MJADALA: Je, ni sahihi waimbaji wa nyimbo za dini kushiriki matamasha ya kidunia?

Lawrichie

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
752
2,044
Amani iwe nanyi nyote.

Nimeona clip ikimuonyesha muimbaji wa nyimbo za injili mchini, Goodluck Gozbert akitumbuiza kwenye tamasha la Tigo Fiesta huko Mwanza. Nimeshangaa na kujiuliza maswali;

i/Mtumbuizaji anaelewa maudhui ya tamasha lile?
ii/Waandaaji walifikiria nini kumleta muimbaji wa nyimbo za injili kwenye tamasha linalokutanisha watu wa imani tofauti tofauti?
iii/Je, kilichofanyika ni halali kidini na kijamii pia?

Karibuni tujadili na kueleweshana pale pasipoeleweka.

Nawasilisha.

Walikosa msanii mwenye mvuto wanaowataka wakaona wamchukue huyo mwimbaji wa gospel lakini walichokifanya clouds sio kitu kizuri lakini pia gozbert good luck naye asingekubali kuwa sehemu ya fiesta.
 
Mkuu, jamaa alituma maombi mwenyewe akashindanishwa na waombaji wengine, akashinda.
Kwa hiyo kama kitu hakimtii hatia moyoni muhusika na hakivunji sheria ya nchi, wacha afanye kwa utashi wake.

Alikuwa miongoni mwa waimbaji ninaowakubali sana, lakini toka atoe ule wimbo wake na kuingia Fiesta ametoka kiasi fulani..
 
Walikosa msanii mwenye mvuto wanaowataka wakaona wamchukue huyo mwimbaji wa gospel lakini walichokifanya clouds sio kitu kizuri lakini pia gozbert good luck naye asingekubali kuwa sehemu ya fiesta.

Nimeshangaa sana yani, sijui ni maamuzi gani haya
 
Siiuji sana biblia ila kunamistali muhim sana nlifundishwa na walimu wangu wa sunday school kipindi cha utoton ambayo inanikuza mpaka sasa japo mingine tunaipuuzia ila MUNGU atusaidie tu
Katika Zaburi 1:1-6
Inasema heri mtu yule asiyeenda katka shauri la wasio haki wala hakusimama ktk njia ya wakosaji wala hakuketi barazan pa wenye mizaa
Bali sheria ya bwana ndiyo impendezayo na sheria yake huitafakari mchana na usiku

SiVyo walivyo wasio haki
hao ni kama makapi mepesi yapeperushwayo na upepo
Huko kwingine mkamalizie
naOmba tumjaji kupitia hay
 
''Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu,
Lakini mwisho wake ni njia za mauti'' MITHALI 14:12
 
Kaka jamaa yuko sahihi kabisa. Neno la Mungu linahubiriwa popote pale bila mipaka ili kuwarudisha kundini waliopotea kwa anasa and etc.
 
Labda kama alimbaishia manzi stejini au alikiss stejini au alipiga bia stejini hapo sasa ndo tutamjadili
 
Anatafuta pesa kijana njaa haivumiliki.

Cha mtu chake eeh bwana chukua saizi yako.
 
Kaka jamaa yuko sahihi kabisa. Neno la Mungu linahubiriwa popote pale bila mipaka ili kuwarudisha kundini waliopotea kwa anasa and etc.

Ile ni sehemu ya burudani, watu walienda kuburudika pale sio kuhubiriwa... kwa lugha rahisi yenye alienda kuburudisha waliofika pale ndio maana alitumbuiza mpaka na viuno alikata ili watu wafurahi.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom