MJADALA MAALUM: Kila Halmashauri/Manispaa itakiwe kuwa na EMS na Fire Brigade yake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MJADALA MAALUM: Kila Halmashauri/Manispaa itakiwe kuwa na EMS na Fire Brigade yake?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 10, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  AgustaWestland image

  [​IMG][h=1]Emergency Medical Services[/h]

  Wakati umefika wa kuondoa Idara ya Uokoaji kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani na kufanya jukumu hilo kuwa ni suala la Halmashauri na Manispaa nchini. Kwa muda mrefu - naamini tangu uhuru - huduma ya uokoaji (rescue service) imekuwa ni sehemu ya wizara ya mambo ya ndani na kufuata mfumo wa kijeshi ambao uko Polisi na Magereza. Sheria ya Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji ya mwaka 1985 imetengeneza kikosi cha taifa zima.

  Kutokana na Sheria hii kikosi kizima kinasimamiwa na Kamishna ambaye anateuliwa na Rais na hivyo kufanya watendaji wake wasiwajibike moja kwa moja kwa halmshauri na miji ambayo wanatumikia; mishahara yao inalipwa toka hazina na wanawajibika kwa uongozi wa kisiasa wa taifa zaidi. Sheria pia inamuweka Kamishna chini ya Waziri ambaye pamoja na kusimamia Jeshi la Polisi pia anasimamia Uhamiaji, Magereza na Wakimbizi.

  Kwa ufupi, jeshi hili limekuwa centralized bila ya sababu kubwa hasa katika kipindi hiki ambacho miji yetu inakua kwa kasi na watu wetu wanatawanyika zaidi na zaidi. Ni muhimu kulifanya jeshi au kikosi hiki kuwa cha mahali zaidi na kukifanya kiwajibike kwa mahali kilipo; kwa mfano kichukue amri yake kutoka kwa Meya wa mahali (siyo mkuu wa mkoa au wilaya). Kiundwe ili kiweze kuajiri na kusimamia mambo yake; kila mji uwe na kikosi chake.

  Lakini siyo kwenye suala la "fire brigade" tu lakini kwenye mji mkubwa kama wa Dar-es-Salaam halsmahauru zinahitaji kuwa na Idara zake za Huduma ya Tiba ya Dharura (Emergency Medical Service) ambayo itawajibika kuitikia wito wa matatizo ya tiba. Mifano iko mingi na ya kutosha ya watu kukosa huduma nzuri ya kwanza kwa haraka kwa sababu ama hakuna magari, hakuna huduma hiyo au mahali ilipo ni huduma ambayo ni binafsi sana na haiwajibiki kwa wananchi. Inawezekana kabisa kuwa na huduma moja ya uokoaji na medical rescue au vikawa vitengo viwili tofauti ndani ya mji mmoja.

  Nini kifanyike:

  a. Mabadiliko ya Sheria ya Kikosi cha Zimamoto na Ukoaji ili kuruhusu na kulazimisha halmshauri ya mjini nchini kuwa na kugharimia kikosi chake cha uokoaji na huduma ya tiba ya dharura. Sheria mpya itaachilia kila halmshauri kujiundia mfumo wake wa uokoaji chni ya viwango vitakavyokuwa vimewekwa kitaifa.

  b. Vikosi vyote vya sasa vya uokoaji kuingiziwa katika ajira za halmashauri, mali na vitu vyao kuingizwa huko. Lakini hili pia litatengeneza uwezekano wa kutengenezwa ajira mpya kwenye halmshauri mbalimbali ambazo kwa sasa hazina huduma hiyo au zinategemea huduma kutoka mikoani au taasisi binafsi. Hili la uokoaji na huduma ya afya ni lazima lionekane ni haki ya wananchi kama vile huduma ya polisi.

  c. Nafasi za ajira mpya kwa vikosi hivi ziende kwa maafisa wa polisi abmao wangependa kutoka kwenye upolisi na kwenda kwenye uokoaji. Hili liendane na kufanya maafisa wa Uokoaji wawe na nguvu za kipolisi vile vile. Sidhani kama sheria ya sasa hivi inawapa nguvu za kutosha za kipolisi.

  d. Mabadiliko haya yatapunguza mzigo wa kuendesha jeshi hili kitaifa kwenye bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani; na badala yake mzigo huu utaenda kwenye halmashauri ambazo zitatakiwa kupanga bajeti yake kwa kuanglaia mahitaji yake. Kwa mfano, mji wa Hanang kwa mfano unaweza usiwe na mahitjai sawa na Kinondoni lakini bado ni mahitaji. Kwa hiyo Hanang wanaweza kuajiri maafisa 10 tu wakati Halamshauri ya Kinondoni ikajikuta inahitaji maafisa 200.

  e. Maisha ya wananchi wetu yataanza kuokolewa kwa haraka zaidi kutokana na kupatikana kwa huduma ambayo inawajibika kwao. Leo hii watu wanahangaikaa kukimbiza wagonjwa hospitali kwa sababu hawajui wakipiga simu ya "emergency" yule anayejibu atafanya nini. Miji kama Dar ikipewa uwezo wake inaweza hata kununua Med-Vac Helicopters yaani chopa zinazotumika kuwahi watu walio katika matatizo ya hatari ya afya ambao kuwasafirisha kwa barabara itakuwa ni kupoteza muda zaidi.

  f. Hospitali kama Muhimbili na hospitali nyingine kubwa zianze kufikiria kujenga au kuwa na maeneo ya kufikishia wagonjwa kwa njia ya helikopta; yaani kujenga Heliports..

  Na mambo mengine yanawezekana kufanya hivi. Hili halihitaji fedha kutoka serikali kuu bali kutoka kwenye halmashauri. Halmashauri ambazo hazina uwezo sana zinaweza kupair up na halmashauri nyingine na maeneo ambayo ni madogo sana ndio yanaweza kuhudumiwa ama na sekta binafsi kwa mkataba au na vikosi vya polisi ambavyo vina mafunzo hayo zaidi chini ya serikali kuu.

  Hili lawezekana au haliwezekani na kwanini?
   
 2. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2012
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Mzee mwanakijiji naungana na wewe katika wazo hili ambalo naamini linalenga kuboresha ufanisi na ukaribu wa huduma hii kwa wananchi. Kuna vikwazo vikuu vitatu vinavyokabili utekelezaji wa wazo hili,
  Mosi, halmashauri zetu ziko katika hali duni kifedha kiasi cha kuzifanya ziendelee kuwa tegemezi kwa serikali kuu miaka 20 toka zirudishwe kwa sheria za serikali za mitaa za mwaka 1982 na pia miaka zaidi ya kumi toka sera ya ugatuaji wa madaraka ya mwishoni mwa miaka ya 1990.

  Pili, Sheria ya Utumishi ya umma ya mwaka 2002 bado inazibana halmashauri katika suala la kuajiri na kufukuza watumishi na hii ni kikwazo tayari cha kutosha kwa wazo lako, labda sheria ibadilishwe au ile za utumishi wa serikali za mitaa ya 2000 (nadhani) ipewe meno zaidi.

  Tatu, huduma za uokoaji na zimamoto bado zinachukuliwa kama ni shughuli za usalama wa raia na mali zao na hivyo zinaratibiwa na wizara ya mambo ya ndani. Sera ya ugatuaji wa madaraka haihusishi wizara ya mambo ya ndani na shughuli zake. Katika ngazi ya wilaya, ni wakuu wa wilaya ndio wenye majukumu ya kusimamia usalama wa raia na kwa mazingira yaliyopo ili wazo hili litekelezeke ni sharti kuwe na uoaji wa majukumu ya wakurugenzi wa halmashauri na yale ya wakuu wa wilaya ambao sio sehemu ya serikali za mitaa (halmashauri)

  Mwisho, pamoja na hayo ya juu, katika suala la kupunguza gharama za uendeshaji nadhani ni vyema tukafanya tathmini ya gharama za huduma hizi kwa sasa, ufanisi wake katika utendaji pamoja na uwezo wa halmashauri husika katika kutoa huduma hizi na nyinginezo kabla ya kushauri upelekaji wa majukumu haya katika ngazi ya serikali za mitaa.

  Kinadharia hii ni wazo zuri sana ila je kiutendaji tumejipangaje kulifanikisha?
   
 3. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Kabisa mkuu nakuunga mkono, shughuli hizi zinatakiwa ziwe chini ya Halmashauri/manispaa za wilaya. Zipo kamati za maafa za wilaya lakini hazina uwezo kibajeti na hata vifaa vya uokoaji wakati wa majanga. Wakati umefika sasa huduma hizi zikawa chini ya halmashauri za wilaya nchini kama zilivyo huduma nyingine kama afya nk.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  Nadhani kwa uliyoyasema hapo juu ina maana tukitaka kulifanikisha itabidi tujipange ili lifanikiwe; linaweza kuanza kwa phases kwa mfano katika halmashauri zenye makao makuu ya miji..
   
 5. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #5
  Apr 10, 2012
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  kaka

  pesa za mishahara hakuna

  msd taaban

  wewe unazungumzia haya mambo haya?
   
 6. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #6
  Apr 10, 2012
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 775
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Kwa kuanzia wangeanza na manispaa za dar. Kifedha sidhani hizi halmashauri zinamatatizo na hii itatusaidia kuepusha hudima ya Zimamoto kuwa centralized kwa jiji zima pale fire wakati jiji limepanuka
   
 7. T

  TumboMbele Hali Member

  #7
  Apr 10, 2012
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kuna haja ya makusudi kabisa kuwa na zimamoto kila halmashauri ya wilaya. Hivi karibuni hapa Pangani kuna gari iliungua moto mpaka ikawa majivu wakati tunsubiri zimamoto itoke Tanga umbali wa kilomita 50.
   
 8. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #8
  Apr 10, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,600
  Likes Received: 1,678
  Trophy Points: 280
  Tuanze na Madaktari kwanza kila Kata then Ambulance na vingine vifuate.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  Inapotekea medical emergency au tatizo la moto kinachohitajika siyo daktari kwanza bali watu wa huduma ya kwanza na waokoaji. Lengo ni kuhakikisha kuwa mgonjwa anapewa nafasi ya kutibiwa kwa kupatiwa huduma ya kwanza iliyo bora. Think about it. Daktari akija eneo la tukio ambalo halina vitu vya huduma ya kwanza ataanzia wapi kutibu?
   
 10. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #10
  Apr 10, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kwanza Pesa sio Tatizo la msingi tataizo la mmsingi ni vipaumbele sahihi kwenye allocation ya bajeti finyu . Ndio maana kuna bajeti sabau resouce always ziko scarse hata iwe Norway, USA, canada.

  Nitatoa mfano
  • kwenye halmashauri kuna viongozi wa Kisiasa/watendaji wanatumia ma VX. Why. Kwenye haamshauri hizo hizo kuna nyingine hazina hata ambulence ya bito.
  • Usishangae Mgao wa mafuta mkurgenzi wa halamshauri ni mkubwa kuliko hata mgao wa Gari la Polisi kufanya doria kwenye halmshauri hiyo.

  Kifupi vipaumbele vyetu ni vya kisiasa zaidi na sio vya kiutekelezaji na kitendaji .So Kikwazo kikubwa sio Pesa kikwazo kikubwa ni POlitics na Politician tena na hlii neno demokrasia mhhh . Itafikia wakati watu watakuwa wanaomba wabunge wao wafe ili wanajimbo wapate neema. Bcs Politics is more rewarded than anything else. Kikosi chazima moto na Uokozi Kipo kipo tu. Na maranyingi kwenye matukio wanaomba msaada kwenye makampuni binafsi wakati ilitakiwa kuwa vice versa

  Piga Hesabu
  Mawaziri na makatibu wakuu na Ma Rc na ma DC wakibadiishaVX zao japo kuwa vitara pesa itayookolewa kwenye mafuta kwa mwaka ingewezakupelekwa kwenye utajiwahudumamuhimuausehemuhasa zinazohitaji VX kama. Kwa sasa VX ya mwanasiasa inaweza kutumia.imetengewa lita 200 kwa wiki...hakuna anayeshtuka........ from masaki to posta.!!!!!!!!!!!!!
   
 11. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #11
  Apr 10, 2012
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mosi: Utendaji utakuwa rahisi chini ya Halmashauri za miji...ziko karibu na watu kuliko muhundo ulivyo sasa. Tujipime kwa wenzetu wa nchi zilizoendelea na jinsi halmashauri zao zinavyoshiriki katika kulinda maisha ya wananchi.

  Pili: Nambari ya dharura nayo ni 'kimeo'. Tukiboresha haya mawili kwa kuyapatia meno ya kisheria basi tutakuwa na mfumo unaoeleweka.

  Kwa kumalizia, Mitaala yetu ya elimu lazima iweke suala la mambo ya huduma ya kwanza hasa CPR..Hili litasaidia sana katika kuokoa maisha.

  Wakatabahu,

  Shadow
   
 12. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #12
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  MKJJ, mimi naamini haya yawezekana maana hakuna halmashauri zisizokuwa na pesa tena kwa wingi tu!! Katika nchi hii tatizo kubwa ni mind set ya wananchi pamoja na watawala!!

  Kuna kazi kubwa tu ya kubadili mid sets zetu! Tuliweza hili, watawala na watawaliwa wataweza kutengeneza priorities!! Tatizo lingine ni mipango, tumeshinwa kabla ya kuanza kwasababu ya kukosa planning!

  I am out for now...
   
 13. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #13
  Apr 10, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,600
  Likes Received: 1,678
  Trophy Points: 280
  Kaka kama wazo ni kuokoa maisha basi tuanze na VIFO vya MAMa na MTOTO, kwani naamini hawa wanaohitaji Emergency ni wachacche sana kuliko wakina mama na watoto wano kufa wakati w akujifungua na ujauzito, TUIMARISHE HUMA HII YA MAMA KWA MTOTO!
   
 14. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #14
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Wazo zuri lakini Halimashauri zetu hazina pesa kuweza anzisha huduma hizo, pia hata ukitoa tenda kwa watu binafsi waanzishe huduma hii basi itakula kwao kwani wanainchi walio wengi ambao watapata huduma hizo hawana uwezo wa kulipa kazi itakayokuwa tayari imefaanyika, mie naona bora kama somo la First Aid lingeanzishwa katika primary schools zote na watu wakafahamu kama wenzetu wa huko ulaya basi maisha ya watu wengi yangeokolewa eg kama ndugu na rafiki wangekuwa na elimu ya first aid naamini Kanumba angepona

  Swala la Moto nalo nalitizama ki hivyo kwanza kabla hatujatoka kwenye dimbwi la umaskini wetu,

  Hebu angalia Dar yoooote unayoijua MKJJ ni wapi pana EMS/Resque agent wa serikali? au Jeshi? Sembuse Halimashauri? kweli MKJJ unatakiwa urudi nyumbani.
   
 15. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #15
  Apr 10, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  Fire ya Knight Support ukiwaita hawazimi moto mpaka usign nvoice na wakimwaga maji USD 20,000
   
 16. T

  Topical JF-Expert Member

  #16
  Apr 10, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wazo zuri sana; kwa kuongezea

  a. ile department ya disasster management iliyoko ofisi ya PM; inaweza kutoka hapo ikapelekwa kwenye Halmashauri; idara kana pesa zinazoliwa kila mwaka kwakuwa hazitumiki kabisa; kukiwa na disaster wanapitisha bakuli wakati wana budget kila mwaka..

  b. Idara ya ustawi wa jamii iondoke katika wizara ya kazi iende halmshauri huko ndio wanajua nani yatima, kiwete, kipofu n.k. haka idara pia kana budget halafu kana tumia sana donor funds vibaya..seminara na upuuzi mwingi..

  c. Halmshauri inaweza kupewa funds kutoka kwa mifuko ya jamii (nssf, ppf) kwa maigizo ya serikali kila mwaka kutoka kwenye budget ya mambo ya jamii (uhusiano) kuliko kufadhili mipira, uzinduzi na upuuzi mwingine.na starehe..za kijinga kwa taifa la watu maskini..
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Apr 10, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Sambamba na hilo kuwepo pia na mfumo wa kuripoti matukio ya dharula ulio wa kisasa zaidi na wenye kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

  Na kuwe na elimu ya kutosha ya kuwaelimisha na kuwatanabahisha wananchi kuhusu umuhimu na ulazima wa kupiga simu (kama 9-1-1) kwenye hiyo/hizo mamlaka za huduma za dharula pindi patokeapo dharula.

  Tena ikiwezekana hiyo hata kwenye mitaala iingizwe ili iwe moja ya mambo ambayo watu wanajifunza kuanzia elimu ya chini hadi ya kati.

  Lengo hapo ni kujenga hayo mazoea ya kupiga simu kunakohusika ili msaada uweze kupatikana haraka iwezekanavyo.

  Kwa nchi za wenzetu hata vitoto vya miaka 5 vinajua vifanye nini patokeapo dharula ya kitiba.

   
 18. dattani

  dattani Member

  #18
  Apr 10, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15
  German imeziondoa hizi Chopa kwa matumizi yao ya ndani kwa sababu ya kuongezeka vifaa vingi vya huduma ya kwanza na hivyo uzito kuwa mkubwa. Hivyo basi hapa ziko air base Baden Baden German, zinauzwa bei kuanzia €500,000 pamoja na offer ya kukufundishia madokta wako emergency rescue, kuwapiga msasa mapilot wako na technicians wako bure. kutokana na hali ya foleni zetu, hizi zingesaidia kumwahisha mahututi kufikishwa kwenye huduma au pia kuwapeleka first responder team sehemu ilipotokea ajali ili kuwastabilize casualties kabla ya kuwasafirisha kwa malori/pikapu/buses kuelekea hospital za karibu na major roads eg segera/morogoro strip
   

  Attached Files:

 19. Gracious

  Gracious JF-Expert Member

  #19
  Apr 10, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,750
  Likes Received: 343
  Trophy Points: 180
  Nitarudi baadae
   
 20. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #20
  Apr 10, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,691
  Likes Received: 661
  Trophy Points: 280
  Tunalipa kodi?
  Zinatosha? .... baada ya hapo ndiyo tuzungumzie haya mambo.
   
Loading...