisi ni mtu aliesoma toka Primary hadi Chuo kikuu, tena ngazi ya Phd, ukiachia primary education ambayo hutolewa kwa kiswahili, Elimu yote iliyobaki, hutolewa kwa lugha ya kiingereza.

Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Kimeutangazia Ulimwengu kuwa kinafundisha kozi fulani fulani kwa lugha ya kiingereza, na hata sasa navyoandika uzi huu, kuna mamia ya wanafunzi, ambao wapo mbioni kupatiwa ufadhili wa masomo katika nchi mbalimbali, ambapo badala ya vile vyuo viombe hawa wanafunzi wafanye mitihani ya English test proficiency kama Toefl na IELTS Waliomba wanafunzi hao kuleta tu barua toka vyuoni kwao za kuonesha kuwa walisoma masomo yao kwa Lugha ya kiingereza.

Mamia ya wanafunzi wa UDSM wamepeleka hizo barua, lakini sasa tunakuja gundua kuwa kuna graduate wa had level ya Phd ambae alisoma na kufaulu hapo ila bado hayupo sawa na lugha hiyo ya kufundishia ya chuoni hapo

Swali ni je? UDSM wanadanganya? kuwa English ndo lugha ya kufundishia hapo au wapo sahihi? na Je kama hawadanganyi Imekuwaje mtu akafaulu masomo yaliyofundishwa katika lugha ambayo yeye haijui?

UDSM wana la kujibu katika hili.

Maelfu ya wanataaluma mbalimbali wakiwemo madaktari, Mainjinia, Wana anga etc, katika nchi za Japan, China, Uswiss,North Korea, Russia etc, hawajui hata kiingereza kidogo. wamesoma katika mitaala ya lugha zao, na wamegraduate kwa hiyo, hata ukienda kwenye vyuo vyao, vimeainisha kabisa kuwa lugha ya kufundishia ni lugha hiyo.
Kwao hiyo sio habari

Habari ni kuwa na Injinia mwenye cheti cha chuo kinachotoa masomo yake kwa lugha ya kiingereza, na amefaulu ila hajui kiingereza hata cha kuombea maji ya kunywa.

Sina hakika kama haya yanayosemwa ni kweli, ila kama ni kweli namba moja kiingereza kinampiga chenga, UDSM wana la kujibu.
 
kuna kitu unatafuta hope utakipata
 
Back
Top Bottom