Mjadala: Tatizo la kujieleza kwenye usaili wa kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjadala: Tatizo la kujieleza kwenye usaili wa kazi

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Sipo, Nov 26, 2009.

 1. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kuna tatizo la kujieleza wakati muomba kazi anapoenda kwenye usaili. Uzoefu unaonyesha kuwa wasailiwa wengi huwa wanachanganyikiwa na kushindwa kujibu maswali kwa ufasaha na kujikuta wanakosa kazi.

  Thread hii lengo lake ni sisi wanaJF kuelezana mambo ya muhimu ya kufanya/kuzingatia wakati wa kufanyiwa usaili.

  Karibuni


  ---------------
  phil_kabuje: Epuka lugha hizi za mwili (body languages) wakati wa kufanya usaili (interview)

  1.Epuka Kukunja mikono yako Kifuani hii huonyesha kujiamini kupita kiasi, dharau au wakati mwingine huashiria kutokubaliana na kile kinachozungumzwa

  2. Kama umesimama, jitahidi unyooke, epuka kuegamia ukuta au kupishanisha miguu (kuchora alama ya X). Kama umekaa usiegamie sana kiti kwani hii huonyesha ishara ya uvivu. Kaa ukiwa umenyooka

  3. Epuka kuwa wakwanza kukwepesha macho kwa haraka unapomuangalia anayekufanyia usaili au aliyekuuliza swali. Hii huonyesha kukosa kujiamin au tabia ya udokozi. Daima angalia mbele usiiname chini unapoulizwa maswali

  4. USITAFUNE KITU chochote mdomoni iwe pipi au vidole vyako (hasa kwa wanawake)

  5. Usionyeshe Ishara yoyote mbaya unapomzungumzia muajiri wako aliyepita (hata kama ndiye sababu ya wewe kuacha kazi)

  6. Usiwanyooshe vidole wanaokufanyia usaili

  7. Usitikise sana kichwa kupita kiasi. Ni vizuri kutikisa kichwa unapoonyesha kuelewa kile unachoambiwa, lakini mara nyingine inawezekana ukaulizwa swali la mtego ambalo hutakiwi kukubali!

  8. Usiweke mikono nyuma au mfukoni unapoingia ndani au ukiwa umesimama. Hii hunyesha hali ya kutotaka kuwa muwazi, au majivuno.

  9. Unachokizungumza kifanane na uso wako. Mfano unapozungumzia kitu kinachokufurahisha halafu una sura nzito, una hatari! Jitahidi kutoa tabasamu kila unapoulizwa swali au kuelezea kitu

  10. Usiangalie sana juu ishara ya kukumbuka kitu. Hii huonyesha kutokuwa na hakika ya kile unachokizungumza!
   
 2. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #2
  Nov 27, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kuvaa kiofisi, kufika mapema katika eneo la usahili, kujiandaa kisaikolojia hasa kwa kujiuliza maswali ambayo unahisi unaweza kuulizwa, ni vyema kuuliza watu wenye uzoefu na usahili ili wakupe michango yao, uwe na uhakika na unachokijibu, kama hujui sema 'haujui' na utakifanyia kazi, usitetemeke, kabla ya usahili vuta pumzi kwa nguvu, usiongee haraka haraka! pia usivae nguo ambazo hunamazoea nazo kiasi cha kukufanya usiwe huru!
   
 3. bht

  bht JF-Expert Member

  #3
  Nov 27, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  JP ya muhimu sana ulosema hapo....plus sikiliza maswali kwa makini, usishushe pumzi unapoulizwa swali (as if kilichoulizwa kimekuchosha), be confident, be honest (kama hujui usisite kusema, kama hujaelewa au kusikia swali vizuri), dont loose focus....
   
 4. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #4
  Nov 27, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Husipanie kujibu maswali kwa pupa, sikiliza kwa makini na wakati wa kujibu husiangalie pembeni au juu au kufikicha vidole. Waangalie wanaokusaili moja kwa moja pasipo kusita wala kupepesa macho kwa uwoga.
   
 5. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #5
  Nov 27, 2009
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tena usijifanye mjuaji,kama kuna panel ya watu watano kila mtu anakuuliza swali usijichanganye wakati wa kujibi,anza kumjibu yule aliekuuliza swali wa kwanza zen fuata wengine kila mmoja na wakati wake.
   
 6. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #6
  Nov 27, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Halafu kama kuna panelist unayemfahamu, husijifanye kumfahamu ukaanza kumchekea na kumkenulia meno, jifanye kama vile huwajui wote ni wageni kwako na wana heshima sawa
   
 7. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Kama hufahamu kingereza waambie tafadhari tumieni kiswahili
   
 8. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #8
  Nov 27, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  ni kweli kuwahi mapema eneo la tukio kunasaidia kukuandaa kisaikolojia kuliko umefika umechelewa kwanza utapanic
   
 9. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #9
  Nov 27, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  hahaha kama unaenda kufanya job na mzungu utaombaje kuongea kiswahili
  pia kuna watu wengine ni wataalam sana wa kuandika lugha kuliko kuongea na wapo wanaoweza kuongea lugha kwa ufasaha kama chiriku hivyo tunapishana sana
   
 10. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #10
  Nov 27, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,934
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Nitasema machache:

  1. Hakikisha CV yako ni yako kweli (usiandike sifa au uzoefu ambao huna!). Kama ni kazi inayotaka uzoefu, maswali mengi yatataka kutest uzoefu wako katika maswala kadhaa. Ni vema ukajiandaa vizuri kuelezea kazi ulizokuwa unafanya, mafanikio na challenges ulizokutanana nazo na jinsi ulivyozitatua.

  2. Jaribu kufahamu matarajio (requierements) ya kazi unayoiomba. Interviwer mara nyingi atauliza maswali ili kujiridhisha kama kweli you are up to the job!

  3. Jaribu kuifahamu kampuni na shughuli inayofanya (bidhaa, wateja, challenges nk). Hii itakusaidia kujibu baadhi ya maswali. Unakuta mtu anaingia kwenye interview hata jina la kampuni anayoomba kazi anashindwa kulitamka kwa ufasaha halafu eti anaomba kazi ya kuwa afisa uhusiano!

  4. Jaribu kufuatilia mambo mbalimbali yanayoendelea duniani(Current issues) na jinsi yanavyohusiana na kazi unayoomba au kampuni au tasnia inayokuhusu.

  5. Hobbies,interests etc. Mara nyingi watu wanajiandikia tu kwenye CV hata vitu ambavyo kiukweli hawana interest navyo. Ukisema unainterest na football basi hakikisha kweli unafahamu mambo kadhaa kuhusu football. Au kama unasoma novel, basi kweli iwe unasoma. Si unaulizwa angalau uelezee kwa ufupi novel uliyoisoma karibuni, unaanza kujiuma hata title au muhusika mkuu humkumbuki!

  nk, nk, nk
   
 11. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #11
  Nov 27, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wakati wa kujibu maswali kuwa brief, husitumie muda mrefu sana kujibu swali, kwa maaana usaili ni kama mtihani ukiongea sana utapoteza pointi ya msingi.
   
 12. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #12
  Nov 27, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,429
  Likes Received: 3,792
  Trophy Points: 280
  Unapokaa kwenye kiti avoid ku-lean back....
   
 13. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #13
  Nov 27, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Husionyeshe kuwa umekariri baadhi ya maswali
  that means ukiulizwa swali weka pose then ndio ujibu
  sio kwa sababu hilo swali ulishalisoma kwenye website au kwenye kitabu then unaposikia linaanza kuulizwa hata kabla muulizaji hajamaliza nawe umeanza kujibu. Acha papara
   
 14. Obhusegwe

  Obhusegwe JF-Expert Member

  #14
  Nov 27, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 232
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Samahani kaka naomba nikusahihishe kdg hapo juu naona una common error ya maneno haya... Husionyeshe inabidi useme usionyeshe, Husitumie inabidi useme usitumie, n.k n.k. Hapo H haihusiki kabisa, samahani nimeona nitoe angalizo hili kwani nimeona hizi common error zinajitokeza sana humu jf. Sorry 4 this

  Back to the topic, ni kweli kuingia kwenye intavyuu inahitaji kujiandaa kisaikolojia. Mi intavyuu ya kwanza kabisa kuna vitu kibao nilichemsha na baadae nikaja kugundua kuwa kumbe ningekuwa nimejiandaa kisaikolojia ningeweza kujibu vzr, na kazi nilikosa!! Nawashukuru wote waliotoa ushauri. Mungu awabariki
   
 15. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #15
  Nov 29, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Noted with thanks Sir!!!
   
 16. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #16
  Nov 29, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  Cha muhimu jitahidi CV yako iwe na vitu unavyovifahamu,
   
 17. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #17
  Nov 30, 2009
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,171
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Vaa nguo smartly. Kuna maxza muonekano wako pia.
   
 18. K

  Kijamani Senior Member

  #18
  Nov 30, 2009
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni mengi yametajwa kuhusu usaili.Nimefurahishwa na komenti moja ya firstlady1 nikahisi kama namfahamu kutokana na utashi wake.Firstlady1 tafadhali nitafute kupitia kijamani@hotmail.com.
   
 19. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #19
  Nov 30, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145


  Mfano mzuri tu nilikuwa tanga mwezi wa saba kulikuwa kuan Interview pale mamkla ya maji walio itwa kwa usahili walikuwa wachache sana 4 ila aliye pata job appearance and dress code was mbaya ilikuwa siyo kiofice wana JF alikuwa anamadevu kama osama shirt ya mikono mireku kakunja amenyoa kipara midevu kaiachia.

  Pili swala la muda alichelewa kwanza kama 15mins jinalake lilipoitwa kwaajili ya kuingia kwa chumba cha interview walipotaka kumwita mtu mwingine ndio akawa ametokezea na akaingia sasa hapo niambie FL1 akili yake ilikuwa imetulia kweli na akaweza kujibu vizuri na akapata kazi?? mavazi yake na mwonekano wake tu? Ilikuwaje Meza kuu inayo wasahili ilimpitiusha huyo bwana?? Pili ilikuja kugundulika elimu yake ilikuwa ndogo zaidi kuliko ya wale wengine watatu?

  Me nadhani kuna tatizo pia kwa jopo au meza kuuu inayowashili wanaoomba kazi.

  Mie kwakweli ktk swala la usahili TZ kunavituko na vimbwanga vingi sana.

  Pia walioajiliwa wengi wakuta sio elimu walizo somea na ungugunisation ni mkubwa kupita kiasi.
   
 20. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #20
  Nov 30, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kiutaalama usaili ni kama sales in marketing,pale unanadi bidhaa zako,kwa suala la kuomba unaenda kuuza sifa na uzoefu ulionao kwa kazi ulioomba yaani hapa muajiri au wakala wa muajiri ni mteja wako.hivyo hakikisha kila unachonadi ni kweli kina sifa hizo.

  jambo la muhimu sana uwe tayari kujibu kwanini unataka kufanya kazi na muajiri huyo vilevile kwani umeacha kazi ya mwanzo?

  jitahidi kujua scale za mshahara za nafasi uliomba sio tu kwa muajiri huyo muhimu katika soko la ajira sifa zako na uzoefu wako unathamani gani?

  Ukipewa nafasi ya kuwauliza swali jitahidi uulize usisime sina swali?
   
Loading...