Mjadala: Kwanini tusiwe na Ukomo wa kuwa Mbunge na Udiwani? Kuna faida nyingi sana kufanya hivyo

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,493
5,528
Ndugu Wajumbe,

Taifa letu lina raia zaidi ya Milioni 60 na kila baada ya Miaka mitano tunafanya uchaguzi wa kuchagua wabunge madiwani.Lakini katika hio miaka mitano mitano huwa tunakuwa na zaidi ya Wabunge 350 pamoja na wa viti maalumi ambao wote hulipwa kila mmoja zaidi ya TZS Bilioni 2 kwa kipindi cha miaka mitano ya ubunge wao.

Kimsingi kwa kiwango hiki cha Pesa ina maana kwa kupitia Bunge tu kila baada ya Miaka mitano tunaweza kuzalisha mamilionea 300 ambao wanaweza kuwa wawekezaji na wafanya biashara wakubwa wanaoweza kuzalisha ajira na kukuza uchumi.Sasa kwa nini mtu awe Mbunge kwa zaidi ya kipindi kimoja.SI NI BORA iwe ni SHERIA kwamba baada ya kipindi unamuachia mwingine naye ale mema ya nchi?

Kwa mtazamo wangu,uamuzi huu utakuwa na faida kuu tatu.

Kwanza uatawafanya wabunge wawe makini katika kazi zao kwani wanajua wamepewa chance moja tua na wakikosea ndo basi tena.Kwa hivyo watatunga sheria ambazo wananjua wakitoka na wao zitawabana katika shughuli zao mfano viwango vya kodi na tozo pamoja na regulations za ajabu hazitapita

Kwa Malipo ya zaidi ya Bilioni 2 wanayopata katika kipindi chote cha ubunge wanao uwezo wa kufungua shughuli za kibiashara ambazo kwa kila mbunge anaweza kuajiri angalau watu 50 ambao ukiweka hesabu sawa ni sawa na ajira 15000 kila baada ya miaka mitano.

Pia kwa kuwa tutakuwa tunazalisha Mabilionea 300 kila baada ya miaka mitano ina maana tunaweza kujikuta kama taifa tunakuwa na Mabilionea 1200 wa moja kwa moja kutoka Bungeni na wengine ambao watatotaka na shughuli zao za kiuchumi

Tujadili faida nyingine za kufanya viongozi kuwa na Awamu badala ya kugombea mpaka wanafanana Majimbo na kufikiri wao ni wafalme.
 
Ukitaka ugomvi na wabunge waambie wapitishe mabadiliko haya mawili
1:Kupunguza mishahara yao na marupurupu
2:Ukomo wa kugombea iwe miaka 10

Hapo huwa wanaungana wote sio CCM wala Upinzani wote lao moja.

Jenerali Ulimwengu alishawahi kupendekeza hivyo ukomo wa wabunge wakaja na sababu ya kitoto sana eti nchi inabidi iwe na "succesion" kwamba eti Rais akimaliza miaka 10 na wabunge watakua wamemaliza miaka 10 kwahiyo tutajikuta watu wanaoingia katika uongozi woote ni wapya hawajui kuongoza serikali ktk mihimili yote miwili😄😄

Kitu ambacho ni uongo mtupu haiwezekani wabunge wote karibia 350 wamalize kwa pamoja
 
Hilo linaweza kutatuliwa kwa kuwa kuna Civil service ambao hasa ndo wahusika wakuu wa uendeshaji wa serikali.Wabunge hata wakifa wote haimaanishi kwamba hakuna succession kwa sababu taasisi za serikali zinao watumishi
 
Wewe wale watu ni wakali pale mjengoni wanaweza wakakupiga hata mawe

We jaribu kupenyeza hio hoja uone😄😄
 
Wewe wale watu ni wakali pale mjengoni wanaweza wakakupiga hata mawe

We jaribu kupenyeza hio hoja uone😄😄
Hii hoja niko nayo serious na ni moja ya ajenda zangu katika kampeni.natafuta Pesa ya kuchukua Fomu tu,Nikachuane na Bashite Mwenzangu wa Jimbo La Kigamboni
 
Wewe wale watu ni wakali pale mjengoni wanaweza wakakupiga hata mawe

We jaribu kupenyeza hio hoja uone😄😄
Hii hoja niko nayo serious na ni moja ya ajenda zangu katika kampeni.natafuta Pesa ya kuchukua Fomu tu,Nikachuane na Bashite Mwenzangu wa Jimbo La Kigamboni.
 
Back
Top Bottom