Mjadala kwa watarajali katika nyanja za afya (interns) na changamoto za ajira

Asha Hincha

Member
Jul 13, 2021
15
15
Kwa watarajali, intern doctors, intern pharmacists na kadhalika.

Nakumbuka tunapokuwa shuleni sekondari kunakuwa na zile fikra kwamba zipo kada ambazo ukizisomea uwapo chuoni basi ajira ni nje nje, hivyo watu wanaenda kusomea kada hizo akiwa na wazo kwamba hatopata shida ya ajira baada ya kuhitimu, moja wapo ni kada ya afya.

Kiuhalisia mambo ni tofauti, tunashuhudia wapo madaktari, wafamasia, wataalamu maabara wengi mtaani ambao hawana ajira, hivyo basi kwa namna moja ama nyingine tunaweza kusema suala la ajira ni wewe kama wewe na juhudi zako bila kujali umesomea kada gani,

Yapo mambo ningependa kuyazungumzia,

Mtazamo kuhusu kujiajiri, unapo muambia mtu ajiajiri wazo la kwanza ni nitajiajiri vipi sina mtaji? nikisema nifungue biashara lazima niwe na mtaji, nikisema nianze kutoa huduma kulingana na kile nilichosomea nayo siwezi kuanza tu kuna hatua nyingi za kupitia ambazo ndani yake siwezi kukwepa suala la mtaji

Nikija kwenye mada yangu ya watarajali (interns), unapopata nafasi ya kufanya utarajali katika kituo chochote ni uhakika asilimia 99% utapokea malipo ya internship kwa mwezi ambayo ni 80% ya mshahara wa daktari, mfamasia, mtaalamu maabara n. k, kwa makadirio (kulingana na mishahara ya sasa) ni laki 5 mpaka laki 9/ 1 M kulingana na kada uliyopo,

Huu ni muda wa kujitathmini na kuwekeza kwaajili ya maisha baadae, baada ya kuingia mtaani utakapo hitimu, si muda wa kuponda mali kama hukuwahi kumiliki simu kali basi ndo utamiliki, kama ulikua umepanga nyumba ya ovyo basi utatafuta nyumba kali na wengine wanaamua kuoa na kuanzisha familia.

Ukimaliza internship kuna safari ndefu mpaka usimame kimaisha, nasema pesa unayoipokea ni kubwa mno ambayo inaweza kukufaa baadae utakapo ingia mtaani endapo utaitumia vizuri/au kuiwekeza.

1. Jaribu kuishi kwa mipaka katika kipindi hiki
Si kwamba ujibane uishi maisha magumu hapana, lakini kuwa na mipaka katika matumizi, ishi maisha ya kawaida kwa kupata huduma zote muhimu, lakini kuwa na malengo ya baadae.

2. Weka akiba
siku zote kabla pesa hujaanza kuitumia kwa chochote toa kiasi ulichojipangia kukiweka akiba, kisha inayobaki sasa ndiyo utaipangia matumizi ukianza na mahitaji ya msingi, ili baadae usije kupelea pesa na kwenda kuchomoa mpaka ile akiba isipokua kwa dharura kama maradhi n. k. Kama utaanza tu kuitumia ela unapoipata ukitegemea baadae utabakisha akiba amini kwamba matumizi huwa hayaishi.

3. Ni vizuri zaidi kuwekeza ukiwa bado unapokea pesa (kabla hujamaliza internship),
ni bora pesa ikiwa kwenye mzunguko na kuingiza faida kuliko kuihifadhi pesa hiyo hiyo tu kwa muda mrefu, fanya tafiti ni sehemu gani unaweza kuwekeza pesa yako kama ni biashara au kampuni za uwekezaji na manunuzi ya hisa ndogo ndogo, wekeza kidogo kidogo kwanza usiiweke pesa yote kwa pamoja.

N. B ni muhimu kuomba ushauri kwa watu unaoona wamekuzidi katika masuala ya kibiashara, uwekezaji na fedha kiujumla.
Kwa hili naimani mpaka unaingia mtaani tayari una msingi mzuri wa maisha hata kama utachelewa kupata ajira,

Karibuni tujadili namna gani nyingine za kufanya tujikwamue kama vijana, pia tusisahau kuvote wadau.

SHUKRANI.
 
Back
Top Bottom