Mjadala: Mbwana Samatta ndio mchezaji Bora wa muda wote Tanzania

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,876
7,366
Katika soka la Tanzania vimepita vizazi mbalimbali Kama kina lodgar Tenga, Sunday Manara, King kibaden, Mwamedi Mwameja, Edbily Lunyamila na hivi karibuni Juma Kaseja.
Lakini kwangu Mimi japo vizazi vingi sijaviona hapo killingana na mafanikio yao niseme wazi kwangu Mbwana Samatta ndio mchezaji wangu Bora wa muda wote Tanzania
Kwanini? Hizi hapa ni sababu zangu
Napima kwa mafanikio
--Mbwana Samatta ndio mchezaji wa Kwanza kushinda Africa champions league akiwa na TP Mazembe
--Samatta ndio mchezaji pekee wa Tanzania kuwa mfungaji Bora wa Africa champions league mwaka 2015
--Samatta ndio mchezaji pekee wa Tanzania kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Africa(wanaocheza ligi ya ndani) mwaka 2015
--Samatta ndio mchezaji pekee ya Tanzania kuchezaji Ueropa league na anabahatika kufika hadi hatua ya Robo fainali
Changamoto kubwa inayomkabili Samatta ni kupata mafanikio na Taifa stars Kama Messi anavyoangaika na Argentina

Mjadala uko wazi Kila mtu anamtazamo wake ila jitaidi ukija kuchangia njoo na Facts sio porojo za vijiwezi
Toa facts kwanini flani ni Bora
IMG_20151109_173923.jpg
12407463_1651933801734351_1469028646_n.jpg
SAMATTA%2B2.jpg
photonews-10733519-102_1535055748.jpg
 
Huu mjadala niliusikia clouds, au Edgar or kotinyo ndo kapost?anyway kwa kizazi hiki yeye ndo taa ya soka la Bongo
 
Mbwana anakipaji lkn si kile cha kutisha, ila uzuri wa Mbwana alijitambua anataka nini akajituma hatimaye Mungu akampa. Ila tokea nianze kuangalia mpira Kuna watu na wakubali kuliko Samatta walikuwa na vipaji vikubwa lkn hawa kujitambua wala kujituma mtu kama Lunyamila, Boban, Chuji hawa watu kwangu walikuwa hatari, ila ujinga wao na kutojitambua kwao waliona soka la bongo wamemaliza.
 
Hilo halina ubishi.....labda aje kutokea mwingine zaidi yake na mwenye record kumzid yeye.....lkn kwa sasa yeye ndo bora
 
Katika soka la Tanzania vimepita vizazi mbalimbali Kama kina lodgar Tenga, Sunday Manara, King kibaden, Mwamedi Mwameja, Edbily Lunyamila na hivi karibuni Juma Kaseja.
Lakini kwangu Mimi japo vizazi vingi sijaviona hapo killingana na mafanikio yao niseme wazi kwangu Mbwana Samatta ndio mchezaji wangu Bora wa muda wote Tanzania
Kwanini? Hizi hapa ni sababu zangu
Napima kwa mafanikio
--Mbwana Samatta ndio mchezaji wa Kwanza kushinda Africa champions league akiwa na TP Mazembe
--Samatta ndio mchezaji pekee wa Tanzania kuwa mfungaji Bora wa Africa champions league mwaka 2015
--Samatta ndio mchezaji pekee wa Tanzania kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Africa(wanaocheza ligi ya ndani) mwaka 2015
--Samatta ndio mchezaji pekee ya Tanzania kuchezaji Ueropa league na anabahatika kufika hadi hatua ya Robo fainali
Changamoto kubwa inayomkabili Samatta ni kupata mafanikio na Taifa stars Kama Messi anavyoangaika na Argentina

Mjadala uko wazi Kila mtu anamtazamo wake ila jitaidi ukija kuchangia njoo na Facts sio porojo za vijiwezi
Toa facts kwanini flani ni Bora
View attachment 922752View attachment 922754View attachment 922755View attachment 922756
Mbwana Samatta hajayafikia mafanikio ya kina Tenga na hata mafanikio ya kina Nsajigwa na kundi lake.
Ukweli uko hapa.
Kina Tenga na wenzake walicheza fainali za AFCON.
Kina Nsajigwa na wenzake walicheza fainali za CHAN na kubeba kombe la challenge
Huyu Samatta na wenzake hawajaleta hata kikombe cha chai
Usilinganishe watoto na wanaume.
 
Vizazi vya soka vya zamani vilikuwepo vye uwezo kumshinda Samata, tatizo lao wao waliamini mafabikio ni kuchezea Yanga na Simba tu, hivyo walivyofika kwenye hizo timu ndoto ikawa imefanikiwa na hawakujituma zaidi, kuna wengine waliwahi hata kuchukuliwa na timu za nje lakini wao waliona Yanga na Simba ndo sehemu sahihi kwao hivyo vipaji vyao vikapotelea hapo.Wengine walilewa tu sifa za hapa na pale za kununuliwa pombe na kupata wanawake nje ya hapo hawakuhitaji kingine zaidi waliona wamemaliza kila kitu.

Mbwana Samata alichowashinda wengi ni ndoto zake kuwa nataka kufika sehemu fulani na kuwa fulani, angekuwa mwingine kwa namna Samata alivyokuwa anasifika pala TP MAZEMBE mpaka anatungiwa nyimbo mpaka anakuwa mchezaji bora wa Africa na pesa aliyokuwa anapata pale angesema hapa ndio penyewe angebweteka hapo, lakini Samata huyu aliona hiyo haitoshi anataka zaidi ya hapo hivyo akaenda ulaya Krc Genk, huko nako kwake hapatoshi hivyo anajituma afike zaidi ya pale..kwa vyovyote vile mtu mwenye ndoto na anayetamani kuzifikia ndoto zake hukuakionyesha juhudi zake ni bora kuliko yoyote yule hata angrkuwa ni mcgezaji mzuri kiasi gani lakini hana ndoto huyo hawezi kuhesabika wala kuandikwa popote pale
 
Mbwana anakipaji lkn si kile cha kutisha, ila uzuri wa Mbwana alijitambua anataka nini akajituma hatimaye Mungu akampa. Ila tokea nianze kuangalia mpira Kuna watu na wakubali kuliko Samatta walikuwa na vipaji vikubwa lkn hawa kujitambua wala kujituma mtu kama Lunyamila, Boban, Chuji hawa watu kwangu walikuwa hatari, ila ujinga wao na kutojitambua kwao waliona soka la bongo wamemaliza.
Boban kacheza UEFA champions League ujue lakini tayari ana silver wear ya kombe la challenge unamlinganisha vipi na Mbwana Samatta ambaye hajafikia hivyo vitu
 
Mbwana Samatta hajayafikia mafanikio ya kina Tenga na hata mafanikio ya kina Nsajigwa na kundi lake.
Ukweli uko hapa.
Kina Tenga na wenzake walicheza fainali za AFCON.
Kina Nsajigwa na wenzake walicheza fainali za CHAN na kubeba kombe la challenge
Huyu Samatta na wenzake hawajaleta hata kikombe cha chai
Usilinganishe watoto na wanaume.
Hata kina Tenga hawajafikia Mafanikio ya Bwana Samata, maana Tenga hajawahi kuwa mchezaji bora Afrika, hao kina tenga hawajawahi kuwa wafungaji bora afrika, hao wakina tenga hawajawahi na timu zao kufika walau nusu fainali ya Club bingwa afrika....huyo dogo kwa mafanikio yuko mbali sana
 
Kwa mafanikio yes you maybe right..

Lakini kwa burudani ya soka uwanjani, aisee hapana...
Sahihi kabisa kwa mafanikio kweli anaongoza lakini kwa ubora na kusakata soka hapana...kuna vichwa vilipita hapa tz hata vingekuwa ulaya vingesumbua tu kama kina Hussein Aman Masha,Hamis Thobias Gagarino, Sanif Lazaro, Peter Tino Stephen Musa.....nk
 
Kwenye National team hata robo hajawafikia.
Ndiyo maana Maradona anaheshimika sana Argentina kuliko Messi kwa sababu alileta kombe nyumbani

Back
Top Bottom