MJADALA MAALUM: Kila Halmashauri/Manispaa itakiwe kuwa na EMS na Fire Brigade yake?

Kaka kama wazo ni kuokoa maisha basi tuanze na VIFO vya MAMa na MTOTO, kwani naamini hawa wanaohitaji Emergency ni wachacche sana kuliko wakina mama na watoto wano kufa wakati w akujifungua na ujauzito, TUIMARISHE HUMA HII YA MAMA KWA MTOTO!

so unafikiria kuleta huduma hii kwenye halamshauri na karibu zaidi na wananchi kutahatarisha afya ya mama na mtoto na hakutasaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto?
 
Decentralisation ya governing system imakuwa inapigiwa kelele sana na kwa miaka sasa, lakini kwa sababu wanazozijua wao wakubwa wameamua kuweka pamba masikioni. Haiwezekani karibu kila kitu kinasimamiwa na ofisi moja. Ukiwa kwenye mikoa ya Rukwa, Kigoma, au hata upande wa West Kilimanjaro ndio unaona umuhimu wa decentralisation.
 
we need to walk before we can run...,to put it bluntly hata kutambaa hatujaanza..!!!!

Cha kufanya ni kuongeza punda baiskeli na bajaji za kuwabebea wajawazito wetu.., na huko wanakuondea hata kitanda wala huduma hakuna..., anyway watalala kwenye floor
 
Hivi unajua kwamba kuna baadhi ya watu hawajawahi hata kuwa na simu zile za dial lakini walitoka kutokuwa na simu na wakaenda kuwa na Ipads! Hatua za maendeeleo si lazima ziende 1, 2, 3 , 4.. wakati mwingine (na mara nyingi) baadhi ya jamii huruka kutoka 1.... 7.. so si lazima tupitie kwenye vibajaji na baskeli tunaweza kwenda moja kwa moja kwenye chopa!
 
Mwanakijiji angalau ungetoa estimates za manispaa na halmashauri za wilaya (mapato) halafu ungeweza kujua kama wanaweza kuanzisha EMS na fire.

Sasa, nikianza hili lote itabidi nianze kufanya utafiti na kukusanya takwimu mbalimbali, kuzicchambua n.k hili ni wazo tu (concept) ambalo wahusika ambao wakiwa interested wanaweza kuliendeleza na kuona kama linawezekana. Nilipopendekeza kuanzishwa kwa Polisi Kanda hasa kwa Dar sikutoa mapendekezo ya mfumo wowote bali lilikuwa wazo, likaangaliwa na kufikishwa kwa wahusika na wakalijaribisha na sasa limeonekana kufaa; limetumika hadi Tarime. So, si wakati wote unapotoa wazo fulani basi ni lazima ulifanyie kazi zote wewe mwenyewe! Lengo ni kuinspire tu watu wengine na wao walio katika nafasi zaidi wanaweza kuona wanaweza kwenda nalo vipi.

Namaanisha kama zinatosha kuanzisha huo mpango.

Nilikuelewa ndio maana ya swali langu - ni lini na wapi kodi zimewahi kutosha kufanya kila kitu. Suala zima ni kuhoji yote hayo kwa mfano jinsi ya kufinance vitu kama hivi (Si lazima iwe kodi peke yake kama swali lako linavyodokeza), kama kuna haja ya kubadili matumizi fulani fulani, n.k La maana ni kuwa wanapokaa watu na kusema tuone inawezekna vipi katika mazingira mbalimbali ya nchi yetu basi swali linalofuatia ni jinsi gani ya kugharimia na nina uhakika TZ inao watu wenye vichwa vya kutosha tu kufikiria namba mbalimbali ya kufinance.

a. Imagine kwa mfano katika kila halmashauri, kila mtu mwenye kiwanja chenye nyumba/jumba atalipa kodi fulani kwa ajili ya "Emergency Services". Sema kwa haraka tu kwamba kwa mwaka wanalipa Sh 10,000 tu. Mji una nyumba zinazokidhi hili zipatazo 30,000. Ina maana kwa mwaka halmashauri hiyo itakusanya 300,000,000. Sasa shilingi milioni 300 si kidogo kwa source moja tu na nimeweka kiwango cha chini sana and very reasonable na kinaweza kutofautishwa kati ya majengo ya makazi na majengo ya biashara.

b. Fikiria kwamba kila biashara katika halmashauri ambayo inatoa bidhaa na huduma mbalimbali itatozwa shs 250 tu kwa kila bidhaa au huduma inayozidi shilingi 25,000 (flat fee) kwa ajili ya huduma ya dharura (EMS na Fire) kila siku kiasi gani kinaweza kukusanywa? Imagine biashara ziko 200 tu na kila moja inauza vitu 50 tu kwa siku. Kwa siku hizo biashara zitakusanya shilingi milioni 2.5; kwa mwezi 75 milioni na kwa mwaka milioni 900!!!

Ni mifano ya juu juu tu of course lakini inajaribu kuonesha tu kuwa tukiamua kuwa na kitu kama hiki si vigumu kuweza kukiendesha hata kwenye halmashauri ndogo kabisa!

Uzuri wake ni kuwa mnapokuwa na "local financing" ina maana wananchi wanaweza kudai huduma vizuri na vyombo hivyo vinaweza kuwajibishwa na wananchi wenyewe.
 
Watanzania tuna ugonjwa wa kuogopa gharama kabla ya kufikiria kwanza umuhimu wa jambo. Ugonjwa huu unaanzia kwa viongozi wetu mpaka kwa mwananchi wa kawaida. Hata Mwl. Nyerere amewahi kuoongelea katika mojawapo ya hotuba zake wakati akieleza umuhimu wa kutoa muda wa kutosha kwa wanachama wa ccm kuwatafakari na kuwachambua watu waliojitokeza kuteuliwa kuwa wagombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya ccm. Kwa mujibu wa Mwl. Nyerere ni kwamba wazo hilo lilikataliwa na viongozi waandamizi wa chama kwa kisingizio kuwa ni gharama na gharama yenyewe eti ni chama kulazimika kuwalipa wajumbe posho mara mbili. Mwl. Nyerere aliwashangaa sana watu wazima kutoa sababu hiyo na ndipo alipowaeleza kwamba kama wazo lake lina mantiki na muhimu basi walichopaswa kufanya ni kuona ni namna gani wanaweza kulitekeleza na siyo kusingizia suala la uwezo wa fedha.

Nimeamua kurejea suala hili la Mwl. Nyerere kwa sababu linafanana kwa kiasi kikubwa na hoja yako kwamba kwanza tujadili umuhimu wa jambo lenyewe then tukiridhika na kukubaliana nalo tuone ni namna gani tunaweza kumudu kulitekeleza. Binafsi nimekuwa muumini sana wa DECENTRALIZATION POLICY kwa maana kwamba mambo mengi hapa nchini hayaendi mbele kwa sababu yamehodhiwa na dude linaloitwa serikali kuu. Kila jambo command lazima itoke Dar es Salaam. Halmashauri za Wilaya zingepewa nguvu na capacity ya kutosha, nchi hii ingekuwa mbali sana kimaendeleo. Hata suala hili unaloongelea MM nalo linaingia kwenye hoja hii na nimeona namna wenzetu wa Afrika Kusini walivyoimaisha local governments zao kiasi kwamba sasa imekuwa kama no mashindano katika suala la kujiletea maendeleo.
 
Huu mjadala unaanza kunikumbusha ule mjadala wa daraja linalounganisha bara na visiwani.

Lililotolewa lilikuwa wazo (concept kama alivyosema Mwanakijiji) tu lakini watu walidai details utadhani Mwanakijiji ndiyo mkandarasi.

Nilichogundua ni kwamba watu wengi hawana proactive thinking.
 
Yule mkurugenzi wa halmashauri ya Moshi mjini alitenga 15Millioni kwajiri ya chai na vitafunwa na bajeti ikapita. BAdo tunadai hakuna fedha????
Tumewaachia watu wasio na maono wala njozi za kutuondoa hapa tulipo watrace njia na kutuongoza kazi kwetu.
Tutafika kweli??
Pia,naamini kwamba vikosi vya zima moto na uokoaji si jambo ililo vichwani mwa Viongozi wetu wa kitaifa na hata Wabunge wetu.
Wabunge zaidi ya 90% hawajui wajibu wao, akili zao zimegusa glass ceiling, hawawajibiki kwa waliowachagua au hawaoni jambo hilo litawapa ulaji kivipi.

Pesa Tanzania siyo Tatizo hata kidogo tatizo ni vichwa vya watu tuliowakabidhi nchi.

Kwa kawaida nchi inajenga Economic structure ndipo iimarishe Social structure.

Sisi Tanzania tunalazimisha kuwa na high social Structure kabla ya kujenga Economic structure.

Tunajenga majumba yanayo hitaji maji umeme 24/7 wakati umeme ni wa mgao,maji tunasubiri mvua inyeshe.

Tunanunua magari ya kifahari na aghari sana wakati barabara nzuri hakuna

Tuna import misosi yenye sumu za viwandani kutoka nchi nyingine na kuiga kula kama nguruwe wakati huo huo hatujengi hospitali nzuri zenye uwezo wa kutibu magonjwa ya shibe.

Tunaangamia kama Taifa kwa sababu tumewaachia watu wasio na maarifa watuongoze.

Vifo vya Watanzania ni Mradi waMabilioni wa kitaifa, wanaofaidi ni Wabunge,Mawaziri, Idara ya Mahakama,Rais na Ikulu na watendaji ndani ya serikali. Kwa kila Mtanzania anaye kufa kwa kukosa huduma kuna TSHS Millions kadhaa zimeingia isivyo halali kwa MH fulani ndani ya serikali ya CCM. Sisi tukiacha kufa njaa itawaingilia hadi vyumbani kwa wake zao.

kaka

pesa za mishahara hakuna

msd taaban

wewe unazungumzia haya mambo haya?
 
Watanzania tuna ugonjwa wa kuogopa gharama kabla ya kufikiria kwanza umuhimu wa jambo. Ugonjwa huu unaanzia kwa viongozi wetu mpaka kwa mwananchi wa kawaida. Hata Mwl. Nyerere amewahi kuoongelea katika mojawapo ya hotuba zake wakati akieleza umuhimu wa kutoa muda wa kutosha kwa wanachama wa ccm kuwatafakari na kuwachambua watu waliojitokeza kuteuliwa kuwa wagombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya ccm. Kwa mujibu wa Mwl. Nyerere ni kwamba wazo hilo lilikataliwa na viongozi waandamizi wa chama kwa kisingizio kuwa ni gharama na gharama yenyewe eti ni chama kulazimika kuwalipa wajumbe posho mara mbili. Mwl. Nyerere aliwashangaa sana watu wazima kutoa sababu hiyo na ndipo alipowaeleza kwamba kama wazo lake lina mantiki na muhimu basi walichopaswa kufanya ni kuona ni namna gani wanaweza kulitekeleza na siyo kusingizia suala la uwezo wa fedha.

Nimeamua kurejea suala hili la Mwl. Nyerere kwa sababu linafanana kwa kiasi kikubwa na hoja yako kwamba kwanza tujadili umuhimu wa jambo lenyewe then tukiridhika na kukubaliana nalo tuone ni namna gani tunaweza kumudu kulitekeleza. Binafsi nimekuwa muumini sana wa DECENTRALIZATION POLICY kwa maana kwamba mambo mengi hapa nchini hayaendi mbele kwa sababu yamehodhiwa na dude linaloitwa serikali kuu. Kila jambo command lazima itoke Dar es Salaam. Halmashauri za Wilaya zingepewa nguvu na capacity ya kutosha, nchi hii ingekuwa mbali sana kimaendeleo. Hata suala hili unaloongelea MM nalo linaingia kwenye hoja hii na nimeona namna wenzetu wa Afrika Kusini walivyoimaisha local governments zao kiasi kwamba sasa imekuwa kama no mashindano katika suala la kujiletea maendeleo.
Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam ina polisi wake, ina fire Department yake na inaweza kuwa na EMS, inaweza pia ika outsource hizo services.
Ukitaka kuja polisi wa Dar walivyo, angalia avatar ya king kong.
Hospitali za wilaya, barabara, sewage system, umeme n.k vyote hivyo vinaweza kuwa chini ya Halmashauri, na wana uhuru huo.
Angalieni quality za hizo services wakuu, halafu ndiyo tuseme tatizo ni mawazo , mipango au fedha?
Mimi naona tatizo ni fedha, either upatikanaji au matumizi.
 
Madela umesema kitu kizito vile vile; kinachoendelea ni kama mradi mmoja hivi. Ninachoogopa ni kwamba ukiliachilia jambo hili kwenye serikali kuu basi watakaonufaika ni vibosile fulani hivi. SIjui kama watu wamewahi kujiuliza ni kwanini msafara wa Rais unakuwa na ambulance? Jibu watakalokupa hawawezi kufikiria kuwa kila Mtanzania naye anastahili hivyo hivyo!!
 
Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam ina polisi wake, ina fire Department yake na inaweza kuwa na EMS, inaweza pia ika outsource hizo services.

Una uhakika Jiji la Dar lina "Police wake"; yaani kikosi cha kusimamia masuala ya usalama wa raia na mali zao na kuzuia uhalifu? au unazungumzia "askari wa jiji" ambao siyo "polisi"? Fire department ya jiji la Dar ina ukubwa gani kulinganisha na mahitaji ya jiji la Dar? EMS kwanini haipo hadi sasa?

Ukitaka kuja polisi wa Dar walivyo, angalia avatar ya king kong.
Hospitali za wilaya, barabara, sewage system, umeme n.k vyote hivyo vinaweza kuwa chini ya Halmashauri, na wana uhuru huo.

The operative word ni "vinaweza... kwanini haviko? Sheria na mfumo umevifanya hivyo?

Angalieni quality za hizo services wakuu, halafu ndiyo tuseme tatizo ni mawazo , mipango au fedha?
Mimi naona tatizo ni fedha, either upatikanaji au matumizi.

Ni zaidi ya fedha; uongozi, maono, uadilifu, uthubutu, mipango n.k Vinginevyo, unaweza kuwa unaamini pia tatizo la ATCL ni fedha...
 
Una uhakika Jiji la Dar lina "Police wake"; yaani kikosi cha kusimamia masuala ya usalama wa raia na mali zao na kuzuia uhalifu? au unazungumzia "askari wa jiji" ambao siyo "polisi"? Fire department ya jiji la Dar ina ukubwa gani kulinganisha na mahitaji ya jiji la Dar?
Nina uhakika, kwani askari wa jiji kazi yake ni nini? Askari wa jiji siyo kama States walivyo na city code enforcers, ni askari anayeweza kukukamata na kukufikisha mahakamani. Tatizo ni moja kuwa Dar askari wake hawapelelezi makosa ya jinai, lakini wanaweza kukukamata kama wewe ni kibaka.
Pia Dar hawana SWAT Squad, lakini hiyo wakitaka pia wanaweza kuanzisha, depending on the laws enacted. Pia hawawezi kusimamia Traffic. Lakini ni polisi kama polisi wengine. Hata vyuo vikuu navyo vina polisi wake, tofauti ni jurisdiction tu.
Kwanini hawana EMS? They can if they want!!, it's not like you are bringing something new, these things are already in the paperwork, vinasubiri execution tu.
Kuna mji kama Houston, ambapo kuna watu wa kawaida tu wanamiliki ambulance na kuzikodisha city of Houston, wengine ni watanzania ninaowajua.... this is another way!.
There are so many ways these things can be done, ila kwetu sisi tunadhani kwamba labda wabongo hawajui hizi systems.
Kwa halmashauri ya jiji kama la Dar kuwa na Police force inayomiliki silaha, kumiliki ambulances na fire trucks ni mzigo ambao hawauwezi, they are a failure. hata stendi kuzisafisha hawawezi, madawati kwa wanafunzi hamna,sidhani hata kama jengo la halmashauri ya jiji lina vyoo vya kuvuta.
 
Well siyo Polisi ni code enforces; siye tunazungumzia Polisi wanaohusika na makosa ya jinai; kwa sheria yetu hili ni jukumu la Jeshi la Polisi la Tanzania.

Pia Dar hawana SWAT Squad, lakini hiyo wakitaka pia wanaweza kuanzisha, depending on the laws enacted. Pia hawawezi kusimamia Traffic. Lakini ni polisi kama polisi wengine. Hata vyuo vikuu navyo vina polisi wake, tofauti ni jurisdiction tu.

Hata vyuo vikuu vina Polisi lakini ni Polisi wale wale wa Jeshi la Polisi; wale wengine ni walinzi tu na wana usalama hawana nguvu ya polisi na pendekezo ambalo tunalo hapa linahusiana hata na hilo lakini haiwezekani tu kuanzisha polisi bila kubadilisha sheria iliyopo.

Kwanini hawana EMS? They can if they want!!, it's not like you are bringing something new, these things are already in the paperwork, vinasubiri execution tu.

Vingine, haviwezekani hadi ubadili sheria. Na of course sileti kitu kipya... ni kitu ambacho tayari kinafanyika na kinaweza kufanyika ni kujaribu kuongeza msukumo. We're not reinventing the wheel, but we're trying to have the wheel work for us too!
Kuna mji kama Houston, ambapo kuna watu wa kawaida tu wanamiliki ambulance na kuzikodisha city of Houston, wengine ni watanzania ninaowajua.... this is another way!.

Nimelidokeza hilo kwenye original post.

There are so many ways these things can be done, ila kwetu sisi tunadhani kwamba labda wabongo hawajui hizi systems.

Not at all; kama kujua hakuna kitu ambacho watu wetu hawakijui; tunachozungumzia kwanini hawakifanyi. Kujua kunasaidia nini kama hufanyi; watu hawajisifii kujua!

Kwa halmashauri ya jiji kama la Dar kuwa na Police force inayomiliki silaha, kumiliki ambulances na fire trucks ni mzigo ambao hawauwezi, they are a failure. hata stendi kuzisafisha hawawezi, madawati kwa wanafunzi hamna,sidhani hata kama jengo la halmashauri ya jiji lina vyoo vya kuvuta.

Well, hawawezi kwanini? sasa kama hawawezi hivyo vingine vyote kwanini bado wanavifanya au wanaachwa wafanye wakati hawawezi? Na kundi moja la watu kutokuweza linaweza vipi kuwa sababu ya kutofeanya mengine na watu wengine. Kama Dar hawawezi haina maana Tanga hawawezi, Mwanza au Arusha hawawezi!
 
Back
Top Bottom