MJADALA: Je, ni sahihi waimbaji wa nyimbo za dini kushiriki matamasha ya kidunia?

Joined
Sep 20, 2019
Messages
43
Points
95
Joined Sep 20, 2019
43 95
Amani iwe nanyi nyote.
Nimeona clip ikimuonyesha muimbaji wa nyimbo za injili mchini, Goodluck Gozbert akitumbuiza kwenye tamasha la Tigo Fiesta huko Mwanza. Nimeshangaa na kujiuliza maswali;
i/Mtumbuizaji anaelewa maudhui ya tamasha lile?
ii/Waandaaji walifikiria nini kumleta muimbaji wa nyimbo za injili kwenye tamasha linalokutanisha watu wa imani tofauti tofauti?
iii/Je, kilichofanyika ni halali kidini na kijamii pia?
Karibuni tujadili na kueleweshana pale pasipoeleweka.
Nawasilisha.
IV MMEKOSA KAZI? mmekalia kuhukumu tu watu wakati nyie wenyewe majanga MWACHENI na maisha yake
 

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
10,637
Points
2,000

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
10,637 2,000
Kwani kuitwa FIESTA ndio maana yake tamasha la shetani..?

Wakulima tumekuwa tukisherehekea mavuno kwa kuimba na kucheza ngoma za asili, na hata hivyo burudani zimekuwepo tangu na tangu na pia matamasha ya kitaifa.... kwahiyo kila lifanyikalo nje ya nyumba za ibada ni la shetani..!!
Ndugu, hii hoja ni mfu. Kwani anayetajwa hapo ni nani? Je, ni matendo gani yanaambatana na tamasha hilo? Mbona unajitoa ufahamu kwa kutetea maovu? Kilicho kinyume na Mungu ni cha shetani, hakuna namna nyingine kuelezea. Hebu lete hoja kinzani tuone.
 

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
10,637
Points
2,000

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
10,637 2,000
Kwa waandaaji walidhamiria kupeleka mziki wa injili kwa hao watu, na ilikuwa target nzuri sababu mnawakusanya pamoja afu mnawapiga nondo za Injili

Na pia walitaka kunufaika pia kwa kuleta ladha ya tofauti kwa mashabiki wao

Kwa Mwimbaji nae pia hilo ndo lengo, pamoja na kuhakikisha kuwa wimbo wake unawafikia walengwa wake, Wimbo wake huu mpya, umeimbwa kuwalenga wakristo walio kengeuka, ambao wakiwa kanisani wanasinzia, ila wanapenda kuparty na kwenda kunywa beer, Wimbo una lengo la kuwafanya wakumbuke wanachofanya kuwa si sawa afu watafakari mienendo yao na wamuombe Mungu awasaidie.Hawa sio wakristo ambao ungewapata kokote kule kwa wingi ,zaidi ya kwenye TigoFiesta. Na wamejaa mtaani.

Na piaaa, kuhoji hili suala unakuwa hauna tofauti Na Mafarisayo walio hoji kama ni halali kwa Yesu kwenda Kula nyumban kwa Zakayo Mla Rushwa na mtoza Ushuru na kuhoji kama ni halali kwa kupakwa mafuta yule mama kahaba.

Jibu la Yesu lilikuwa simple kuwa wenye njaa ndo wanaohitaj chakula, wagonjwa ndo wanaohitaji kumuona Daktari.

Huyo mwanamziki ndo mwanamziki pekee ambae nimeona had sasa aliefanikiwa kuifikisha injili kwa walengwa.

Wengine wanapeleka injili kwa wachungaji, Injili peleka kwa walevi huko
Nondo za injili, what a joke. Nambie nondo zipi hizo zilizopigwa fiesta. Ama kweli mwapotea kwa kuyakataa maarifa
 

Forum statistics

Threads 1,343,413
Members 515,033
Posts 32,783,872
Top