Mjadala redio imaan: Vyombo vya habari vya Tz ni janga la taifa na Vinamchukia Kikwete live

Kusema radio hii inafanya kitu kizuri kutuchonganisha kidini sio sahihi!
kwako kuchonganishwa kwa kuwa unapata manufaa.lkn wengi tunaamini inasema ukweli na inatoa data. wewe kama chadema kanusha hizo data mbona mnakimbilia WAPO fm tu na redio imaani hata mkialikwa kukanusha mnakimbia?
 
sio suala la dini hapa ni kuwa nabii hatambuliki nyumbani kwao!Nilishawahi kupost hata kuwa Kikwete ni bora zaidi ya wengine waliomtangulia ukiondoa mwalimu!lakini nikasema kinachomharibia ni kushindwa kuwadhibiti maswahiba wake hasa kuwakana na kuwachukulia hatua za kinidhamu na kisheria wanaoiba mali za nchi hii!

usilete hoja za kitoto eti mbwa ni bora kasoro mkia
 
Tuachane na udini, mtu apimwe kwa utendaji wake.

Dini kisiwe kipimo cha utendaji, watanzania ni wamoja.

UDOM na Mandela, ulizonukuu, ni initiatives za JK?
 
Mie sio chadema wa CCM,mie ni raia ninayepima upepo kwa misingi ya haki na kweli!watu wote wana haki sawa kama ambavyo dini zote zina haki sawa!Mwanadamu hawezi kumtetea mungu kwa nguvu na vitisho bali Mungu mwenyewe ana uwezo wa kujitetea!
 
Hapo kwenye red panaposema "Vyombo vya habari vya Tz ni janga la taifa" panaweza kuwa na ukweli fulani mkuu, kama ukizingatia kuwa pana vituo vya redio vina wahariri wenye elimu ndooogo sana.

Kwamba kuna wahariri ambao hata hawajui Uislam umejengwa kwenye msingi ule ule ambao Ukristo umejengwa--yaani imani katika Mungu mmoja kwa mtizamo wa Kiyahudi, na kwamba kiukweli hizi dini mbili zina lengo linalofanana. Mpumbavu mkubwa wewe unayetafuta kupanua mwanya unaozitenga hizi dini mbili badala ya kutafuta yale yanayoziunganisha imani hizi. Furkan unaijua wewe? Taurat ya Musa unaijua wewe? Injili ya Issa bin Mariam unaijua wewe? Mjinga mkubwa wewe! Waliompigia kura Kikwete 2005 na 2010 walikuwa Waislamu peke yao? Wanaolinda Kikwete hata akiwa chooni ni Waislamu peke yao?

Una uhakika Salva Rweyemamu, na yule binti sijui nani--ahaa, anitwa Premmy Kibanga-- pale kwenye kitengo cha habari cha Ikulu, ambao wanakosa hata usingizi kusafisha mabaya ya Kikwete katika vyombo vya habari ni Waislam? Eti "maagzeti mengi yanayoripoti maagzeti hayo ni wahahariri wake wengi ni wakiristo." Mkumbwa Ally Unamjua wewe? Pale Daily News. Ni Mkristo yule?

Chambua taarifa ya habari moja-moja katika chombo cha habari kimoja-kimoja ubainishe tatizo la kihariri hapo badala ya kuzusha lawama za kijumla ambazo katika uhalisia zinaonesha tu ni kiasi gani cha ujinga unacho. Vyombo vya habari vya Tanzania vimefanya kazi nzuri sana kujenga taifa la kidemokrasia, taifa linalojitahidi kadri hali inavyoruhusu kuwa kweli na wazi.


Wadai magazeti mengi na vyombo vyingi vya habari hupotosha habari kwa makusudi.
wamesema sensa limepotoshwa huku hata wale waliokuwa wakivamiwa na polisi usiku wa manane vyombo hivi vilikuwa kimya.
wamesema ukiangalia maagzeti mengi yanayoripoti maagzeti hayo ni wahahariri wake wengi ni wakiristo

lkn wanadai hata wakenya wanavishangaa sana vyombo vyetu vya habari kwa kupindisha mambo.
walitoa mfano Mkufunzi mmoja wa MUM amedai alipoenda kanyata University, kikwete huko anapendwa sana kutokana na kuanzisha UDOM na Mandela univ, lkn vyombo vingi vya habari vya tanzania haviandiki habari hizo badala yake vinatizama vinamtizama Kikwete kama kikwete na Imani yake ya dini jambo ambalo ni janga kubwa kwa taifa
 
sio suala la dini hapa ni kuwa nabii hatambuliki nyumbani kwao!Nilishawahi kupost hata kuwa
(Kikwete ni bora zaidi ya wengine waliomtangulia ukiondoa mwalimu!lakini nikasema

kinachomharibia ni kushindwa kuwadhibiti maswahiba wake hasa kuwakana na kuwachukulia hatua za kinidhamu na kisheria wanaoiba mali za nchi hii!)

kwenye blacket hapo cjuwi unaelewa maana ya kufaulu na kushindwa kufaulu

=na kusema mpira ule bila goli kipa lingekuwa goli
je¿ nini wajibu wa kipa c kuokoa magoli

so hiyo blacket ni kushindwa kwa kikwete kuliko marais waliopita
 
mpaka sasa sijamuelewa huyu mtoa mada alikua anamaanisha nini haaeleweki kabisa

Mkuu ukiwafuatilia hawa jamaa utachanganyikiwa. Very illogical, wanalishwa maneno and then they don't do their homework.
 
Mods kama hamtaki wengine tuchangie,ni bora mpige marufuku hizi thread.Otherwise wacheni maoni ya watu.
 
sensa chini ya ccm ni safi. uchaguzi chini ya CCM ni uovu? akili nyengine ukaimbiwa na wewe ujiambie hata ukijiita msomi lkn hili mumepotoka. kesho ukisikia kanisa limekosoa sensa hata chadema watageuza upepo
''Tupoi ni Tupoi'' UAMSHO kweli vichwa maji sensa ni issue ya taifa haina dini wala chama UAMSHO kwa u tupoi wenu mmeidakia NA KUTIA UDINI,
Bila kufikiri kuwa Pamoja na issue ya sensa kuwa ya kitaifa ila ikiharibika mnaikomoa serikali ya DHAIFU maana ndo yenye DHAMANA ya usimamizi wa utekelezwaji wa mpango huo wa kimataifa (Mwisho mmejikuta hamjui mhesabiwe muwe ma KHAFIRI ama mkatae mwende segerea,Tena wala msirukie kwenye vyama vya siasa na mijadala ya DHAIFU, linyweni tu limbwata limbwatike mtumiwe tena 2015).
USHAURI: Pelekeni watoto shule kizazi kijacho wajitambue wao na mahitaji yao ya kijamii na kidini.Nyie mmeshachelewa MAANA sehemu ya akili Ya uelewa hakikui tena wala kupokea taarifa mpya.
Maana hata kujiwekea mfumo wenu wa kujua idadi yenu mmeshindwa!...,,hata makanisa UYOGA yanawashinda.! ndo mtaiweza RC?.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom