MJADALA WA ELIMU NA UDINI TANZANIA (Tafadhali isome yote, ingawa ni ndefu) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MJADALA WA ELIMU NA UDINI TANZANIA (Tafadhali isome yote, ingawa ni ndefu)

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Hacha, Jun 15, 2012.

 1. H

  Hacha Member

  #1
  Jun 15, 2012
  Joined: May 20, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MJADALA WA ELIMU NA UDINI TANZANIA

  Adui wa Waislamu ni utamaduni wa kiarabu wa Ghuba

   Ukristo, ama Uislamu na serikali si tatizo katu!

  Na Mobhare Matinyi, Washington DC

  Naomba nichangie hapa kama Mtanzania - na si kama mwislamu au mkristo au mpagani.

  Mosi, ni kweli kwamba kitabu cha yule padri mzungu, Dkt. John Sivalon, kinaleta shida sana
  mawazoni mwa watu. Lakini turejee kwenye ukweli wa kisomi, kwamba huwezi kuhitimisha jambo zito kwa kutumia chanzo kimoja. Hatuna maandiko mengine ya watu wasiokuwa na upande yanayothibitisha aliyosema padri huyu, kwamba nchini Tanzania kulikuwa ama kuna na upendeleo wa kielimu.

  Hakuna utafiti wowote unaothibitisha haya ila zipo tafiti nyingi zinaonesha kwamba Tanzania iko nyuma mno kielimu.

  Aidha, ni muhimu pia kuchunguza ili kujua kwamba Dkt. Sivalon alisema hivyo katika mazingira
  gani. Uongo unaweza kubadilishwa kuwa ukweli na ukweli kufanywa uongo. Je, tuna hakika na
  maneno ya huyu mwandishi padri? Kwani padri ni nani? Si ni binadamu tu? Najua ukitaka kuvutia upande mmoja itabidi useme aliyodai yapo lakini hali halisi inagoma. Nitaeleza.

  Pili, ingawa Mwalimu Julius Nyerere analaumiwa kwamba aliwabana waislamu kielimu, lakini
  kiukweli kama si yeye, hali ya kielimu ya waislamu nchini ingekuwa mbaya zaidi. Tusisahau kuwa
  tulipopata Uhuru, serikali ya Mwingereza haikutuachia shule za kutosha kwa sababu ilikuwa serikali ya kiwizi tu. Wakristo na dini za waasia, wakiwamo wabohora, waismailia na wahindu walikuwa na shule, lakini waislamu hawakuwa na shule. Nyerere alilazimika kukabiliana na ukweli huu.

  Sasa tukumbuke pia kuwa, wakoloni wa Ulaya walikuja Afrika Mashariki kwenye karne ya 19 wakati wakoloni wa Uarabuni walikuwapo tangu karne ya 13. Kwa miaka 600 Waarabu hawa hawakujenga shule hata moja; bali walijenga madrasa kwa ajili ya masomo ya dini, jambo ambalo lilikuwa heri lakini halikutosha. Shule za kwanza zilijengwa Tanganyika na Mjerumani zikiwa ni za darasa la kwanza hadi la nne kwa kutumia Kiswahili. Zanzibar zilijengwa sana sana na Mwingereza. Tafuta maana na historia ya maneno haya: (i) darasa/madarasa (ii) shule (iii) skuli. Jiulize yamekujaje?

  Kimsingi, Nyerere ndiye aliyezitaifisha shule za wasiokuwa waislamu ili na watoto wa waislamu
  waende kusoma kwa sababu walikuwa wanakwepa kubadilishwa dini na kulishwa nguruwe ingawa wakristo wengine kama wasabato hawali nguruwe hata kwa viboko.

  Tatu, baada ya uhuru, nchi yetu ikapiga hatua zaidi na tukaanza kujenga shule za msingi. Nyerere akajenga shule kwa juhudi kubwa zaidi kwenye mikoa iliyokuwa nyuma ambayo mingi ilikuwa ni ya pwani waliko Watanzania waislamu wengi zaidi. Huko kwingine wananchi walifanya kazi kubwa kujijengea shule kwa bidii kubwa. Haikutosha, Nyerere akaweka nafasi maalumu kwa makabila ambayo hayakuwa na watoto wengi shuleni. Ukweli ni kwamba waliofaidika zaidi ni makabila ya mikoa ya pwani (na kule umasaini kwa kutaja machache tu), ambako shule ilikuwa kama kituo cha polisi kwao. Watanzania wengi tulikuwa washamba, tunakwepa shule.

  Nyerere haikuishia hapo tu, bali akiwa anaongoza TANU na baadaye CCM, akajenga shule za
  Jumuiya ya Wazazi ya chama nyingi kwenye mikoa ya pwani, kama ile ya Bagamoyo na ya Vituka nje ya Dar es Salaam. Alipopata msaada kutoka Kuba, aliiachagua mikoa ya pwani pia kujengewa shule, na ndipo tukapata shule za sekondari kama Kibiti, Ruvu, n.k. Hata ile ya Waswidi ilijengwa Kibaha na ndiyo alikosoma kiongozi wetu wa sasa, Rais Jakaya Kikwete. Nyerere alifanya hivi kuwasaidia Watanzania wengi wakiwemo hao mnaowaita waislamu ambao mimi nawaita Watanzania.

  Ni kweli kwamba kwa wakati huo hakujenga sekondari nyingi, lakini kule kwingine kama Kilimanjaro waliamua kujenga shule za sekondari za binafsi kwa nguvu zao na ndiyo maana hadi leo wanazo nyingi. Serikali ya Nyerere ilitaifisha tu zilizokuwepo na ilipojenga, ilijenga kwenye mikoa yenye waislamu wengi. Ndiyo ukweli huo ila watu hawataki kuutafuta. Rekodi zipo, tafuteni muone.

  Nne, Serikali ya Tanzania haikuishia hapo. Wakati wa Rais Ali Hassan Mwinyi, waislamu
  walilalamika kuhusu suala la elimu. Zikafanyika juhudi nyingi ikiwamo kumweka Profesa Kighoma Ali Malima kwenye sehemu kama elimu. Juhudi hizi zilipelekea serikali kulifungia jarida maarufu la Afrika lililokuwa likichapwa London baada ya kueleza mambo kifitina.

  Itakumbukwa kuwa Marehemu Malima alianzisha awamu mbili za kwenda shule kwenye sekondari za serikali. Lengo lake likiwa kuongeza idadi ya watoto wanaokwenda sekondari wakiwemo wa kiislamu na wa kikristo pia. Wakati wa Marehemu Malima pia Tanzania ikapata nafasi za masomo kwenye mataifa ya kiislamu ya Misri, Algeria, Iran, na Uturuki, maalumu kwa ajili ya waislamu.

  Marafiki zangu walikwenda huko na walinithibitishia kwamba hii ilikuwa maalumu kwa waislamu tu. Hata hivyo, bado Waislamu waliendelea kwenda nchi nyingine zisizokuwa za kiislamu bila tatizo. Huu ulikuwa msaada mkubwa na mkakati mzuri wa kuwasaidia Watanzania kupata elimu. Mmoja wa wahitimu hao leo ni mtaalamu wa kuheshimika nchini wa TEKNOHAMA akiwa kama mkurugenzi hapo alipo.

  Tano, ikaja serikali ya Rais Benjamin Mkapa na yenyewe ikaweka rekodi ya kuwapa waislamu
  majengo ya chuo kikuu. Leo hii kipo Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro kwa kutumia majengo ya
  serikali ya kilichokuwa chuo cha TANESCO. Chuo hiki kinaongozwa na wasomi Waislamu
  Watanzania wanaoheshimika kama akina Profesa Juma Mikidadi aliyesomea udaktari wa falsafa kule alikosomea Nyerere, Edinburgh, Uskochi.

  Serikali ya Rais Jakaya Kikwete pia imejenga shule nyingi za sekondari nchi nzima na sijasikia ubaguzi kwa upande wa mikoa yenye waislamu wengi. JK pia amehakikisha waislamu wanaongoza wizara ya elimu ili kuondoa malalamiko, na si kweli kwamba eti asiyekuwa mwislamu akiwa waziri wa elimu, basi waislamu wanashindwa kusoma. Hakuna ukweli hapa.

  Najua kuna malalamiko mengi kuhusu shule na hata hospitali za misheni, lakini tuzitendee haki. Hizi ni za kuhudumia Watanzania wote, na ndiko binti mmoja wa rais wetu alikosemea pia (Kifungilo, Lushoto). Hata Mzee Yusuph Makamba hukiri kwamba alisomea kwenye shule za wamisheni na ndio maana anaimudu Biblia. Tuweni wakweli kwenye hili. Waislamu wanatibiwa kote huku, wanasoma kote, na ruzuku ndiyo mkombozi wa Mtanzania mnyonge pindi anapohitaji huduma za afya.

  WAISLAMU KWENYE VYEO NA ELIMU

  Sita, labda, tuje kwenye hili moja: KWA NINI HATUNA WAISLAMU WENGI KATIKA
  NAFASI ZA JUU SERIKALINI? Hili jambo ni la kweli, lakini inabidi tujiulize swali jingine zaidi:
  KWA NINI KUNA MADAI KWAMBA WAISLAMU HAWAJASOMA?

  Nianze na historia yetu. Waarabu walipokuja kwenye karne ya 13 walileta vitu kadhaa vikuu vikiwa ni viwili: dini nzuri ya Kiislamu na utamaduni wao wa kishenzi. Ndiyo, sijateleza ulimi wala mkono, Waarabu walileta utamaduni wa kishenzi. Utamaduni wa Kiarabu siyo dini ya Kiislamu na dini ya Kiislamu siyo utamaduni wa Kiarabu.

  Watanzania wengi wanachanganya haya mawili kwa kutokuwa na upeo. Tuulizeni tuliosafiri duniani, kuna Wazungu na Wachina Waislamu na kuna Waarabu Wakristo kama Wakoptiki wa Misri. Uislamu siyo Uarabu na Uarabu siyo Uislamu na kwa hakika Uislamu ndio uliopunguza ushenzi wa Waarabu (ujahiliya) na kuwapa utu na ustaarabu.

  Tukumbuke pia, Uislamu ndiyo ulioongoza elimu duniani kwenye karne ya sita, saba na nane na hata vyuo vikuu vya kwanza duniani vilikuwa vya waislamu, na haya majoho ya mahafali za leo yalianzishwa na Waislamu, siyo wazungu.

  Nirejee kwenye rekodi. Taasisi ya kwanza ya kielimu kwa Waarabu duniani ilikuwa Ez-Zitouna ya
  Tunisia iliyoanzishwa mwaka 737, lakini kinachokubalika kama chuo kikuu cha kwanza duniani ni
  Al-Karaouine cha Moroko cha mwaka 859. Chuo kikuu cha pili duniani kilikuwa Al-Azhar cha Misri
  mwaka 970 na cha tatu kilikuwa Nizamiyya cha Iraki mwaka 1065. Wazungu pamoja na kelele zao zote, chuo kikuu chao kwa kwanza ni Bologna cha Italia mwaka 1088 na baadaye mwaka 1096 kile cha Paris. Hakuna, ubishi, Waislamu ndio waanzilishi wa vyuo vikuu duniani.

  Saba, lakini si waislamu wote hupenda elimu, kama ilivyo kwa dini nyingine pia. Ukienda kwenye
  nchi za Maghrebu (Afrika Kaskazini) kama Moroko, Algeria, Tunisia, na Misri na zile za Mashariki
  ya Kati kuanzia na Uturuki, Siria, Iraki, Lebanoni, na Yodani kidogo, hadi Irani, kuna waislamu
  wengi wenye elimu kubwa.

  Hapa Marekani Waislamu wa mataifa haya wanaheshimika, mathalani, wahandisi na wataalamu mahiri wa teknohama hutoka Uturuki, Pakistani na India wakati madaktari mahiri hutoka Irani. Mataifa ya Pakistani na Irani ndiyo pekee yaliyomudu kuwa na wataalamu wake wenyewe wa nyuklia bila kusaidiwa na mataifa ya Ulaya na Marekani na wote walikuwa Waislamu, akiwemo Abdul Qadeer Khan wa Pakistani.

  Aidha, mwanasayansi aliyesimamia urushaji wa satelaiti ya India ya kwanza mwaka 1980, ni mwislamu Avul Abdul Kalam ambaye baadaye alikuwa Rais wa India mwaka 2002 hadi 2007. Ninachotaka kusema ni kwamba ukiondoa Waislamu walioko kwenye
  Ghuba ya Uarabuni, wengine wote ni wasomi wa uhakika. Sababu ni moja tu: UTAMADUNI.

  Nane, hali ni tofauti sana kule Ghuba kwenye nchi za Saudia Arabia, Yemeni, Kuwaiti, Omani,
  Katari, Imarata (Falme za Kiarabu) na Bahareni. Huko Ghuba watu hawataki shule. Tusiwasitiri sana na kuficha ukweli: Ghuba hawataki shule. Hawa watu wa Ghuba ndiyo waliotuletea utamaduni wao huu Afrika Mashariki kuanzia kule Somalia, shuka hadi Lamu, Malindi na Mombasa Kenya, njoo kwetu Tanzania anzia na Pangani hadi Kilwa na Mafia, teremka mpaka Pemba iliyoko kaskazini mwa Msumbiji - kote huku kuna watu wenye utamaduni wa Ghuba wa kukataa shule.

  Tusifichane ukweli, maeneo haya watu hawataki shule. Hili liko wazi. Kwa kuwa Waarabu wa Ghuba ndiyo walioleta pia Uislamu, basi watu hujumuisha kwa pamoja tatizo la kukosa elimu na hii dini nzuri ya Uislamu. Narudia tena, utamaduni wa kukataa shule ni wa Waarabu wa Ghuba, siyo Waislamu hapa duniani. Tatizo letu Tanzania ni kwamba Waislamu wengi (siyo wote) wamechukua utamaduni wa kimwinyimwinyi wa Ghuba wa kuzikimbia shule kana kwamba ndio ujanja. Hiki ndiyo chanzo cha malalamiko yote haya; hakuna cha uonevu wala nini!

  Saudia watu ni vilaza watupu kiasi kwamba kuna Wamisri milioni moja na zaidi wanaofanya kazi za kitaalamu. Kila taifa la Ghuba isipokuwa Yemeni na Omani, lina wageni wengi zaidi nchini mwake kuliko wenyeji kwa sababu wananchi wao ni vilaza; hawataki shule. Yemeni na Omani hawana mafuta wala gesi asilia, yaani ni maskini na ndio maana hakuna wageni wengi. Hata hivyo, ukienda Omani kuna Watanzania wengi sana (hasa wenyeji wa Zanzibar), laki sita na ushee na wao pia shule hamna kitu; wanaiga uvivu wa wenyeji wao.

  Tisa, hivyo basi, Waislamu wa pwani ya Tanzania, kama wenzao wote wa Somalia, Lamu, Malindi, Mombasa, Pemba, Unguja, Mafia, Kilwa, Lindi na Pemba ya Msumbiji, wana utamaduni wa Waarabu wa Ghuba wa kugomea shule. Tofauti na Waislamu wa Tanzania walioko Machame na Usangi mkoani Kilimanjaro, au Usukumani, au kule Bukoba, na hata wale wa Uganda (kabila la Baganda), wao wanapenda shule.

  Maeneo yote waliyokaa Waarabu, kuanzia Bagamoyo, halafu fuata ile barabara ya watumwa hadi Kondoa, nenda hadi Tabora, fika mpaka Ujiji, ingia mpaka Kongo Mashariki, kote huku shule si mali kitu. TATIZO SI UISLAMU BALI NI UTAMADUNI WA UARABU WA GHUBA. Anayebisha hongera zake.

  Kumi, tafiti tatu ninazozijua, moja ya Ilana Kessler wa Chuo Kikuu cha Georgetown cha Marekani
  ya mwaka 2005, na ile ya Erasmus Kaijage wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ya mwaka 1999,
  zinaonesha kwamba wanafunzi wa shahada ya kwanza wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliokuwa Waislamu ni kati ya asilimia 14 – 15 tu ya wanafunzi wote.

  Aidha, Baraza la Udhamini la Waislamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DUMT), liliwahi kutoa taarifa yake kwamba kati ya mwaka 1986 hadi 1990, kwa wanafunzi walioingia chuoni hapo kusoma shahada ya kwanza Waislamu walikuwa asilimia 13 tu. Hiki ni kiasi kidogo mno, lakini ni kidogo cha kiasi gani cha Waislamu nchini? Lazima tujue hili nalo pia, hata kwa makadirio tu.

  Kumi na Moja, sasa turudi kwenye jingine. Nyerere aliamua tuachane na sensa ya kupekua dini za watu kwa sababu nzuri kabisa - alitaka Watanzania tusitambuane kwa dini zetu (na makabila pia). Hivyo, ili kuweka usawa tukaanzisha msemo huu: Tanzania sisi nusu ni Waislamu na nusu ni Wakristo. Huu ni msemo tu na hauna usahihi. Aidha, hata kama sensa ya zamani ilionesha kwamba waislamu, ama wakristo, au wapagani ndiyo wengi, haina maana yoyote leo wakati taifa letu lina watu milioni 45 hivi. Tulipata uhuru tukiwa milioni 12 na baadaye Zanzibar ikaongeza laki tatu. Watanzania hatukuwa na kelele za asilimia ngapi ni dini hii na ile. Leo zimerudi. Inakera sana!

  Kwa mujibu wa taarifa kadhaa za kitafiti (siyo mimi), Waislamu nchini Tanzania ni theluthi moja ya wananchi wote. Aidha, kwa bahati ama kwa mpangilio, rais wetu wa sasa, Mheshimiwa Kikwete, alipoteua mawaziri Novemba 2010 aliweka theluthi moja waislamu, na hivyo hivyo kwa manaibu. Wote tunajua. Hali kadhalika, alipoteua mawaziri na manaibu wao hii juzi, aliweka theluthi moja waislamu kwenye uwaaziri na pia kwenye unaibu.

  Alipoteua Tume ya Kupitia Katiba, kwa wajumbe wa Bara aliweka pia theluthi moja yake waislamu. Iko wazi. Rais Kikwete, nijuavyo mimi, anajaribu kwa kila hali kuliangalia hili suala la kelele za udini ili asiiharibu nchi yetu. Hatopenda kukumbwa na malalamiko akishaondoka kwani na yeye ni binadamu kama sisi. Anakuwa mwangalifu sana hata kama kuna wakati anateleza kibinadamu. Je, hesabu zake zina maana gani? Nina hakika anajua anachokifanya na kamwe hawezi kuwaonea waislamu ambao ni Watanzania kama sisi wote. Hawezi kufanya uonevu.

  Sasa, zifuatazo ni taarifa zinaonyesha idadi ya waumini wa kiislamu nchini Tanzania:

  (a) Taasisi ya Kiislamu ya Asoon ya Iran ambayo inatunza rekodi za idadi ya Waislamu katika nchi zote duniani inadai Waislamu nchini Tanzania ni asilimia 35 ya wakaazi wote;

  (b) Taasisi ya utafiti iitwayo Pew Research Center ya Marekani ambayo ilifanya utafiti wa idadi ya Waislamu duniani inadai kuwa nchini Waislamu ni asilimia 30 ya wakaazi wote; (c

  (c) Ofisi ya Demokrasia, Haki za Binadamu na Uhuru ya Serikali ya Marekani inasema katika utafiti wake asilimia 35 ya wakaazi wa Tanzania ni Waislamu. Hizi si takwimu pekee na sijaweka za Wakristo kwa sababu sitafuti ushindani na siamini kama idadi ina maana yoyote Tanzania, na hizi kelele za idadi hazitufai; ni ujinga lakini anayezitaka aanzie na hizo hapo juu.

  Aidha, mnamo Aprili 2011, mwanazuoni mmoja wa Tanzania, Mohamed Saidi, alialikwa kuhudhuria warsha ya Mustakabali wa Demokrasia Afrika Mashariki iliyofanyika kwenye Chuo Kikuu cha Iowa, nchini Marekani. Akadai kwamba Waislamu ni asilimia 70 ya Watanzania
  wote lakini akashindwa kujibu maswali ya ni wapi wanakaa Watanzania hao kiasi kwamba
  hawaonekani kwa wingi huo.

  Mwaka 1994 pia, kwenye jarida la kitaaluma la Nordic Journal of African Studies, mwanazuoni mwingine aliyekuwa Chuo Kikuu cha Uppsala cha Uswidi, Abdulaziz Lodhi, alidai katika makala yake ya “Waislamu Afrika Mashariki: Zamani na Leo,” kwamba Waislamu nchini Tanzania ni asilimia 60. Hakueleza wako wapi. Nirudie: kelele za idadi ya waumini ndani ya Tanzania ni ujinga. Lodhi alidokeza pia kuwa Waislamu nchini Kenya ni asilimia 25, ya wakaazi wote, Uganda
  ni 45 na Msumbiji ni asilimia 40. Takwimu hizi zinapingana zingine zote zilizopo duniani zikiwemo
  za taasisi za kiislamu.

  Kumi na Mbili, kwa nini idadi inakuwa muhimu hapa, achilia mbali kelele ninazozipinga? Ni kwa
  sababu tunataka kuielewa hii asilimia ndogo ya wasomi wa kiislamu hapa Tanzania imekaaje? Je, leo hali ni nzuri zaidi kwa sababu tuna chuo kikuu cha kiislamu na vyuo vikuu ni vingi zaidi? Tunahitaji utafiti ili tujue Waislamu wengine wameishia wapi. Lakini ile nadharia yangu ya UTAMADUNI WA WAARABU WA GHUBA si ya kusahau.

  Kiukweli, hakuna mfumo wa kumfanyizia Mtanzania mwislamu. Hakuna ushahidi wala nia. Mimi
  nimekulia na kusomea Dar es Salaam kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita, na JKT kabisa. Waislamu wote marafiki zangu waliokuwa wakali darasani waliendelea na elimu ya juu. Kwenye shule ya msingi yetu tulikuwa watoto wanne machachari, mimi, Waziri, Salum na Izihaki, na wote tulifaulu.

  Nilipokwenda Azania mwaka mmoja nyuma yetu palikuwa na kijana mwislamu wa Pemba
  aliyeongoza Tanzania nzima mwaka wao na akafanya hivyo tena alipokuwa Tambaza kidato cha sita. Baadaye alikwenda Ulaya kusomea uhandisi kwa nafasi iliyotoka serikalini; hakunyimwa nafasi yoyote. Hao wanaonyimwa wako wapi? Tulipomaliza kidato cha sita aliyeongoza Tanzania nzima alikuwa mwislamu, Karim, na alikwenda Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  Uchache wa Waislamu kwenye vyeo unaweza ukachangiwa na idadi ya kweli ya waislamu nchini,
  pamoja na idadi ya wanaofika kwenye elimu ya juu kulinganisha na wasiokuwa waislamu. Tanzania, tukiri, kwamba tumeathirika na utamaduni wa Waarabu wa Ghuba, hasa huku pwani ambako kwa bahati ndiko kwenye Watanzania wengi waislamu. Hakuna cha kushangaa bali huu ndio ukweli. Mambo ya vyeo ni matokeo tu lakini tuna uwezo wa kuleta mabadiliko.

  HITIMISHO NA OMBI

  Tufanye juhudi kuwakomboa wale wote walio nyuma kielimu Tanzania. Wako wengi, kwa dini na
  makabila mengi tu, lakini wote ni Watanzania. Walio nyuma wasiseme eti kuna uonevu, bali waondoe kilichowakwamisha. Sasa Wakurya waliokuwa wanakimbilia jeshi wanaacha shule, nao wamlaumu nani hivi leo?

  Hatuwezi kulinganisha utamaduni wa elimu wa watu wote nchini, mathalani, watu Kilwa, Mafia, Rufiji na Pangani, na watu wa Moshi, Kyela, au mkoani Kagera. Sijasema kwamba hakuna wasomi huko, la hasha! Wapo, ila ni wachache kulinganisha na wenzao na tafiti zipo.
  Mathalani, watoto waliopata “A” kwenye somo la dini ya kiislamu kwenye mtihani wa kidato cha sita uliopita ni Rahma A. Mushi na Mabina M. Mabina. Kwa nini? Ukweli unauma lakini ukweli ni dawa ya matatizo; huwezi kutibu malaria kwa dawa ya kichocho.

  Watanzania tuweni wakweli. Mwenyezi Mungu hapendi waongo. Kwa nini shule za binafsi hazina
  pia waislamu wengi? Nani anawazuia waislamu kujenga shule Tanzania hivi leo? Je, kama kweli
  unataka mtoto wako apate elimu safi, na amekosa nafasi ya shule ya serikali, utampeleka wapi? Pale Kinondoni Muslim ambapo wanafunzi huanguka mitihani? Tuseme ukweli.

  Naamini tunao uwezo wa kuyatatua matatizo yetu ya kihistoria na kitamaduni na si kukaa chini
  kupanga vurugu kwa madai ya kuonewa. Waislamu wa Saudi Arabia hawajasoma licha ya utajiri wao. Je, hao nao waziri wao wa elimu na baraza la mitihani limetoka Tanzania? Mbona waislamu wa Uturuki, India, Pakistani, Tunisia, Moroko, Misri, Senegal na Afrika Magharibi yote wana elimu?

  Tutafute chanzo cha kweli cha tatizo, halafu wote tushirikiane kulitatua; wote kabisa. Rais Mwinyi husema kila siku: Waislamu pelekeni watoto shule, acheni kulalamika. Waislamu wa duniani kwingine ni wasomi na walioko Tanzania wanaweza kuwa wasomi kama watakavyo. Tukumbuke pia, kama taifa, bado tuko nyuma mno kielimu na tunahitaji kuruka na ungo wakati wenzetu wanatambaa!

  Wabilahi Tawfiki!

  Mwandishi wa makala hii, Mobhare Matinyi, aliwahi kuwa mhariri mkuu hapa Tanzania lakini kwa sasa ni mkufunzi kwenye Taasisi ya Mambo ya Nje ya Marekani, jijini Washington DC. Ana shahada tatu za uzamili (Masters) katika mawasiliano ya kisiasa, masuala ya mikakati (strategic studies), na uhusiano wa kimataifa.

  Anapatikana matinyi@hotmail.com.


  IMETOKA KATIKA GAZETI LA JAMHURI LA JUMANNE JUNI 12-18, 2012 ISSN NO. 1821-8156
  TOLEO NO. 28
   
 2. Olaigwanani lang

  Olaigwanani lang JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 480
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hongera sana professa umesema ukweli......
  but kuna msemo wa kiingereza unaosema kwamba.."if you want to put something secrete to africans...write a book.."

  kama wataisoma hii.....,wataelimika...wakikataa basi ndo hivo tena....!
   
 3. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Umeeleweka mkuu. Asiyetaka kuelewa ana lake jambo!
   
 4. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Haya sasa ngoja tumsikie Sheikh Ponda and Co.
   
 5. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ningalifurahi angalichambua kwanini wakiristo wanasomeshwa kwa kutumia mkataba wa MOU lkn nchi inazidi kuwa maskini na ufisadi na kukosa wataalam na kuomba nje. jee kunafaidaganiya kusomesha dini 1 huku UFISADI kitaifa ukikuwa?
   
 6. N

  Ndakilawe JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 4,084
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  umenifumbua ufahamu wangu katika mengi ambayo nilikuwa siyajui!
   
 7. T

  Thesi JF-Expert Member

  #7
  Jun 15, 2012
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ukweli bila chenga
   
 8. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,659
  Trophy Points: 280
  Namsubiri Seleman Filambi wa MUM aje na data mpya! Kwake John Sivalon ni kama msaafu!
   
 9. sister

  sister JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,029
  Likes Received: 3,940
  Trophy Points: 280
  atakayeendelea kubisha ni mbishi tu ukoo mzima unamjua.
  thanx mkuu somo nimelielewa.
   
 10. mwakaboko

  mwakaboko JF-Expert Member

  #10
  Jun 15, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 1,841
  Likes Received: 257
  Trophy Points: 180
  Asante kwa kutuelimisha Mkuu, nimefurahia sana andiko lako MKUU.
  Ila ndugu yangu kuna watu watakuja hapa nu kukushutumu kuwa umetumwa na kanisa naomba uwavumilie na tayari wameiingia. Hao wako kwenye chungu na wengine wanasema eti ni wasomi wenye PhD. Nakushukuru sana mkuu kuna mengi nilikuwa siyajui nimeyajua sasa baada ya kusoma andiko lako. Tupe mengine MKUU
   
 11. K

  KIGIGI Member

  #11
  Jun 15, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kiukweli, kama watanzania wote wangesoma hii makala, hakika wangefumbuka fikra zao ambazo kwa sasa zimejaa chuki juu ya wengine. Prof. yote uliyosema ni kweli. ukiangali sana maeneo yote ambayo mwarabu aliwahi kukaa mpaka leo hii hali zao ni duni na sijui kama watakuja badilika kama hawatokuwa tayari kusoma makala kama hizi na kuzifanyia kazi. Mwaka jana nimefanyia field yangu pale ujiji Kigoma kata ya Kagera, kiukweli hali inatisha. wakazi wengi wa pale ni waislamu. Wazazi wa pale hawajui kusoma wala kuandika na hwapendi watoto wao waende shule bali huwalazimisha kwenda kukariri kiarabu tu. Hivi kweli kwa hali kama hii malalamiko yataisha?. Waislamu ifike sehemu wabadilike, wasiendelee kulishwa maneno ya sumu na viongozi wao wa dini.

  Makala hii naiprent kwa faida ya wote.
   
 12. t

  thinka JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 335
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Ndo mana bakwaata wanataka kiengele chaa dini kiwekwe hzo taasisi zimepata wap hzo asilimia na kigezo gan waametumia kumjua mtu muislam au mkristo?kama jina kwa wasio mfaahaam utawezaa kujua zito kabwe ni dini gan?
   
 13. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #13
  Jun 15, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Umesahau, NYERERE PIA ALIANZISHA UJAMAA NA KUJITEGEMEA VIJIJINI, NA YEYE ALIANZISHA AZIMIO LA ARUSHA NA YEYE NDIO ALIIUA HII NCHI na kufikia hapa tulipo! na yeye NDIO ALIANZISHA UDINI na mpaka leo tunalumba,a tena wewe ni mnafiki, unajidai sio muislamu, mkirisito wala mpagani, wewe ni Mkirisito! hatudanganyiki mpaka kieleweke!

  Usipotoshe kuna shule nyingi pia zilijengwa na waismailia ambao ni waislamu acha kupotosha watu !
   
 14. t

  thinka JF-Expert Member

  #14
  Jun 15, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 335
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  katikaa makala yako inaonyesha ww wa dini gan.pale unapokataa yalioandikwa na padri kwa sababu tu hayaendan na ww unayoyataka kusikia unasema uwezi kuthibitisha kutoka source moja.nan kasema ipo hyo tu?pili umeikubal taasisi ya kiiran eti ni ya kiislam kwa sababu tu wameongea unayoyataka ww.
   
 15. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #15
  Jun 15, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,401
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Jamani someni neno kwa neno hadi mwisho. Unakurupuka ku-quote na kuweka hoja legelege wakati zimeshafafanuliwa humo ndani. Acheni uvivu wa kusoma na kutafakari. Kweli ukitaka kutunza siri Bongo weka kwenye maandishi. Natamani hata kuwakata vibao kwa uvivu wenu.
   
 16. UKI

  UKI JF-Expert Member

  #16
  Jun 15, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 699
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  makala imeeleweka vizuri mno mpka nimepata elimu fulani ambayo nilikuwa siifahamu ila nasikitika kuwa watu hawapingi kwa hoja badala yao wanatoa maneno ya mtaani? kweli na elimu yako bado unatoa comment za ajabu ajabu inasikitisha sana na inauma sana kwakweli yeye katoa makala kama una maoni tofauti pinga kwa hoja sio kutoa maneno ya kejeli. kama utashindwa kujiongoza kichwani mwako kama kiongozi je familia utaiweza kweli? nahisi kuumia na mtu anasema mpka kieleweke ni kipi ambacho hakieleweki? kwa hiyo mtafurahia kuona damu za watu zikimwagika ndio kitaeleweka? hata mauwaji ya rwanda yalichangiwa sana na media kila mtu kutoa maoni yake yatakuja kutuponza sote.
   
 17. A

  ADK JF-Expert Member

  #17
  Jun 15, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 1,169
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Pongezi mkuu makala imeenda shule hasa mods wangeihamishia kule jukwaa la dini, wachangiaji wangekuwa wengi mno
   
 18. Hute

  Hute JF-Expert Member

  #18
  Jun 15, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,062
  Likes Received: 3,927
  Trophy Points: 280
  hao boko haram hawawezi kusoma yote hiyo, walivyo wavivu kusoma, ndio maana wako nyuma. ukiwambia wacheze bao asubhi hadi jioni wanaweza, ukiwambia wachambue mchele pilau lipikwe wanachambua hata gunia. lakini ukiwaambia wasome kurasa kumi tu za kitabu wanaleta sababu kibao mara ohhh umeona sisi sio wasomi mara oohh unatudharirisha waislam....yaani kwao hata uwape kila kitu hawakosi kulalamika. kwani nani amewazuia kujenga shule na mahospitali, wao kwa wao wanapigana kwa majambia huko misikitini sembuse kwa wenye dini tofauti....hata uchukue ile tosamaganga leo, au mzumbe high school ubadilishe iwe ya kiislam leo, itakaa miaka miwili tu itabadilika na kuwa kama kinondoni muslim...wamerithi toka kwa waarabu, wao wanafikiria kutumia kitabu cha mtume, hawafikirii kwa kutumia ubongo ambao Mungu wa kweli amewaumbia....dawa yake ni kuwapuuza tu, watalalamika hadi watazeeka na sisi watoto wetu wataendelea kupaaa kwasababu hatuna muda huo wa kupoteza kulalamika ila kufanya kazi kwa bidii na kutengeneza maisha ya baadae ya watoto wetu.
   
 19. J

  JITU PEVU Member

  #19
  Sep 5, 2014
  Joined: Jul 22, 2014
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata ukweli ukaelezwa usiku na mchana,jukum la kubaini na kuweka usawa ktk elimu,maendeleo na fursa baina ya jamii moja au kikundi kimoja na kingine ni la serikali na ndo chombo pekee ambacho kina dhamana ya kukabiliana na changamoto kama hizo.UHAKIKI,Hata mkoloni alipoleta elimu haikuwa rahisi kulifanikisha ila walifanikiwa,Sera za usawa baina ya wanaume na wanawake ilikuwa na changamoto ila inaendea kufanikiwa kulikoni jamii iaminishwe kuwa uvivu na utamaduni ni sababu ya kuhalalisha baadhi ya jamii ziendelee kukosa haki zao na kula msoto wa maisha magumu ktk ardhi huru?HUO NI UNANGA NA WATAPOIBUKA MAGAIDI WAKIAMINI WANAONEWA, KWA KULEA HALI HIYO HAPO NDIPO WAJINGA WATAELEWA NINACHOKIELEZA.
   
Loading...