Umenena ndugu, yaani hatupumui kila siku ni kadi za harusi. Tumechoka jamani raisi tuondolee balaa hili umaskini unatunyemelea kwani tusipochangia tunatengwa na marafiki
Mi nashauri sherehe ziwepo sana tu,sema serikali itoze kodi kubwa sana ili waoaji wajitathmini kama kufunga harusi kwa sherehe au kimyakimya.Maana sherehe ni mambo ya kitajiri.
Tukubali tusikubali michango ya harusi , send-off na kitchen parties ni kero na ni kujimaliza kiuchumi kwa baadhi ya watu.Kwanza asilimia kubwa ya michango hiyo haifiki kwa walengwa. Kuna haja gani ya kuchanga m.20 alafu maarusi wanapewa na kamati m.1 ati zawadi. Ni vyema michango ya pesa zote wapewe maarusi wakaanzie maisha na kusiwe na send-ff wala kitchen parties ila familia ya mioaji na anayeolewa waweke pamoja resources zao kufanikisha shghuli.Pia kusiwe na biashara ya mahari
Duh eti sherehe mwisho saa kumi na mbili jioni! Hivi kwani sherehe ya harusi imekuwa disco toto!? Wanaohudhuria sherehe za harusi ni watu wazima wanaojielewa mie sioni tatizo hapo!!
Kuhusu kuchangia kila mtu ana utashi wake hulazimishwi!
Tuko mstari mmoja mkuu, mi huwa nakereka sana, sherehe yako unishughulishe mie, mipango yako niigharamie mie, haiingii akilini. Ndiyo kama unavyosema tunachanga kuogopa kutengwa.
Jambo zuri hili naamini sio wote wanaotoa michango ya harusi wanaifurahia,
wengi wanaogopa kutengwa na jamii.
Hii michango ipigwe marufuku kwani ni matumizi mabaya ya fedha.
Duh eti sherehe mwisho saa kumi na mbili jioni! Hivi kwani sherehe ya harusi imekuwa disco toto!? Wanaohudhuria sherehe za harusi ni watu wazima wanaojielewa mie sioni tatizo hapo!!
Kuhusu kuchangia kila mtu ana utashi wake hulazimishwi!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.