MJADALA: Je, Pikipiki gani ni bora kwa matumizi ya nyumbani au biashara kwa Tanzania?

Naomba kujua Bei ya mzigo huu ukiwa mpya
images.jpeg
 
Nina Dt nabadili block, jamaa wa veta anasema wanachonga block vizuri, ushauri?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama wanachonga vizuri wapelekee hiyo Block yako wachonge. Kama ni Mara ya kwanza kuchongwa utabadili piston kutoka size 25 (Standard) na kutumia size 50 baada ya kulichonga pia utabadili na piston rings au utanunua piston na rings zake kisha hao wajaribu kufitisha kabla ujaondoka.

Uzuri wa block za kijapani una weza kuchonga Mara mbili, moja kutoka standard kwenda size 50, pili kutoka size 50 kwenda 75. Ukimaliza hapo ni kununua block jipya.

Mchina karahisisha mambo block ikichoka tupa pembeni unanunua nyingine na bei ni nafuu.
 
Habari zenu wana JF

Nahitaji kununua pikipiki kwa ajili ya matembezi. Nitakua naitumia maeneo ya Kasulu ambapo kuna tope sana na vumbi jingi kipindi cha kiangazi. Bajeti yangu ni 2M mpaka 3M.

Nawasilisha, Naomba ushauri na maoni kutoka kwa wazoefu.
 
Kuna zile mzee wa 'nje ya box' kigwanox alitaka apewe mkopo nadhani zitafaa zaidi.


Let's meet at the top, cheers 🍻
 
Kama huko kwenu ni off road sana..tafuta kitu XL honda 125..hutojuta aseee..sema ongeza bajeti manahizo ni parefu kidogo...
Ila kua xl toyo waweza cheki hizo.


#MaendeleoHayanaChama
 
Kama kwa matembezi tafuta moja kati ya hizi hapa:

CBR 250 au 150

Ninja 300 au 250

R3

Duke 390 RC
 
Mimi natumia hii mkuu lakini spare zake ni mpaka miji mikubwa mfano mimi naagiza dar
IMG_20200913_224204_310.JPG


4ml tsh
 
KWA USHAURI WANGU KWA BAGET YAKO ACHANA NA MASIFA !! NUNUA MAHINDRA ARROW CHUMA YA MUHINDI , IKO POA MNO MAFUTA KAMA INANUSA TU , KWA MWENDO PIA INAJIWEZA LAKINI PIA UMBO LAKE LINAVUTIA SANA , HAUTAKUJA KUIJUTIA HATA SIKU MOJA NI PIKI PIKI IMARA MNO NINAYO TANGU MWAKA 2016 MWEZ WA 3 MPK SASA SIJAGUSA ENGINE ZAIDI YA KUMWAGA OIL MAFUTA INATUMIA LITA 1 KWA KM 45
IMG_20200725_172415.jpg


sent from HUAWEI
 
kwanza sikushaur pikipik za mataili ya spoko mana utakuwa unaweka tyubu ndan itakubid utembee na pamp kwaajil ya miiba ikitoboa taili
pia nivizur uchukue pikipik ya stater kwa sababu ya tope kupiga makiki pikipik ikizima kwa maji utachoka wenyewe.

so kwa upande wang nakushaur boxer zile madguard ya juu mbele ila injin chukua ile model ya zaman huta jutia mana vifaa vinapatikana popote sisi ndo tunazotumia huku mbugan.

Habari zenu wana JF

Nahitaji kununua pikipiki kwa ajili ya matembezi. Nitakua naitumia maeneo ya Kasulu ambapo kuna tope sana na vumbi jingi kipindi cha kiangazi. Bajeti yangu ni 2M mpaka 3M.

Nawasilisha, Naomba ushauri na maoni kutoka kwa wazoefu.
 
Habari zenu wakubwa?

Ninaomba ushauri tafadhali.

Ninahitaji pikipiki kwa matumizi binafsi ya kawaida. Ninapenda TVS HLX family.

Sasa napata utata ni ipi nichukue kati ya TVS HLX 150cc Gia 4 na TVS HLX 150cc Gia 5.

Ni ipi bora, kwa uimara, mwendo, unywaji wa mafuta nk.
 
Habari zenu wakubwa?

Ninaomba ushauri tafadhali...

Chukua TVs hlx 150x hii ndio chuma nzuri na engine yake ina nguvu kuliko hlx series zote.
Kua na 4 gears or 5 gears hizi mbembwe tu.
Pikipiki nzuri tunaangalia
1. Nguvu (power)
2. Uimara
3. Speed
 
Back
Top Bottom