Mjadala kuhusu uwajibikaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjadala kuhusu uwajibikaji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yona F. Maro, May 9, 2008.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  May 9, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kwa mambo yaliyojitokeza, Monduli mpaka Bariadi ni kufedhehesha Utawala Bora na miiko iliyowekwa na wenye mapenzi mema (waliyaita maadili ya viongozi wa umma).
  Kama kweli ni busara, tulijiwekea miiko sisi wenyewe na kuikubali, kwamba pindi utakapopata nafasi ya kutumikia umma wa Wadanganyika (Watanzania) , inakupasa uifuate. Pamoja na sheria mbalimbali, waliweka pia Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma (Na. 13 ya 1995). Sheria hii pamoja na mambo mengine, inaweka misingi ya maadili yanayotakiwa kuzingatiwa na viongozi wa umma ili kujenga na kudumisha utawala bora na utawala wa sheria. Lakini sivyo! Sheria hii inawataka viongozi kufanya kazi kwa uadilifu, kutaja mali na madeni yao, kufanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni, kubainisha mgongano wa kimaslahi, kubainisha zawadi au maslahi ya kiuchumi, matumizi sahihi ya taarifa na kuepuka rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.
  Sasa hawa ndugu zetu (waliowajibishwa, japo sikubaliani na hili sana kwani sioni kama kweli wamewajibishwa kwani bado wanapeta, tena sana tuu). Eeeh, siunaona bado ni waheshimiwa sana tuu, na kesho na kesho kutwa utawakuta wanateuliwa kwenye manyadhifa flani flani tena nyeti, nani ajuaye?
  Halafu, hili la “Hero’s welcome”! Duh! Wajameni, hata hatumwogopi Mungu! Lakini anyway, labda wanastahili, kwasababu hata baada ya jamaa kumtaka Baraba badala ya Yesu, walisherehekea sana !
  Mapungufu mengi:
  1) Impunity: Huyu JK aliamua kulipa fadhila kwa washkaji wake. Sasa kuwawajibisha ndio ngoma. Washkaji wamejenga kiburi, ndo maana unaona hawafanywi kitu;
  2) Mapungufu kwenye hiyo Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma: Kama kiongozi atakosea kwa mujibu wa sheria hiyo, mbona hatuoni wakiwajibishwa? Nadhani kuna mapungufu hapa;
  3) Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma: Hiki ni kijichaka cha kuwaficha mafisadi! Si mnakumbuka baadhi ya wadau siku za hivi karibuni walipita pale kutaka kujua ABCs, lakini wakawekewa ngumu!

  Hili la kuwazomea, sawa, lakini I do feel kwamba tunahitaji kufanya zaidi ya hilo .
  a) Tuanze na tuendelee kusambaza elimu ya uraia. Watu wetu wana mwamko wa mabadiliko, sema huwa wanashindwa kwa nguvu ya “vijisenti”;
  b) Hivi hakuna watu wenye uthubutu kama Mzee wa Kesi (Mchungaji Mtikila) kufungua kesi ya kimkakati? Hii inaweza kuwa kama mfano, wengine wataogopa.

  Tujadili
   
 2. O

  Ogah JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  shy

  .....please tumia uwezo wako wa IT,..........ili JF iwafikie wananchi wengi........kwani kwa wananchi ndio mahakama nzuri.....only if wakiwa well informed!!..............na huo ndio uwe mkakati wetu
   
Loading...