Mjadala: Upinzani utaanzaje kujipanga kwa uchaguzi wa serikali za mitaa wa 2024 na hatimae uchaguzi mkuu wa uraisi wa 2025 ndani ya mazingira magumu?

Nashauri Mr Mbowe aongeze umakini Kwa suala la maridhiano.

Timeframe ni muhimu, ninanusa harufu ya HADAA mahali!!!!
Huyu jamaa yuko makini kwani anasubiria kikosi kazi kimalize kazi na hayo maridhiano wasipopata mwafaka watalianzisha ndani na yule Lisu atalianzishia Airport kwani uwanja utakuwa wao.
Ndo maana watu wanalazimisha arudi sasa ili joto lisiwe Kali wakati Mwamba anajua anachokifanya ili mwisho uwe mzuri kwao ila sisi tutabaki tunasema tungejua na hiyo tungejua mandamano yatakuwa yameshaenea nchi nzima.
Mwanaccm mm nakuwaga muwazi kuendana na mazingira yalivyo
 
Wewe wachangamsha baraza sio?
 
Ukisema kama nina mbinu niwapelekee huko ofisini kwao unakuwa hutumii njia sahihi ya kufikiri kwa undani kwani waonyesha kukata tamaa lakini amini nakuambia hiki tukiongeacho hapa kina maana kubwa sana.

Bado naamini machafuko si njia sahihi bali njia za kawaida tu zatosha. Lakini kwanza tuna budi kuangalia hali ya kiuchumi ya upinzani je, wana hali gani kifedha? Shughuli za uendeshaji wa chama wahitaji fedha na mipango, je Chadema ina vyanzo imara vya fedha ambavyo huko mbele vitaweza kuwa mbadala wa ruzuku kutoka serikalini?

Fedha nyingi huelekezwa katika maeneo kama ya kidijitali na huko ndiko kwenye kukiimarisha chama lakini je ni kwa mtindo upi?

Ok, tuseme Chadema yaanza na uchaguzi wa serikali za mitaa hii ndo njia sahihi ya kujenga "base" ya viongozi wengi ambayo itasaidia kupatikana wabunge wengi kwa mtindo mmoja tu.

Sasa basi, wewe wataka kuwa diwani wa kata fulani lakini si mhuni, umesoma uzuri hadi chuo kikuu na ni lazima ushinde katika kata yako. Hivyo Chadema digital itaandaa "profile" ya mgombea, vipeperushi vinavyomuongelea mgombea na mwisho sera zake zote anoziuza kwa wapiga kura. Hali ni hiyohiyo kwa wagombea ubunge na hiyo si tu bila mkutano wa halaiki bali vipeperushi vyenye ujumbe tosha kwa mpiga kura.

Hizi ni hatua ambazo zapaswa kutekelezwa mwanzoni katika ya upigaji kura ya maoni na namna ya kuufikisha ujumbe kwa wananchi kulinganisha sera au ilani ya CCM na ile ya kwenu, wapi CCM wameshindwa na ninyi au mgombea wenu atafanya nini tofauti.

Hii hatua ya Chadema UNGANISHA au "connect" ni hatua ambayo ikifika kwa walengwa mgombea anakuwa hana shida ya kujitambulisha maana tayari ajulikana kabla hata ya siku ya mkutano wa kampeni.

Mambo yaliyomo katika hii "Connect" au UNGANISHA ni pamoja na uchapaji, utumaji na uwasilishaji wa ujumbe ama kumtambulisha mgombea au kuweka msisitizo wa siku ya kupiga kura.

Hivyo katika eneo husika la kugombea udiwani au ubunge kipeperushi maalum kinachomhusu mgombea kwamba yeye ninani, na ana sera zipi na taarifa zingine atapewa mpiga kura ili achambue.

Asikwambie mtu, hakuna siri kubwa ya kupiga kura kama utumiaji wa sanduku la kura hivyo kwenye hili mbinu kadha wa kadha huitajika ili kuhakikisha wingi wa kura unaleta hofu kuu kwa watawala na DS yao.

Mbinu ingine ni ile ya mvuto na kusajili wanachama katika kila kata kwa kutumia mfumo wa kidijitali na sio kukusanya panyaroad mitaani na wahuni wengi ambao wataviuruga mrindimo wa kisiasa. Hivyo Chadema Digital yapaswa kuweka platform ndani ya tovuti yake ambayo itasajili wanachama wapya kwa kutumia Chadema Digital App ili kusajili vijana au kuwatambua na kuwafanyia uhakiki wale "grassroots" wote ambao ndo nguzo muhimu ya uimarishaji na uhamasishaji.

Eneo hili la Chadema Digital CDM hawajalitendea haki kwani bado tovuti yao imejazwa mipicha tuu kila kona badala ya mambo mengine muhimu sana katika ulimwengu wa mitandao.

Sasa nimalize kwa kusema zipo njia nyingi zaidi ambazo hata wewe bado huzifahamu na labda mwenyekiti Mbowe atanielewa, kuna "Doorstep App", kuna "contact creator" nyakati za kampeni na pia kuna "Word Press Network". Hizi ni zile za kuingia ndani zaidi kumpata na kumshinda mtesi wako.

Tuendelee ntazungumzia kiaina maana hizi ni mbinu na huwezi kuweka mbinu hadharani.

Richard naona umetawaliwa na nadharia, uhalisia ni huu, kwanza CDM kwa sasa haina fedha nyingi ya kuendesha shughuli zake, labda za watu wakujitolea, ambao nao wameingia woga kwani wanaweza kukomolewa na dola, na haya tumeona kwa wengi waliosupport upinzani.

Fahamu kuwa kwa sasa wafuasi wengi wa upinzani na wananchi wengi wamelipuuza box la kura. Hivyo usitegemee wapiga kura hasa wa upinzani kujitokeza tena kwa wingi, labda Lisu arudi apandishe hamasa. Kile kitendo cha wafuasi wa upinzani kuwapigia kura, na kulinda kura za wagombea wao, kisha wakaondoka kwenda kuunga juhudi, na hawa akina Mbowe kwenda kwenye maridhiano sasa, wafuasi wengi wa upinzani wamekosa imani sana na mwenendo huo. Huu ushauri wako unaosema sioni kama utakuwa na maana au nguvu yoyote kwa watu waliopuuza box la kura, machafuko tu ndio njia ya ukweli kwenye hali hii.
 
Nadharia ni hatua mojawapo ya kufikia lengo lako, hata ukiataka kuendesha gari si utapitia kwanza nadharia au ukisoma kemia si kuna nadharia kwanza na kisha vitendo?

Hivyo weye chukulia hii ni nadharia na ikipenya na kungia kwenye fikra utafahamu nini namaanisha.

Nadharia zipo nyingi tu hii tunoiongelea hapa ni nadharia ya mabadiliko au "theory of change" kwamba yaelezea kuhusu njia fulani ya kipekee ambayo ikitumika italeta matokeo chanya na yenye ufanisi.

Angalia mfano wa dhana ya mabadiliko alotengeneza jamaa aitwa Align yaitwa Align Theory of Change.

1663347666695.png

Hapo kwa harakaharaka ni kwamba hali ya sasa yaani "current condition" ni kwamba si nzuri kiuchumi na pia kuna mambo mengi yasofaa kabisa kinyume na matarajio ya wapiga kura.

Pili, stratejia ni kwamba tupo kwenye hatua ya kutengeneza mijadala na hii mada ni mojawapo na stratejia hizo.

Tukimaliza hii twaingia kwenye kuchukua hatua yaani "Action" na kufuatia kuangalia matokeo yaani Impact ya hatua zilochukuliwa.

Tukipita hapo yaani 2024 na 2025 tunakuwa na Vision yaani maono sahihi na twaendelea na kazi.
 
Nimewasikia viongozi wa CDM, Mnyika na Mbowe wakisisitiza kutoshiriki uchaguzi wa 2024 na 2025 bila kwanza kupatikana KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi.

Tafsiri ya HOJA zao ni:

1. KUSUSIA uchaguzi.

2. Kushinikiza madai Yao yapatikane kabla ya Uchaguzi, yaani kugomesha wananchi Ili uchaguzi usifanyike Hadi madai muhimu kufanyiwa KAZI.

Hoja NO 2. yaweza onekana NYEPESI Kwa watawala wakaipuuza bt Hali ya kiuchumi inaweza sababisha uungwaji mkono mkubwa sana ndani ya JAMII mbali na wananchi Walio Wanachama wa Vyama kinzani.

Chama Tawala wakisaidiwa na deep state mara zote kimekuwa na THINK tanks wawezao kuona MBALI na kurekebisha mapema.

Tuliona mfano wa kupatikana Jina la Magufuli asiyetegemewa Ili kuinusuru chama kuanguka.

Natabiri mifumo isiyoonekana kuwa nyuma ya hoja ya KATIBA mpya na TUME huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote kama njia pekee ya kuinusuru Nchi na machafuko ya chaguzi kandamizi.

Ameeeen.
Katiba yetu ya mwaka 1977 inaweka wazi utaratibu wa mikutano ya hadhra kwa sasa mazingira yaliyopo hayana tofauti na ya yale ya mwaka 2010 na mwaka 2015 , Upinzani uache uwoga ujenge hoja na agenda inayokidhi matarajio ya wananchi waendeshe mikutano ya Hadhra katika mazingira hayahaya ya sasa , haki haiombwi haki inatafutwa kwa nguvu , tunahitaji viongozi wa upinzani wenye kukaa frontline kama ilivypkuwa miaka ya nyuma ya 2005- 2015,mobilization ya wananchi kuhusu elimu ya demokrasia , na mamlaka waliyonayo kikatiba nk.
 
Nasisi tumezidi kunamuda tuisaidie chadema Mana Kama chama kimetusemea vyakutosha

tuendelee kuwaombea kwenye kipindi hiki champito na mipango yao inayoiua ccm taratibu kwa uhakika
 
Katiba yetu ya mwaka 1977 inaweka wazi utaratibu wa mikutano ya hadhra kwa sasa mazingira yaliyopo hayana tofauti na ya yale ya mwaka 2010 na mwaka 2015 , Upinzani uache uwoga ujenge hoja na agenda inayokidhi matarajio ya wananchi waendeshe mikutano ya Hadhra katika mazingira hayahaya ya sasa , haki haiombwi haki inatafutwa kwa nguvu , tunahitaji viongozi wa upinzani wenye kukaa frontline kama ilivypkuwa miaka ya nyuma ya 2005- 2015,mobilization ya wananchi kuhusu elimu ya demokrasia , na mamlaka waliyonayo kikatiba nk.
Mkuu, nashukuru sana kwa kunielewa.

Katiba ni kweli huenda yaweka wazi utaratibu wa mikutano ya hadhara.

Lakini usisahau sheria ya vyama vingi je nayo yaweka wazi suala la mikutano ya hadhara?

Kwa mfano mikutano mikuu ya kila mwaka huweza kufanywa mara moja au mbili kulingana na katiba za vyama, jer sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 yasemaje juu ya hilo?

Lakini juzi CC ya CCM imekutana na je imetumia sheria ipi ya mikutano ya ndani au wiki mbili zilopita makamu mwenyekiti wake Kinana amezunguka kanda ya ziwa na pia waziri wa fedha kaonekana Singida akihutubia umati.

Hapo ndipo haya yanpoitwa maridhinao yanapotakiwa kuainisha masuala haya.

Sasa je, ni kifungu gani ndani ya katiba ya JMT chatoa fursa kwa chama cha upinzani kufanya mikutano ya hadhara?
 
Nadharia ni hatua mojawapo ya kufikia lengo lako, hata ukiataka kuendesha gari si utapitia kwanza nadharia au ukisoma kemia si kuna nadharia kwanza na kisha vitendo?

Hivyo weye chukulia hii ni nadharia na ikipenya na kungia kwenye fikra utafahamu nini namaanisha.

Nadharia zipo nyingi tu hii tunoiongelea hapa ni nadharia ya mabadiliko au "theory of change" kwamba yaelezea kuhusu njia fulani ya kipekee ambayo ikitumika italeta matokeo chanya na yenye ufanisi.

Angalia mfano wa dhana ya mabadiliko alotengeneza jamaa aitwa Align yaitwa Align Theory of Change.

View attachment 2358956

Hapo kwa harakaharaka ni kwamba hali ya sasa yaani "current condition" ni kwamba si nzuri kiuchumi na pia kuna mambo mengi yasofaa kabisa kinyume na matarajio ya wapiga kura.

Pili, stratejia ni kwamba tupo kwenye hatua ya kutengeneza mijadala na hii mada ni mojawapo na stratejia hizo.

Tukimaliza hii twaingia kwenye kuchukua hatua yaani "Action" na kufuatia kuangalia matokeo yaani Impact ya hatua zilochukuliwa.

Tukipita hapo yaani 2024 na 2025 tunakuwa na Vision yaani maono sahihi na twaendelea na kazi.

Muda wa nadharia umeisha, kwa sasa CCM inategemea kukaa madarakani kwa shuruti kupitia vyombo vya dola, hizo njia za kushindana kwa sera tuwaachie Wakenya ambao tayari walishapita hatua ya machafuko, na sasa wako hatua ya demokrasia ya kweli ambapo sera ndio zinapigiwa kura.

Hapa kwetu tuko kwenye hatua ya tume kuchaguliwa na kupokea maagizo kutoka kwa mwenyekiti wa CCM, wapinzani wanaenguliwa kihuni, usalama wa taifa ndio wanakuwa na fomu fake za matokeo, mawakala wa upinzani wanazuiwa kuingia kwenye vituo vya kupigia kura. Hizo njia unazopendekeza zimeshatumika sana imegeuka ni kupotezeana muda. Machafuko tu ndio iliyobaki. Kama bado watu wanaogopa kufanya machafuko ni bora kuachana na kwenda kusimama kwenye box la kura kupoteza muda.
 
Mkuu, nashukuru sana kwa kunielewa.

Katiba ni kweli huenda yaweka wazi utaratibu wa mikutano ya hadhara.

Lakini usisahau sheria ya vyama vingi je nayo yaweka wazi suala la mikutano ya hadhara?

Kwa mfano mikutano mikuu ya kila mwaka huweza kufanywa mara moja au mbili kulingana na katiba za vyama, jer sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 yasemaje juu ya hilo?

Lakini juzi CC ya CCM imekutana na je imetumia sheria ipi ya mikutano ya ndani au wiki mbili zilopita makamu mwenyekiti wake Kinana amezunguka kanda ya ziwa na pia waziri wa fedha kaonekana Singida akihutubia umati.

Hapo ndipo haya yanpoitwa maridhinao yanapotakiwa kuainisha masuala haya.

Sasa je, ni kifungu gani ndani ya katiba ya JMT chatoa fursa kwa chama cha upinzani kufanya mikutano ya hadh
Sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 namba 05 inaweka wazi utaratibu wa kuendesha mikutano ya hadhra , upinzani uache uwoga ,haki haiombwi inatafutwa kwa nguvu .......
 
Sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 namba 05 inaweka wazi utaratibu wa kuendesha mikutano ya hadhra , upinzani uache uwoga ,haki haiombwi inatafutwa kwa nguvu .......
Na sheria hiyo pia ilifanyiwa mabadiliko mwaka 2019.

Je, ni haya mabadiliko ya sheria hii ambayo ndiyo yanozuia vyama vya siasa kufanya mikutano ya kisiasa?
 
Mkuu hii mbinu alitumia Tshisekedi na alipopata upenyo tu wote mnajua alivyokigeuka chama tawala kilichopita, so ikifanikiwa huwa ni mbinu nzuri ya kumaliza adui Yako kimya kimya.

2. Kuhusu incumbency ya Samia, kwa maoni yangu dili lilivyokaa ni kwamba Samia ataendelea 2025 ila obviously kwingine kote wananchi waamue, which is a win kwa upinzani maana wameingia kwenye meza ya mazungumzo wakiwa hawana hata madiwani 10 nchi nzima so kupata wabunge hata 120+ na halmashauri za kumwaga kama 2015 hivi ni mafanikio makubwa kuelekea kuifuta CCM 2030.

Kitila Mkumbo amesema chance ni hii tu, akiingia Rais mwingine tusahau katiba mpya Wala tume huru na CCM itatawala milele. So ni bora ujifanye mjinga katiba ipatikane afu mnyooshane baadae maana hatokua na la kufanya tena.

Katiba yetu ya mwaka 1977 inaweka wazi utaratibu wa mikutano ya hadhra kwa sasa mazingira yaliyopo hayana tofauti na ya yale ya mwaka 2010 na mwaka 2015 , Upinzani uache uwoga ujenge hoja na agenda inayokidhi matarajio ya wananchi waendeshe mikutano ya Hadhra katika mazingira hayahaya ya sasa , haki haiombwi haki inatafutwa kwa nguvu , tunahitaji viongozi wa upinzani wenye kukaa frontline kama ilivypkuwa miaka ya nyuma ya 2005- 2015,mobilization ya wananchi kuhusu elimu ya demokrasia , na mamlaka waliyonayo kikatiba nk.
Hiyo ni Kweli, Kuna miaka zaidi ya Saba imepita bila ELIMU ya URAIA kutolewa Kwa wananchi.

Vijana kuanzia miaka ishirini kurudi chini hawajui chochote kuhusu HAKI ya Kuchagua na kuchaguliwa kama msingi mkuu mojawapo wa Maendeleo.

ELIMU ya URAIA ni HAKI, ipiganiwe. Ameeen
 
Tusizunguke sana sijui kuna mbinu yoyote ya kuleta katiba ama sijui CDM wajipange. Bila nchi kupinduliwa, ama wafuasi wa CDM/wananchi kuleta machafuko, tusitegemee mabadiliko yoyote ya maana, sana sana watu wengi hawatajitokeza kupiga kura.

Hiyo Kenya tunayoona wanaheshimiana ni kwakuwa kulitokea machafuko baada ya uchaguzi wa 2007. Ifahamike wakati wa Moi wakenya walikuwa waoga kuliko sisi. Ongeeni maelezo yoyote na mbinu zozote mzitakazo lakini itakuwa kufurasha genge tu, machafuko ndio yataifanya demokrasia ya nchi hii iwe bora.
Huu ndio ukweli ambao watu wanaogopa kuuzungumza. Bila mapinduzi hakuna mabadiliko. Wananchi tutakapoona tumeshindwa kuhimili mikodi ndio mabadiliko yatakapotokea, kutegemea vyama vya siasa na chaguzi ni kujidanganya.
 
Lema ameshauri CDM ijiondoe kwenye maridhiano, Ili turudi KUHESABIWA.

Naunga mkono HOJA.

Maana wakati maridhiano yakiendelea, wanaendelea kuumiza raia. Wanazidi kuzuia mikutano Eti tusubiri upuzi wa mukdala!!!!
 
Back
Top Bottom