Mjadala; Nini cha kufanya gari yako ikigongwa au kugonga?

Salaam wakuu, Uzi wa zamani kidogo naona umepoa. NAOMBA KUULIZA; What if umegonga/gongwa na mmoja wapo akafariki. Hapa case Kwa aliyebaki ikoje? Hususani labda Hawa waendesha pikipiki/baiskeli/guta na vitu kama hivyo amejigonga Kwa gari lako na ikatokea akaumia sana au hata kufa. Hapa case inakuwaje na malipo (kama yapo kwa mwathirika) inakuwaje! Curious to learn.
 
Mkuu ni sahihi kabisa umeelezea vyema.

Ila kumalizana mara nyingi kuna save time na usumbufu wa kufuatilia.

Ili bimayake ilipe (wewe ni third party) inabidi kuwe na court judgement(maamuzi ya mahakama kusema who was at fault. Hii ni document ambayo ni lazima kuwa nayo ili ulipwe na bima.

Ili kuipata hii inabidi usubiri si chini ua mwezi mmoja kwa mahakama zetu hizi.
Sasa mwezi mzima hutumii gari yako plus kwenda mahakamani au kumuuliza askari mwenye hilo jalada ni usumbufu sana pia wanaomba sana hela ya maji mkuu.

Watu wanamalizana sio kwamba hawataki kufuata process ila time.
Ikifika mwezi wa nne, miaka 4 inakamilika nikiwa ninasubiri siku ya kuitwa mahakamani kutoa ushahidi. Tuligongwa magari 5 na lori.

Mhusika aliyekuwa anasimamia shauri hilo alisema, baada ya taratibu za kutoa maelezo na kadhalika, kuwa faili limepelekwa kwa mwanasheria wa Serikali ili kufungua mashtaka.

Alikuwa ana kauli yake hiyo sasa: "namba yangu ya simu hii, kwa lolote, unicheki".

Gari langu lishagongwa na kuharibika mbele na nyuma, na rushwa nitoe.....

Ni ngumu sana kwangu mimi kuiamini hiyo taasisi.
 
Niligongwa ubavuni mlango wa nyuma kushoto, kwenye junction,nilionyesha ishara ya kukata kona, kuna jamaa akaja mzima mzima ametanua kushoto kwangunikamuona kwenye side mirror nikafunga brake lakini kwa kua alikua na kasi akabamiza ubavuni. Ilikua mida ya usiku.
Mzee baba panick nikashuka kwenye gari kwa mbwembwe nikimfata jamaa aliyenigonga, koromea sanaa. jamaa akasema nishapata ajali kama hizi mara nyingi tu ila nasamehe. dizaini alikua anataka yaishe, mimi komaa sana, wananchi washakusanyika hapo.
Fikra zikanirudi. vioo vilikua wazi, Ndani kulikua na simu na mazaga mengine! Halahaulaa.
Mzee baba nikaingia kwenye gari ghafla na kuondosha, huku nikaugulia maumivu ya kuibiwa simu.
Nimejifunza panick ni mbaya sana.
 
Kitu muhimu kufahamu inapotokea ajali ni kukaa mbali na akili ya kupanic inapotokea ajali.
 
Ikifika mwezi wa nne, miaka 4 inakamilika nikiwa ninasubiri siku ya kuitwa mahakamani kutoa ushahidi. Tuligongwa magari 5 na lori.

Mhusika aliyekuwa anasimamia shauri hilo alisema, baada ya taratibu za kutoa maelezo na kadhalika, kuwa faili limepelekwa kwa mwanasheria wa Serikali ili kufungua mashtaka.

Alikuwa ana kauli yake hiyo sasa: "namba yangu ya simu hii, kwa lolote, unicheki".

Gari langu lishagongwa na kuharibika mbele na nyuma, na rushwa nitoe.....

Ni ngumu sana kwangu mimi kuiamini hiyo taasisi.
Du! Kwahio gari bado ipo Polisi inashikiliwa hadi leo?
 
Salaam wakuu, Uzi wa zamani kidogo naona umepoa. NAOMBA KUULIZA; What if umegonga/gongwa na mmoja wapo akafariki. Hapa case Kwa aliyebaki ikoje? Hususani labda Hawa waendesha pikipiki/baiskeli/guta na vitu kama hivyo amejigonga Kwa gari lako na ikatokea akaumia sana au hata kufa. Hapa case inakuwaje na malipo (kama yapo kwa mwathirika) inakuwaje! Curious to learn.
Swali zuri ngoja tusubiri majibu
 
Aisee mimi sikugonga wala kugongwa ila gari yetu iligonga nguzo barabarani.

Aisee mziki wa kule police sio wa mchezo ila shughuli iko zaidi TANROADS kama ukiwa umeharibu miundombinu yao na watu wengi hawajui hili,yaani pesa utakayotajiwa unaweza ukazimia.

Nilikuta magari pale Tanroads jamaa wameyatelekeza baada ya kushindwa kulipa uharibifu walioufanya kwny miundombinu kwny ajali mbalimbali.

Nina mfano hapa ila hauna uhusiano na ajali,Kuna jamaa wa Fuso yeye alipata Breakdown highway akamwaga oil barabarani aliambiwa alipe Tsh. 3mil kwa uharibifu wa lami.

So wkt ajali inatokea muwe mnaomba kusiwe na uharibifu umetokea kwny miundombinu ya Tanroads.,hakika utalichukia gari lako na kujuta nani alikutuma ulinunue.
Iyo kumwaga oil ni ishu nyingine,
 
Pana jamaa aligonga Ford Bantam maeneo ya Ngarenaro hapo ile Bantam body yake ni chuma yeye alikua na Alphard kwa alivyokaona kagari kadogo alijua Bantam ndio imeumia maana aliivaa hakuona kuwa mataa yameruhusu upande mwingine gari yake ndio imeharibika anaomba msamaha tuongee nikamwambia wewe nenda katengeneze gari yako sihitaji kulipwa hii ni pick up mibonyeo itakutana nayo tu...labda niwe nimechoka au iwe ajali kubwa hivi vya michubuko huwa nawaambia tembea tuu na hawaamini inaonekana wao wakiguswa wanalipisha watu...ukizoea kulipisha utakuja kulipishwa na hautakuja kuamini utakavyokomaliwa...
 
Hakuna watu washenzī na wenye urasimu kama bima

Ndio maana watu wanamalizana kishkaji tu
 
Back
Top Bottom