Mjadala: Kwanini Tanzania haipendi kutangaza milipuko ya magonjwa makubwa hadi waone shirika la afya duniani litoe tamko?

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,273
21,387
  1. Je; hatuna wataalam wazawa
  2. Je ni hujuma, nchi yetu inasingiziwa kuchafuliwa na mataifa makubwa?
  3. Je milipuko hii ni biashara ya ulaya?
  4. mipaka yetu ipo salama?
  5. Je, ni ukiritimba Wa kisiasa?
  6. Je, ni nini haswa?
Kwanini inchi yetu haipendi kuweka wazi mambo haya?

Nini hasa chanzo kuficha ficha?

Hadi waone shirika la afya duniani linapotoa tamko, na sisi ndiyo kwa mbinde sana tunatoa tamko, tena kwa sentensi za kisiasa kama hizi "kudai ni TISHIO!!!
IMG-20190914-WA0000.jpg
 
Add-on top!!

Nilitarajia milipuko iaanzie mikoa ya mipakani huko kama kigoma,bukoba n.k

Maana tuliambiwa Viwanja vya ndege viko salama, na wana vipimo kwa wageni
 
Siasa imetutawala sana, unadhani Kongo wanapenda haya mambo!
Tuwe makini isijekuwa mbinu ya mabeberu kutuadhibu ili waingie kirahisi.
IMG-20190914-WA0018.jpeg
 
Huo uchumi ni kwa faida ya nani? Endapo watu wakiumwa na kufa?
Ugonjwa wa mlipuko, kama upo, una njia zake za kuudhibiti, kwa sasa haijathibitika kama huo ugonjwa upo au la, bado ni tetesi, lazima zifanyike tafiti za kitabibu kwanza na hatua za awali zichukuliwe. Sasa katika stage hii, unatoaje matamko ya kiboya? Uchumi ni kwa faida yangu mimi, rubbish
 
WHO wanafanya kazi very closely na Serikali (Wizara ya Afya). Basically WHO hawawezi kutangaza kuwa kuna mlipuko bila idhini ya Wizara. Infact ni Serikali ndio hufanya kazi hiyo.

Wakigoma kutangaza, hakuna atakayefanya hivyo otherwise wewe ukijifanya kutangaza, utashughulikiwa. Rejea kilichompata Dr. Mwele Malecela kipindi kile
 
Ugonjwa wa mlipuko, kama upo, una njia zake za kuudhibiti, kwa sasa haijathibitika kama huo ugonjwa upo au la, bado ni tetesi, lazima zifanyike tafiti za kitabibu kwanza na hatua za awali zichukuliwe. Sasa katika stage hii, unatoaje matamko ya kiboya? Uchumi ni kwa faida yangu mimi, rubbish

Watu kuwa na uelewa wa hatari inayowazunguka je ni habari mbaya katika mstakabali wa uchumi? kumtambua mtu mwenye dalili za ugonjwa inachukua siku 3 - 6 ambapo vipimo navyo vinaweza kuonyesha kuwa mgonjwa ana Ebola, je Drs wetu na maabara zao wameshindwa hata kufanya physical diagnosis ndani ya muda muafaka mpaka wasaidiwe na WHO? tuna tatizo mahala fulani na inabidi tujiangalie upya ili tuende na wakati
 
Mabeberu wanakosa sana Usingizi kuona Mola katujaalia Amani na kutunusuru na mabalaa kadhaa ikiwemo Vimbunga na Maradhi hatarishi zaid

Sasa hivi wanajaribu kupandikiza Ebola ili kumlazimisha Jasiri na Jemedari wetu Dr Magufuli ayumbe

Bi Idhni llah Hatoyumba Rais wetu
 
  1. Je; hatuna wataalam wazawa
  2. Je ni hujuma, nchi yetu inasingiziwa kuchafuliwa na mataifa makubwa?
  3. Je milipuko hii ni biashara ya ulaya?
  4. mipaka yetu ipo salama?
  5. Je, ni ukiritimba Wa kisiasa?
  6. Je, ni nini haswa?
Kwanini inchi yetu haipendi kuweka wazi mambo haya?
Nini hasa chanzo kuficha ficha?
Hadi waone shirika la afya duniani linapotoa tamko, na sisi ndiyo kwa mbinde sana tunatoa tamko, tena kwa sentensi za kisiasa kama hizi "kudai ni TISHIO!!!
View attachment 1206831
Mipaka yetu inalindwa na vikosi vilivyotukuka hivyo hakuna milipuko yoyote inayoweza kupenya.
 
Hivi mnaujua athari za kutangaza vitu vya kijinga kama hivyo kiuchumi? hii nchi imejaa watu wajinga sana
Acha kuita vitu vya kijinga...kitu cha muhimu tumuombe mwenyezi Mungu atusaidie kwani sisi kiukweli kwa capacity yetu hatutaweza....kwa taarifa yake Ebola ikiingia haitasubiri wewe utangaze kwani itajitangaza yenyewe....hata hiyo lugha ya uchumi hutaikumbuka tena...
 
Back
Top Bottom