Mjadala Katiba Mpya Zanzibar wapasua kichwa

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
Mjadala wa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano umeendelea kupasua vichwa wanasheria na vigogo wa Zanzibar, ambapo jana imeelezwa si sahihi Rais wa Zanzibar kula kiapo kutetea katiba hiyo, wakati amechaguliwa kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984. Hayo yameelezwa na Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Ibrahim Mzee wakati akiwasilisha mada kuhusu katiba za Tanzania na Zanzibar changamoto juu ya mianya na utata uliopo, katika mjadala wa katiba mpya uliofanyika mjini Zanzibar. Alisema Rais wa Zanzibar anachaguliwa kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar kwa kuitumikia Zanzibar, lakini bado katiba ya Muungano inamlazimisha kuapa kutetea na kuilinda katiba hiyo.

Mzee alisema kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano, Rais wa Zanzibar ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano asiyekuwa na Wizara Maalumu wakati Zanzibar iliungana na Tanganyika kama mataifa mawili yenye sifa sawa kitaifa. “Rais wa Zanzibar anachaguliwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar na sio sahihi kulazimishwa kuapa kutetea katiba ya Muungano,” alisema Katibu huyo huku baadhi ya wajumbe wakipiga makofi katika kongamano hilo.
Alisema katiba ya Muungano imempa mamlaka Rais wa Muungano kuchagua Mawaziri kwa kushirikiana na Waziri Mkuu na kuwapangia kazi baadhi ya Wazanzibari katika wizara yoyote hata kama haihusiki na masuala ya muungano. Katibu huyo wa Baraza alisema kwamba utaratibu huo ni sehemu ya utata uliopo katika katiba hiyo na kutoa mfano Wizara ya Mambo ya Ndani Nchi ambayo inaonekana ni ya Muungano kuna baadhi ya mambo yanahusu upande mmoja peke yake.

Alitoa mfano katika Wizara hiyo kuna Jeshi la Magereza na Kikosi cha Zimamoto ambayo hayahusiani na Zanzibar, lakini Waziri wake anatoka Zanzibar na kusimamia mambo yasiyokuwemo katika mambo ya Muungano. Alitoa mfano mwengine Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kuwa mbali na kupewa Waziri kutoka Zanzibar kuna jeshi la Kujenga Taifa, ambalo halimo katika masuala ya Muungano. Katika mada yake hiyo alisema mkanganyiko mwingine unajitokeza katika suala la Jumuiya ya Afrika Mshariki, kwa vile yapo mambo ambayo Zanzibar ilipaswa kunufaika moja kwa moja bila ya kupitia serikali ya Muungano. Aliyataja mambo ambayo hayamo katika mambo ya Muungano ni Utalii, Afya na Kilimo ambayo yanahitaji kujadiliwa na kuwekewa utaratibu mzuri, kwa maslahi ya Zanzibar.

Alieleza kwamba katiba hiyo pia inaudhaifu katika kutoa mamlaka makubwa ya Tume ya Uchaguzi ambapo inaelezwa baada ya Tume ya Uchaguzi kutangaza matokeo hakuna chombo chochote chenye uwezo wa kuhoji matokeo hayo. “Tume ya Uchaguzi kuwa na mamlaka kuliko chombo chengine hiyo ni kasoro kubwa ya Katiba”, alisema Katibu wa Baraza la Wawakilishi. Aidha, alisema kwamba katiba ya Muungano imeweka kinga kubwa kwa Rais kutoshitakiwa akiwa madarakani na baada ya kuondoka, jambo ambalo alisema linahitaji kuangaliwa katika mchakato huo wa marekebisho ya Katiba.

Alisema viongozi katika mataifa mbali mbali wanapokuwa madarakani wanakawaida ya kujisahau na kuwepo kwa sheria kama hizo kunaweza kusababisha matumizi mabaya ya madaraka. “Nafuu katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 inaruhusu Rais akiwa nje ya madaraka kushitakiwa, tofauti na katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo inazuia Rais kushitakiwa akiwa madarakani na hata akiondoka madarakani,” alisema. Aidha, alisema haikuwa muafaka kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano kueleza Makamo wa Rais kama atafukuzwa madarakani anapoteza na sifa ya kugombea Urais wa Zanzibar.

Alisema hata utaratibu wa kuthibitishwa na Bunge, makamo mpya wa Rais pale inapotokea aliyekuwepo amefariki dunia sio mzuri kwa vile wabunge humjadili na kumthibitisha kwa muda mfupi, jambo ambalo huwanyima wananchi na vyombo vya habari kumchunguza uwezo wake wa kiutendaji na uadilifu. Alishauri inapotokea hali kama hiyo jina na makamo wa Rais litangazwe na lithibitishwe na Bunge baada ya muda wa miezi miwili ili wananchi wapate nafasi ya kuangalia kumbukumbu zake katika masuala ya uadilifu na uwajibikaji.

Wakichangia mada hiyo wajumbe wameshauri kuwepo Tume tafauti mbili za kukusanya maoni ya Katiba ya Muungano ili Zanzibar isifunikwe na Tanzania Bara ambayo ina idadi kubwa ya wakaazi. Wakili mkongwe Mahakama Kuu Zanzibar, Awadh Ali Said alisema kulingana na mazingira ya Zanzibar, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kuna haja iunde tume yake ya kukusanya maoni na Zanzibar iwe na mjadala wake. Alieleza kwamba iwapo mjadala huo wa katiba utafanyika kwa jumla Zanzibar haitanufaika na lolote na badala yake Tanzania Bara watoe maoni yao na Zanzibar watowe maoni yao juu ya katiba mpya.

Wakili huyo alisema Zanzibar ina kero nyingi ndani ya muungano ikiwemo suala la Afrika Mshariki ambapo kuna mambo yapatayo 14, ambayo hayapo katika orodha ya mambo ya Muungano. Ahmed Omar Khamis alishauri tume itakayoundwa isiwe ya ujanja ujanja kama tume zilizotanguliwa na badala yake maamuzi yatakayotolewa na wananchi yatekelezwe kwa vitendo. Hata hivyo, aliunga mkono wazo la kuwepo tume mbili katika ya Tanzania Bara na Zanzibar na kila moja ifanye kazi katika sehemu moja. Naye mwanaharakati, Rashid Yussuf Mchenga alisema wakati umefika Zanzibar iwe na mamlaka ya kisheria kusajili vyama vyake vya siasa, badala ya vyama hivyo kulazimishwa kuwa na sura ya Muungano.Alisema serikali ya Zanzibar ndiyo pekee duniani isiyokuwa na vyama vyake vya siasa, licha ya kuwa na hadhi ya nchi na kutaka wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wawe imara katika kusimamia maslahi ya Zanzibar.

Kongamano hilo limetayarishwa na kituo cha huduma za sheria Zanzibar (ZLSC) kwa kushirikiana na chama cha wanasheria Zanzibar, (ZLS) jumuiya ya waandishi wa habari ya (Wahamaza) na taasisi ya Utafiti ya Bahari ya Hindi, (ZIORI) Zanzibar.

Source: IPPMedia
 
Dawa ya yote haya ni kuwa na serikali tatu au kuvunja muungano.
 
Alieleza kwamba katiba hiyo pia inaudhaifu katika kutoa mamlaka makubwa ya Tume ya Uchaguzi ambapo inaelezwa baada ya Tume ya Uchaguzi kutangaza matokeo hakuna chombo chochote chenye uwezo wa kuhoji matokeo hayo. "Tume ya Uchaguzi kuwa na mamlaka kuliko chombo chengine hiyo ni kasoro kubwa ya Katiba", alisema Katibu wa Baraza la Wawakilishi. Aidha, alisema kwamba katiba ya Muungano imeweka kinga kubwa kwa Rais kutoshitakiwa akiwa madarakani na baada ya kuondoka, jambo ambalo alisema linahitaji kuangaliwa katika mchakato huo wa marekebisho ya Katiba.

Source: IPPMedia

Wazanzibar wanaibua mengi ambayo wabara hatukuyaongelea sana. Hivi Watanzania tutaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu kwa tunaowachagua hadi lini?
 
Dawa ya yote haya ni kuwa na serikali tatu au kuvunja muungano.

Haiwezekani kuendelea kufunikafunika tu mambo yaliyokubaliwa na watu waili Nyerere na Karume. Bora serikali tatu na kila state inabaki na sheria zake na kuwe na katiba ya Jamhuri ya Muungano
 
Tatizo la huku bara CCM wanataka kumonopoly hoja za katiba wakati wanafungwa na uCCM bara na visiwani yaani wakiwa wanatoa hoja wanaogopa kuwaudhi CCM Zanzibar wakati waZanzibari wao linapofika suala la muungano ni wamoja wanatoa hoja as if hatujawahi kuungana nao yaani ndio tunawaomba tuungane kwao hakuna UCCM na UCUF kwa Uzanzibar kwanza na wabara wanaonekana kama wanatakakuwafunika na kuwatawala hivyo wanaweka uzalendo mbele kutetea uzanzibari wao huku bara. Ukitoa hoja inayowabana wazanzibar CCM na viongozi wake watakubana kuwa unahatarisha muungano. Hivyo mabadiliko ya katiba chini ya Viongozi hawa na CCM hii utaniambia jinsi ambavyo tutauza Utanganyika wetu na kuburuzwa na Wazanzibar, Maana wakati wenzetu watajadili bila uoga sisi tutakuwa tunanyoosheana vidole mf. Mabadiliko ya katiba ya Zanzibar ya kuitambua Zanzibar kuwa ni nchi na kuweka kipengele cha serikali ya umoja wa kitaifa kiukweli kimevunja katiba ya Muungano Lakini viongozi wetu wanabisha na kudai wote wanaosema hivyo ni wachochezi na hawaitakii mema Zanzibar eti mabadiliko hayo yameepusha machafuko Zanzibar, Ukiwaambia hatakama yameepusha maafa basi wangefanya mabadiriko ktk katiba ya muungano pia ilikusiwepo kwa msigano wanakuambia hakuna utata wowote ktk katiba hizo mbili. Sasa ktk jambo kama hili hata CUF bara nao wanawaunga mkono CCM maana Uwepo wa CUF unategemea Zanzibar uwepo wa CUF Bara ni kukamilisha masharti ya usajili wa vyama. Maana Lipumba hana ubavu wa kumzidi SEIF yaani wakikorofishana na SEIF Lipumba out, yaani mwenyekiti hafui dafu kwa katibu. Ndio maana hata CUF ktk suala la katiba wamesha tekwa na Upande wa Zanzibar hivyo waBara ktk mjadala wa katiba tusiwategemee CCM wala CUF hafadhali hata NRA , UDP.TLP ,TADEAna UMD wanaweza kuwa wawakilishi Bora kuliko CCM na CUF.
 
Sijui kama wengi mmegundua Serikali ya CCM ilivyozima wimbi la majadiliano ya uundwaji wa katiba mpya kwa kupeleka hoja bungeji kwamba kikao kijacho utapelekwa mswada bungeni kuhusu katiba mpya? Huu ni ujanja tu na unaona hakuna moto moto uli uliokuwepo hapo awali.
 
Swafiiii sana lazima mbivu na mbichi zijulikane. Sasa hayo yaamishiwe ndani ya baraza la wawakilishi ili kupata ridhaa za wawakilishi wa wananchi kisha moto uwashwe kwa kasi kubwa sana.

Mpaka kijulikane. Haiwezekani Rais wetu Zanzibar awe minister asiyena wazira maalum ndani ya muungano.

Lazima aheshimike kama rais wa muungano.
 
Nadhani mkwara wa Wazanzibar utaongeza zadi vuguvugu la madai ya katiba mpya, maana wale jamaa wana mshikamano wa kitaifa wanapoongelea uzanzibar hakuna cha ccm au cuf. Kazi nzito ipo
 
Inaniongezea shaka kuwa moja ya kitu wenzetu (Zanzibar) hawakitaki ni kuhusu kuapa kulinda Muungano, na inaonyesha kweli wanaolazimisha Muungano ni Bara. Juzi tumeshuhudia pia Mh. Lipumba akiwabeza CDM kuwa wanawadharau wa Zanzibari sababu ya mchango wa Mh. Tundu Lissu kuhusu mambo ya Katiba, nafikiri sasa kwa hoja za Mh. Ibrahim Mzee zitamfumbua akili Mh. Lipumba kuhusu mchango wa Mh. Lissu. Nionavyo mimi, tukitegemea serikali ambayo imeapa kulinda Muungano, hatutaweza kuendesha zoezi la kutengeneza katiba yenye taswira ya mahitaji ya wananchi kwa uhuru na uhalisia. Je tunategemea chombo gani huru kitakachojali mawazo huru toka kwa wananchi na kuya implement bila kuyachakachua? Changamoto si ndogo tuliyonayo, tusikimbilie kuanza mjadala kabla hatujahakiki hadidu za rejea (Terms of reference) zinazokidhi haja zetu pamoja na uhuru, uadilifu na uundwaji wa tume itakayoendesha mchakato huo.
 
Utekwaji wa hoja ya uundwaji wa Katiba mpya uliofanywa na Kikwete umedhoofisha jitihada za wanasheria kupata nafasi ya kuendelea kuchanganua tetezi ya hoja hiyo kutoka kwa wananchi. Nashangaa kama isue ya Dowans ndo imemeza kabisa majadiliano ya Katiba mpya
 
Halafu Lipumba mtaalamu wa uchumi anadharau hoja ya Tundu Lissu, wazanzibar hapa wanaongelea sheria na faida kwa wazanzibar, naipenda hii uzanzibar kwanza uchama baadaye.
Lipumba mnafiki anaendelea kujikomba kama kawa anajipendekeza kwa bosi Maaalim, wazanzibar nawapenda pale wanapoongea mambo ya sheria za muungano na katiba pia hapa hatutaki muungano kila nchi isonge kivyake tukakutane kwenye EAC tu.
 
Back
Top Bottom