Landcruser
Senior Member
- Mar 24, 2017
- 179
- 344
Habari wadau wa jf na karibu kwenye mjadala.
Kama tujuavyo mwaka wa fedha ndiyo unaisha. Muda si mrefu bunge la bajeti kwa mwaka mpya wa fadha 2017/18 litaanza kule Dodoma.
Bajeti iliyopita ilikuwa kibwa sana ya tsh trilioni 21; huku sehemu kubwa ya fedha zikielekezwa kwenye miradi ya maendeleo kama walivyodai.
Katika hali halisi sijaona miradi yoyote ya maana iliyofanyika ndani ya hiyo bajeti tofauti na kelele za kwenye majukwaa ya kisoasa ya kutaja tu bajeti kubwa haijawahi kutokea.
Tulianza kwa mbwembwe za kisomewa mapato kila mwezi lakini sijui hayo makusanyo yalifanya nini au ndo tuseme nayo yalikuwa makisanyo 'hewa' maana hii nchi karibu kila kitu jamaa anasema ni hewa.
Au maana ya bajeti ndo zile mbwembwe za kiteua na kutengua na mara kutumbua majipu na mara Bashite na mara Faru John na mara Njaa na sasa ni Ney na mchanga pale bandarini?
Au bajeti huwa ni kelele tu za wabunge na hakuna chochote cha maana?
Kama kweli bajeti kubwa ilipitishwa na makusanyo ya kihistoria yakatokea iweje wanafunzi maelfu wakose mikopo vyuo vikuu? Iweje kwa miaka karibu miwili mfulilizo hamna ajira?. Ilianza tunahakiki hadi wahakiki nao wameona wanfanywa vituko wakaacha hata kulalamika. Madaraja ya wafanyakazi hayapandishwi wakati una bajeti na makusanyo makubwa.
Unadai umeziba mianya ya rushwa na kuwabana wapiga dili lakini mtaani tunalia njaa. Au nyie ndo wapiga dili wenyewe?
Serikali hii imekuwa ya drama kila kukicha. Bajeti kubwa na mbwebwe kila siku lakini mshahara hatupandishwi kwa watumishi.
Je baada ya vile vitanda na mashuka muhimbili matatizo yameisha? JK pamoja na ufisadi mkubwa enzi zake kulipa hawa wanaoitwa watumishi hewa lakini amajiri kwa takribani miaka 8 mfululizo akiwa Ikulu.
CCM mtujengee hoja na si vihoja. Tupeni takwimu na miradi mikubwa iliyoanza na inayoendelea sasa hivi kwa bajeti inayoisha. Nchi imekuwa kama tamthiliya sasa hivi kila kukicha tunasubiri kituko na statements za mkuu wetu pamoja na Bashite. Vituko vimekuwa vingi hadi nchi inazidi kuwa ya hovyo.
Hakuna ushirikiano tena. Tunafanya kazi kiuoga sana. Kiunafiki sana. Kikujipendekeza sana. Hatutafika kama nchi. CCM kimechoka sana ndani yake hakuna hata mtu mwenye uwezo wa kuongoza nyumba kumi. Kipumzishwe tuweke watu wengine. Wapo watu wengi wenye uwezo na uchungu zaidi. Bajeti ijayo ni yale yale. Hakuna jipya. Wataishia kupiga kelele kule Dodoma na baada ya miezi 3 wanajiondokea na bado nono.
Karibu kwa mjadala.