Mjadala kuhusu mchango wa Diplomasia ya Uchumi na Uhusiano wa Kimataifa katika kuchochea fursa za maendeleo kwa wananchi kupitia sekta ya kilimo

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
Zoom Saturday 20/11/2021

Usikose kufauatilia mjadala uliondaliwa na Watch Tanzania utakaofanyika kupitia mtandao wa ZOOM utakaofanyika tarehe 20/11/2021 kuanzia majira ya 10:00 jioni hadi saa 12:00, utakao

jadili MADA kuhusu mchango wa Diplomasia ya Uchumi na Uhusiano wa Kimataifa katika kuchochea fursa za maendeleo kwa wananchi kupitia sekta ya kilimo.

Pia, mjadala huo utarusha mubashara kupitia Watch Tanzania Online, Global TV online, EATV, TBC1 na Mwanahalisi Tv online.

Mjadala huo utawahusisha wadau mbalimbali wa masuala ya kilimo na diplomasia wa ndani nan je ya nchi ambao watoa michango na hoja mbalimbali kuhusiana na suala hilo.

Wadau hao ni pamoja na:
  • Dkt. Canisius NGUGURU-Meneja wa Tanzania Agriculture Institute (TARI)
  • Geoffrey KIRENGA- Mkurugenzi Mtendaji SAGCOT
  • Mhe. Hussein BASHE- Naibu wa Waziri wa Kilimo
  • Frank NYABUNDEGE-Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Agriculture Development Bank (TADB)
  • Abdulmajid NSEKELA – Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB
  • Edwin NDAKI- Dispora Finland
  • Dkt. Jacqueline MKUNDI- Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo na Mkurugenzi Mtendaji wa TAHA
  • Ringo RINGO- Mwenyekiti wa Tanzania Sunflower Processors Association (TASUPA)
  • Dkt. Khalid Salum MOHAMED- Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Utaratibu na Baraza la Wawakilishi)
  • Mhe. Jestus NYAMANGA- Balozi wa Tanzania Nchini Ubelgiji, Luxembourg na Umoja wa Ulaya.
  • Mhe. Job MASIMA - Balozi wa Tanzania Nchini Israel
  • Dkt. Hezron MAKUNDI- Mhadhiri, UDSM
  • Mhe. Queen SENDIGA – Mkuu wa Mkoa wa Iringa.

_Zoom Saturday

Watch Tanzania inakualika kushiriki Mkutano wa Zoom utakaofanyika Novemba 20, 2021 (Jumamosi) kuanzia saa 10 kamili hadi 12:30 jioni.

Mada: Mjadala wa Kitaifa kuhusu mchango wa Diplomasia ya Uchumi na Mahusiano ya Kimataifa katika kuchochea fursa za maendeleo kwa wananchi kupitia Sekta ya Kilimo.

Muda ukifika utaweza kujiunga na kushiriki moja kwa moja kwa kubofya hapa ~ Join our Cloud HD Video Meeting

Au kupitia
Meeting ID: 8809469421
Passcode: 907652

Mkutano huu utarushwa mubashara (Youtube) kupitia EATV, Clouds Digital, Global TV Online, Dar Mpya TV, TBC Online, Mwanahalisi Digital, Mwananchi Digital, EFM Digital, Star TV na Saangapi TV, Daily News Digital, Saangapi TV, ITV, Azam TV na Star TV

Karibu, tujenge Taifa letu pamoja. Usikose!
 
Mkuu ona watu wasivyopenda kilimo; yaani hakuna comment hata moja tangia umepost hii kitu. Asilimia 80 ya Watanzania wamejiajiri kwenye sector ya kilimo!

Nasikia Serikali imeanzisha Kurugenzi ya Economic Diplomacy pale Wizara ya Mambo ya Nje na kateuliwa Balozi kuiongoza hiyo Kurugenzi. Katika mijadala kama hii ni vyema naye akawemo.

Chonde chonde msitusahau na sisi Wavuvi tunapenda tupate fursa hizo zinazoletwa na Economic Diplomacy.
 
Back
Top Bottom