Mjadala: Nywele zangu zinazidi kuisha, nini tatizo?

simon2016

JF-Expert Member
Oct 19, 2020
593
1,669
Kwa yeyote alie mtaalamu au anajua dawa nzuri ya kukuza na kuotesha nywele basi anipe maelekezo kichwa kinazidi kushika kasi ya kipala na bado kwa kwa sasa sijapendelea kua na kipara.

Nywele zinapunguaa pembeni tuu ila katikati zipo kama zilivyoo

Ni serious kabisa kama utajisikia kutania wewe tania, ukitaka kutukana tukana ila kama una ushauri usiache kunambia

Natanguliza shukrani za dhati

20210307_175320.jpg
 
Umri ni swainiii sanaa mkuu. Alafu unapoona wazee vikongwe wanatembea na miwani mikubwaaa na mkongojo kaa ukijua mambo yalianza kama hizo nywele zako. Jikubali tu mzee hakuna mtu anakuwa tayari na uzee au umri mkubwa.
 
Mkuu kunavipara Aina 3
Cha utajiri
Elimu
Umasikini
Chakwako ni Cha Aina gani kwanza kabla ya kuanza kukupa tiba?
 
Bora zako zinakula kushoto..kulia

Mimi zangu paa lote la mbele linarudi nyuma kwa kasi ya ajabu!..cha muhimu piga para tuu no way.

Kila nikikutana na baadhi ya watu wanahisi nina kazi maalumu kule makao makuu Chamwino + V8 juu,kumbe hata mia sina
 
Mkuu jikubali kadiri umri unavyosonga wengine hupoteza nywele. Ikabili tu hiyo hali
 
Kwa yeyote alie mtaalamu au anajua dawa nzuri ya kukuza na kuotesha nywele basi anipe maelekezo kichwa kinazidi kushika kasi ya kipala na bado kwa kwa sasa sijapendelea kua na kipara.

Nywele zinapunguaa pembeni tuu ila katikati zipo kama zilivyoo

Ni serious kabisa kama utajisikia kutania wewe tania, ukitaka kutukana tukana ila kama una ushauri usiache kunambia

Natanguliza shukrani za dhati

View attachment 1719442
Mkuu wewe n8 wa kunyoa kiduku original !piga duku Hilo linyongee na dread mjanja wewe mjini
 
Na mvi kwa mbaali naziona

Jikubali tu

Kama hujaoa inabidi uoe sasa
Hiyo ni kengele imekustua

Utapishana na warembo ohooo
 
Kwa vijana wenye hatari ya nywele kupotea upara/uwalaza ulaji wa mbegu za maboga unaweza kusaidia.

Ulaji wa mbegu za maboga unasaidia pia kupunguza hatari ya tezi dume na kuicontrol kabisa.

Tukirudi kwenye upara kuna mafuta yenye mchanganyiko wa nyonyo na mafuta ya mbegu za maboga unaweza kusaidiana na ulaji wa mbegu za maboga

Ukiyapata tumia kwa miezi mitatu hadi sita halafu lete mrejesho hapa
Kwa yeyote alie mtaalamu au anajua dawa nzuri ya kukuza na kuotesha nywele basi anipe maelekezo kichwa kinazidi kushika kasi ya kipala na bado kwa kwa sasa sijapendelea kua na kipara.
 
Back
Top Bottom