Mjadala; Nini cha kufanya gari yako ikigongwa au kugonga?

Kuna Mama mmoja aligongwa na Mzee basi bana Mama anataka aende kwa Mchina kasehemu kenyewe kadogo sana.
Mzee akampa 50,000 akagoma, nikazichukua nikapanda gari la huyo Mama tukafika Mwenge nikachukua wale mafundi wakasema mbona hapa twaosha tu panakuwa safi....
Kweli bana wakaosha tu nikawapa 15,000
Yule mama alisonya sana

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Aisee kumbe ukikwaruza unaweza kuosha pakangaaa kabisa??
 
Safi sana huu ndo ubinadamu

Sasa kuna mtu atauliza unalipa bima ina kazi gani?
Kuna kitu kinaitwa EXCESS kwenye bima. Hiki ni kiwango wewe unachangia kwenye matengenezo iwapo gari yako itapata ajali. Kwa Mimi ni around 300,000. Sasa ukipata ajali gharama zikawa 1m bima watatoa 700,000 na wewe 300,000. Sasa iwapo gharama za matengenezo ni chini ya 300,000 bima haitatoa chochote utalipa wewe mwenyewe. Hii ndio sababu viajali vidogovidogo mtu anakukomalia kwasababu bima haitamlipa. Hapa nazungumzia bima kubwa
 
jeuri ndugu yake kusudi
Kuna jamaa alikwarua gari ya mwenzake akavunja taa ya mbele wakati anapaki baa

Aliyepasuliwa taa akataka jamaa amlipe bei ya taa na ufundi wamalizane
Mshkaji akagoma akasema ita trafiki waje kupima atalipwa na bima na ndio maana amelipia bima gari yake
Mgongwaji akaondoka...... jamaa alipomaliza bia zake ile kutoka akakuta taa zote zimevunjwa halafu jamaa hamjui
 
Back
Top Bottom