Mjadala uliotupita: Je, kuvunja mkataba wa vifaa vya zimamoto hakutatuletea hasara ya fidia?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
138,420
2,000
CHADEMA imefanya mambo mengine yapite aidha kimyakimya ama kukosa mijadala critical ya wananchi. Baadhi ya mambo hayo ni:

Kuvunjwa kwa mkataba wa Tsh trillion moja na ushee na kampuni moja nje ya nchi (kwa wasiojua trillion moja ina masifuri 12 yaani 1,000,000,000,000/=)

Msanii wa Bongo fleva kuzindua album yake hapo jana tarehe 14. Maandalizi na matangazo yalikuwa mengi. Sijui matokeo yamekuwaje.

Ugonjwa mbaya wa corona ni kama vile Watanzania wameupotezea lakini la hasha. CHADEMA imesababisha habari zote hizi kukosa mijadala mipana.

Nawaombeni sasa muda wenu tuweze kulijadili hili.

Mwanzoni mwa wiki hii Waziri wa Mambo ya Ndani Simbachawene alitoa taarifa rasmi kuwa ule mkataba tata wa vifaa vya Jeshi la Zimamoto wa takriban Tsh. Trillion moja umevunjwa kati yake na kampuni iliyokuwa imepewa/imeshinda Hiyo zabuni. Na akasisitiza kwamba hakuna hasara tuliyopata wala tutakayopata.

Mimi nina maoni tofauti kidogo na waziri.
Kwanza nikiri wazi mimi si mjuzi wa sheria za mikataba lakini hata kama wapo wajuzi hapa, hatutaweza kuujadili mkataba kwa maudhui yake kwakuwa hatujawahi kufahamu kilichokuwa ndani yake. Labda tufanye zile za kibush lawyer tu.

Yangu ni haya hapa

Ule mkataba tumeingia hasara kubwa mpaka sasa. Wote tunatambua mkachato wa kuandaa tenda mpaka kupata wazabuni na hatimaye kusaini mikataba ulivyo mrefu, na kila hatua ni pesa.

Tulishatumia muda nguvukazi, rasilimali na pesa nyingi tu kwenye hili jambo. Hivyo tumepata hasara ya kwanza.

Mpaka kufikia kuhitaji hivyo vifaa tafsiri yake ni kwamba tuna upungufu. Hivyo kama mchakato ungeenda vema, vifaa tajwa vingefika kwa wakati na hilo ombwe la ukosefu/upungufu lingezibika na kumaliza hilo jambo. Mchakato huu umefeli, sasa kuanza mwingine ni gharama nyingine tena hizo. Tumepata hasara ya pili.

Vifaa tajwa vingekuwa vya kisasa. Hivyo kama mchakato ungeenda vema, ingekuwa ni nafasi adhimu kwa vijana wetu kwenda kujifunza maarifa mapya kwa faida ya taifa huku tukizalisha ajira mpya. Hasara ya tatu hii.

Ni wazi kabisa vifaa hivi vingekuja na mitambo ambayo ingehitaji maeneo mapya ya kuifunga. Hili lingefanikiwa Watanzania wengi wangepata ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja na wangechangia pato la taifa kwa kufanya biashara na kuleta nafuu kwenye kaya zao. Hasara ya nne hii.

Kama hili lingewezekana basi kungekuwa na michakato ya ujenzi. Hapa wakandarasi wa ndani, wataalam wa mazingira, wafanyabiashara na wahusika wengine wangepata sehemu ya kuingiza chochote kulingana na fani zao. Mkataba umesitishwa. Hasara ya tano hii.

Kwa kuvunjwa mkataba huu ukiwa hatua za mwisho umetia DOA kwenye biashara za kimataifa. Na tumeonesha umakini duni. Mahusiano ya kidiplomasia pia yanaweza kutetereka kidogo. Hasara ya sita hii.

Usiri na kutoshirikishwa bunge letu kupitia kamati husika. Kama haya mambo yangefanyika kwa uwazi na kwa taratibu tulizojiwekea. Yasingefika huku. Bunge lilifichwa hivyo wananchi walifichwa pia. Matokeo ndio haya. Hasara ya saba hii.

Ndugu waziri pengine hizi hasara hujazizingatia lakini huko mbeleni mambo yanaweza kuwa mabaya zaidi kama yule jamaa aliyepata hii tenda akiamua kwenda mahakama ya kimataifa kulalamika.

Sitaki kulisemea hili kwakuwa sifahamu maudhui ya mkataba kwenye zabuni kubwa kama hizi tena zinazohusika na jeshi ama kwa sehemu vifaa vya kijeshi kuna vitengo kama tisa ni lazima vijulishwe na vishiriki kutoa maamuzi:

Mamlaka ya Rais
Mkuu wa Majeshi
Mtunza Bohari Mkuu
Usalama wa Taifa
Mlipaji Mkuu wa Serikali (hazina)
Bunge
Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Benki Kuu
Mzabuni Mkuu Taifa

Je, kwa hatua zote za mchakato wa huu mkataba hawa wamehusishwa? Na hata sasa je wamehusishwa?

Mchakato wa kuvunja mkataba hupitia njia ileile uliyoanza nayo, huruki hatua. Je kwa uharaka huu wa kuvunja huu mkataba, hatua zote zimefuatwa?

Kwako Simbachawene,
Waziri wa Mambo ya Ndani.Jr
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
138,420
2,000
Lugola, sitaki kuamini Kama alihusika, nahisi kuna majungu sio bure
Kuna maswali ya ziada hapa
Je, taratibu za zabuni zilizingatiwa?
Je, ni kampuni ngapi ziliomba?
Je, ni ngapi zilishindanishwa?
Kama hii iliyoshinda imeonekana kuna shida.

Tatizo ni la nani hapa?

Jr
 
TOHATO

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
960
1,000
Mimi nina haya yaloko pembeni na mada.
Alafu jamaa yupo duniani tuu chaa ajabu kesi yake inaeza ikapotelea hewani.

Ila tuweke kumbukumbu vema tu kuna mtu anaeza muomea Lugalo huruma sa hivi akasahau jamaa kipind cha utawala wake alokuwa anayafanya.

Yaan haya wanayo yafanya Mku wa Mbeya, Dar, Arusha, Arumeru au Hai msiyasahau wekeni vema kwenye kumbukumbu nao kuna muda wao wa msoto hata masije waonea huruma.
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
138,420
2,000
When you are 'successful' you become happy and have bad memory
mimi nina haya yaloko pembeni na mada.
Alafu jamaa yupo duniani tuu chaa ajabu kesi yake inaeza ikapotelea hewani ...
Ila tuweke kumbukumbu vema tuu kuna mtu anaeza muomea Lugalo huruma sa hivi akasahau jamaa kipind cha utawala wake alokuwa anayafanya.
Yaan haya wanayo yafanya Mku wa mbeya,dar arusha,arumeru au Hai msiyasahau wekeni vema kwenye kumbukumbu nao kuna muda wao wa msoto hata masije waonea huruma
Jr
 
Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
10,979
2,000
1. Rais alidanganya umma kwa kusema waliingia mkataba wakati ulikuwa ni mchakato wa kuelekea kwenye Mkataba.
2. Waziri naye anatuchanganya anadai haukuwa mkataba bali mchakato wa kuelekea kwenye mkataba, lakini zaidi ya 99.9% ya maelezo yake yaongelea na kuonyesha kuwa huu ni mkataba badala ya mchakato kuelekea kwenye mkataba.

Hili linalazwa hivi sasa, lakini Time will come, litaamka usingizini na kuanza kutusumbua huko baadaye.
 
njinjo

JF-Expert Member
Feb 15, 2019
2,283
2,000
CHADEMA imefanya mambo mengine yapite aidha kimyakimya ama kukosa mijadala critical ya wananchi. Baadhi ya mambo hayo ni:

Kuvunjwa kwa mkataba wa Tsh trillion moja na ushee na kampuni moja nje ya nchi (kwa wasiojua trillion moja ina masifuri 12 yaani 1,000,000,000,000/=)

Msanii wa Bongo fleva kuzindua album yake hapo jana tarehe 14. Maandalizi na matangazo yalikuwa mengi. Sijui matokeo yamekuwaje.

Ugonjwa mbaya wa corona ni kama vile Watanzania wameupotezea lakini la hasha. CHADEMA imesababisha habari zote hizi kukosa mijadala mipana.

Nawaombeni sasa muda wenu tuweze kulijadili hili.

Mwanzoni mwa wiki hii Waziri wa Mambo ya Ndani Simbachawene alitoa taarifa rasmi kuwa ule mkataba tata wa vifaa vya Jeshi la Zimamoto wa takriban Tsh. Trillion moja umevunjwa kati yake na kampuni iliyokuwa imepewa/imeshinda Hiyo zabuni. Na akasisitiza kwamba hakuna hasara tuliyopata wala tutakayopata.

Mimi nina maoni tofauti kidogo na waziri.
Kwanza nikiri wazi mimi si mjuzi wa sheria za mikataba lakini hata kama wapo wajuzi hapa, hatutaweza kuujadili mkataba kwa maudhui yake kwakuwa hatujawahi kufahamu kilichokuwa ndani yake. Labda tufanye zile za kibush lawyer tu.

Yangu ni haya hapa

Ule mkataba tumeingia hasara kubwa mpaka sasa. Wote tunatambua mkachato wa kuandaa tenda mpaka kupata wazabuni na hatimaye kusaini mikataba ulivyo mrefu, na kila hatua ni pesa.

Tulishatumia muda nguvukazi, rasilimali na pesa nyingi tu kwenye hili jambo. Hivyo tumepata hasara ya kwanza.

Mpaka kufikia kuhitaji hivyo vifaa tafsiri yake ni kwamba tuna upungufu. Hivyo kama mchakato ungeenda vema, vifaa tajwa vingefika kwa wakati na hilo ombwe la ukosefu/upungufu lingezibika na kumaliza hilo jambo. Mchakato huu umefeli, sasa kuanza mwingine ni gharama nyingine tena hizo. Tumepata hasara ya pili.

Vifaa tajwa vingekuwa vya kisasa. Hivyo kama mchakato ungeenda vema, ingekuwa ni nafasi adhimu kwa vijana wetu kwenda kujifunza maarifa mapya kwa faida ya taifa huku tukizalisha ajira mpya. Hasara ya tatu hii.

Ni wazi kabisa vifaa hivi vingekuja na mitambo ambayo ingehitaji maeneo mapya ya kuifunga. Hili lingefanikiwa Watanzania wengi wangepata ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja na wangechangia pato la taifa kwa kufanya biashara na kuleta nafuu kwenye kaya zao. Hasara ya nne hii.

Kama hili lingewezekana basi kungekuwa na michakato ya ujenzi. Hapa wakandarasi wa ndani, wataalam wa mazingira, wafanyabiashara na wahusika wengine wangepata sehemu ya kuingiza chochote kulingana na fani zao. Mkataba umesitishwa. Hasara ya tano hii.

Kwa kuvunjwa mkataba huu ukiwa hatua za mwisho umetia DOA kwenye biashara za kimataifa. Na tumeonesha umakini duni. Mahusiano ya kidiplomasia pia yanaweza kutetereka kidogo. Hasara ya sita hii.

Usiri na kutoshirikishwa bunge letu kupitia kamati husika. Kama haya mambo yangefanyika kwa uwazi na kwa taratibu tulizojiwekea. Yasingefika huku. Bunge lilifichwa hivyo wananchi walifichwa pia. Matokeo ndio haya. Hasara ya saba hii.

Ndugu waziri pengine hizi hasara hujazizingatia lakini huko mbeleni mambo yanaweza kuwa mabaya zaidi kama yule jamaa aliyepata hii tenda akiamua kwenda mahakama ya kimataifa kulalamika.

Sitaki kulisemea hili kwakuwa sifahamu maudhui ya mkataba kwenye zabuni kubwa kama hizi tena zinazohusika na jeshi ama kwa sehemu vifaa vya kijeshi kuna vitengo kama tisa ni lazima vijulishwe na vishiriki kutoa maamuzi:

Mamlaka ya Rais
Mkuu wa Majeshi
Mtunza Bohari Mkuu
Usalama wa Taifa
Mlipaji Mkuu wa Serikali (hazina)
Bunge
Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Benki Kuu
Mzabuni Mkuu Taifa

Je, kwa hatua zote za mchakato wa huu mkataba hawa wamehusishwa? Na hata sasa je wamehusishwa?

Mchakato wa kuvunja mkataba hupitia njia ileile uliyoanza nayo, huruki hatua. Je kwa uharaka huu wa kuvunja huu mkataba, hatua zote zimefuatwa?

Kwako Simbachawene
Waziri wa Mambo ya NdaniJr
Tulielezwa ni MoU
 
Bella Ciao

JF-Expert Member
May 28, 2019
1,746
2,000
Mh lakini nasikia ule mkataba ilikuwa tu ni Memorandam of understang(Mou) kwaiyo ilikuwa ni hatua za mwanzo .. Bado ata hujajadiliwa bungeni
 
Uwazitu

JF-Expert Member
Aug 19, 2019
1,053
2,000
Mh lakini nasikia ule mkataba ilikuwa tu ni Memorandam of understang(Mou) kwaiyo ilikuwa ni hatua za mwanzo .. Bado ata hujajadiliwa bungeni

Kama ni hivyo, kwa nini Lugola alifukuzwa kazi?

Rais hawezi tofautisha MoU ( Memorandums of Understanding )na Contract?

Simbachawene, rekebisha maelezo, unaonesha kufeli mapema sana.
 
Bella Ciao

JF-Expert Member
May 28, 2019
1,746
2,000
Kama ni hivyo, kwa nini Lugola alifukuzwa kazi?

Rais hawezi tofautisha MoU ( Memorandums of Understanding )na Contract?

Simbachawene, rekebisha maelezo, unaonesha kufeli mapema sana.
Mkuu mimi ni kijana tu mdogo na wala sina ajira yoyote ndio maana nilikuwa naangalia Magufuli akimuapisha waziri mpya wa mambo ya ndani na yeye mwenyewe alisema kuwa Lugola alisaini "Memorandum of understanding".. Magufuli alinena kwa kinywa chake... Ata wewe unaweza kwenda Youtube na kujiridhisha
 
Mk54

JF-Expert Member
Dec 29, 2016
938
1,000
CHADEMA imefanya mambo mengine yapite aidha kimyakimya ama kukosa mijadala critical ya wananchi. Baadhi ya mambo hayo ni:

Kuvunjwa kwa mkataba wa Tsh trillion moja na ushee na kampuni moja nje ya nchi (kwa wasiojua trillion moja ina masifuri 12 yaani 1,000,000,000,000/=)

Msanii wa Bongo fleva kuzindua album yake hapo jana tarehe 14. Maandalizi na matangazo yalikuwa mengi. Sijui matokeo yamekuwaje.

Ugonjwa mbaya wa corona ni kama vile Watanzania wameupotezea lakini la hasha. CHADEMA imesababisha habari zote hizi kukosa mijadala mipana.

Nawaombeni sasa muda wenu tuweze kulijadili hili.

Mwanzoni mwa wiki hii Waziri wa Mambo ya Ndani Simbachawene alitoa taarifa rasmi kuwa ule mkataba tata wa vifaa vya Jeshi la Zimamoto wa takriban Tsh. Trillion moja umevunjwa kati yake na kampuni iliyokuwa imepewa/imeshinda Hiyo zabuni. Na akasisitiza kwamba hakuna hasara tuliyopata wala tutakayopata.

Mimi nina maoni tofauti kidogo na waziri.
Kwanza nikiri wazi mimi si mjuzi wa sheria za mikataba lakini hata kama wapo wajuzi hapa, hatutaweza kuujadili mkataba kwa maudhui yake kwakuwa hatujawahi kufahamu kilichokuwa ndani yake. Labda tufanye zile za kibush lawyer tu.

Yangu ni haya hapa

Ule mkataba tumeingia hasara kubwa mpaka sasa. Wote tunatambua mkachato wa kuandaa tenda mpaka kupata wazabuni na hatimaye kusaini mikataba ulivyo mrefu, na kila hatua ni pesa.

Tulishatumia muda nguvukazi, rasilimali na pesa nyingi tu kwenye hili jambo. Hivyo tumepata hasara ya kwanza.

Mpaka kufikia kuhitaji hivyo vifaa tafsiri yake ni kwamba tuna upungufu. Hivyo kama mchakato ungeenda vema, vifaa tajwa vingefika kwa wakati na hilo ombwe la ukosefu/upungufu lingezibika na kumaliza hilo jambo. Mchakato huu umefeli, sasa kuanza mwingine ni gharama nyingine tena hizo. Tumepata hasara ya pili.

Vifaa tajwa vingekuwa vya kisasa. Hivyo kama mchakato ungeenda vema, ingekuwa ni nafasi adhimu kwa vijana wetu kwenda kujifunza maarifa mapya kwa faida ya taifa huku tukizalisha ajira mpya. Hasara ya tatu hii.

Ni wazi kabisa vifaa hivi vingekuja na mitambo ambayo ingehitaji maeneo mapya ya kuifunga. Hili lingefanikiwa Watanzania wengi wangepata ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja na wangechangia pato la taifa kwa kufanya biashara na kuleta nafuu kwenye kaya zao. Hasara ya nne hii.

Kama hili lingewezekana basi kungekuwa na michakato ya ujenzi. Hapa wakandarasi wa ndani, wataalam wa mazingira, wafanyabiashara na wahusika wengine wangepata sehemu ya kuingiza chochote kulingana na fani zao. Mkataba umesitishwa. Hasara ya tano hii.

Kwa kuvunjwa mkataba huu ukiwa hatua za mwisho umetia DOA kwenye biashara za kimataifa. Na tumeonesha umakini duni. Mahusiano ya kidiplomasia pia yanaweza kutetereka kidogo. Hasara ya sita hii.

Usiri na kutoshirikishwa bunge letu kupitia kamati husika. Kama haya mambo yangefanyika kwa uwazi na kwa taratibu tulizojiwekea. Yasingefika huku. Bunge lilifichwa hivyo wananchi walifichwa pia. Matokeo ndio haya. Hasara ya saba hii.

Ndugu waziri pengine hizi hasara hujazizingatia lakini huko mbeleni mambo yanaweza kuwa mabaya zaidi kama yule jamaa aliyepata hii tenda akiamua kwenda mahakama ya kimataifa kulalamika.

Sitaki kulisemea hili kwakuwa sifahamu maudhui ya mkataba kwenye zabuni kubwa kama hizi tena zinazohusika na jeshi ama kwa sehemu vifaa vya kijeshi kuna vitengo kama tisa ni lazima vijulishwe na vishiriki kutoa maamuzi:

Mamlaka ya Rais
Mkuu wa Majeshi
Mtunza Bohari Mkuu
Usalama wa Taifa
Mlipaji Mkuu wa Serikali (hazina)
Bunge
Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Benki Kuu
Mzabuni Mkuu Taifa

Je, kwa hatua zote za mchakato wa huu mkataba hawa wamehusishwa? Na hata sasa je wamehusishwa?

Mchakato wa kuvunja mkataba hupitia njia ileile uliyoanza nayo, huruki hatua. Je kwa uharaka huu wa kuvunja huu mkataba, hatua zote zimefuatwa?

Kwako Simbachawene
Waziri wa Mambo ya Ndani

Jr
Pamoja kwamba ninasaupport harakati za Ngosha kuleta mabadiliko; lakini hili liwekwe wazi.

Mkataba ni legal binding agreement between parties na ni lazima uwe na Article of Agreement ambayo ita set forth the main purpose of the contract and powers of the entity.

The second part ni Conditions of contract ni sehemu inayo determine obligations za kila mmoja na any kind of breach, substantial performance,frustration ikitokea ni procedures gani za kisheria zitafuatwa.

Sheria za kitaifa na kimataifa zimeweka wazi vigezo vya ku Discharge of Contract ( kuvunja Mkataba ambao ulishasainiwa)

1. Discharge by Agreement
2. Discharge by Performance
3. Discharge by Breach
4. Discharge by Expiration

Kwa maelezo ya Simbachawene, Mkataba umevunjwa by Agreement( kwamba wamekubaliana kuvunja); Na kuvunja mkataba by Agreement ni lazima turudi Kwenye Conditions of Contract.

Mkataba wowote lazima uwe na Clause inayotoa ufafanuzi kama entity( taasisi) itataka kusimamisha Mkataba kabda ya Mkataba kuisha ni lazima kuwe na Remedy au Liquidated Damage kwa manufacturer or Supplier.
( lazima kuwe na malipo ya kusimamisha mkataba na wakati mwingine huwa ni malipo makubwa zaidi ya value of the contract hasa kwa mikataba ya kimataifa).

Hivyo; hasara ambaye nchi imeingia kwa boko la Kangi Lugola ipo tena kubwa sana sema Transparency imekuwa ni changamoto kwa awamu ya 5. Kuanzia kwenye tendering process, vikao vya tender board, Evaluation Committee, Preparing solicitation documents it takes a lot of money plus the loss for discharge of contract !

na shauri wabunge wa TZ walifanyie uchunguzi hili swala kujua hasara nchi iliyoingia kwa kuvunja Mkataba huo. Na uchunguzi huo ni kufuatilia upande wa Supplier, huyu atakuwa na mengi ya kusema. Aidha, Ofisi ya Attorney General ina mengi ya kusema, Paymaster General( Doto) ana mengi ya kusema !

Na je hukumu ya Kangi na timu yake imeishia wapi ? Mbona hatuoneshwi kama tunavyooneshwa ya kina Mbowe na kundi lake ? Au mahakama zipo kwa ajili ya upinzani tu tena kwa vitu visivyokuwa na msingi wowote.

Upinzani fanyieni kazi hili suala mje na majibu kuna ukakasi mkubwa sana katika hii issue. Kutuambia kwamba mkataba umeshavunjwa haitoshi, na ni kutowatendea haki watanzania.

Lazima tujue hasara tunazopata pindi tunapofanya blunders kama hizi kwa maslaha ya watu fulani fulani. Kumtumbua Kangi haitoshi, ni lazima tuone anawajibishwa kisheria na hasara zitambulike.

Upinzani hiii iwe ni ajenda yenu kwenye kampeni za uchaguzi!
 
Bella Ciao

JF-Expert Member
May 28, 2019
1,746
2,000
What is MoU?
Hapo ina maana alitia saini ya kuupitia huo mkataba ili aweze kuuelewa vizuri na baadae ukajadiliwe bungeni kama una manufaa ama lah! Alafu baadae mkataba ukikubalika ndio anatis saini ya mwisho
 
Top Bottom