Mjadala uliopo ni Minimum reforms vs comprehensive reforms

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,617
728,447
Hakuna mtanzania yeyote hivi sasa bado anadai katiba iliyopo inajitosheleza...............ubishi uliopo ni kuwa tuitie kiraka cha 16 katiba yetu......i.e minimum reforms..........na hili Bunge tu linatosha kuifanyia kazi............. au tuifumue na kuiandika sote...........................Yaani comprehensive reforms.......na hili Mkutano wa kikatiba tu ndiyo unaweza kulikamilisha na wala siyo Bunge pekee............

Kubwa katika kuamua ni wapi twende ni tujiulize hayo mabadiliko 15 yaliyofanywa na Bunge yalilenga kumjenga nani kati ya kiongozi na raia?

Ukweli ni kuwa aliyenufaika ni viongozi wa juu serikalini na CCM pekee...........ushahidi ni kuwa Sura zihusuzo utawala au the Executive kwenye katiba zimekuwa zikinenepeshwa vilivyo ikilinganishwa na zilivyokuwa sura hizo kwenye katiba tuliyorithi kutoka kwa mkoloni mwaka 1961....................viraka 15 kwenye katiba yetu vilimnufaisha mtawala na wala siyo mtawaliwa.............................

Viongozi wetu kwa kulitumia Bunge wamekuwa ni magwiji sana wa kujikweza kwa kujirundikia madaraka na huku wakitukwaza sisi kwa kutuondolea haki ya kushiriki katika kuamua hatma ya nchi hii wakati sisi ndiyo wamiliki wa hatma ya ajira yao ya kiutawala na ambayo yapaswa kuwa........................

Haya ni baadhi tu ya maeneo ya kutafakari ni wapi twende kati ya minimum reforms kama Pinda alivyotuuma sikio kuwa ndiyo mapendekezo atakayompelekea JK au kama wanaharakati wote tutakavyo kuwa....................comprehensive reforms.............

Vile vile uzoefu tulioupata kutoka kwa Tume ya Nyalali ni kuwa hata mapendekezo yao huwa hayana nguvu za sheria na watawala waweza kuyapuulizia mbali bila kuathirika kabisa lakini Mkutano wa kikatiba una nguvu ya kisheria na mapendekezo yake ni kura ya maoni tu inayohusisha raia wote ndiyo yaweza kuikataa

Hivyo tunahitaji sheria ya kura ya maoni kama sehemu ya njia ya kuipata katiba mpya...........sheria ambayo sisi hatuna............................
 

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,151
1,427
nadhani sheria ya kura za maoni tunayo ni kama ile iliyofanyika zanzibari na hata kipindi tunafanya maamuzi ya kujiunga na vyama vingi tulikuwa na kura za maoni

cha msingi hapa na cha kujiuliza ni kuwa je hawa watawala watakubali kupitisha hayo maombi? kwani sheria zilizopo zina wapa uwanja mpana wa kukubali ama kutokubali juu ya mchakato wa katiba tuitakayo ambayo kwao ni kikwazo

Ila kama itagoma nguvu ya umma huwa ni mwamuzi mzuri sana juu ya viongozi wabishi wasiokubali mabadiliko.

kwa kuwa tumeamuwa kuvuwa nguo,ni lazima kuoga hata kama maji ni ya baridi

KATIBA MPYAAAAAAAAAA KWA MANUFAAAAAAAAA YA TAIFAAAAAAAAAAAAMAPINDUZIIIIII DAIMAAAAAA
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,617
728,447
nadhani sheria ya kura za maoni tunayo ni kama ile iliyofanyika zanzibari na hata kipindi tunafanya maamuzi ya kujiunga na vyama vingi tulikuwa na kura za maoni

Ya Zanzibar ni ya huko.......................sisi huku bara hatuna sheria ya kura ya maoni..........................huo ndiyo ukweli wetu............
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom