Mjadala: Je, ni kweli Magari aina ya Nissan Xtrail ni mabovu?

Jozi 1

JF-Expert Member
Aug 16, 2015
6,559
2,000
Wadau nimejichanga toka 2014 mpaka leo nimetimiza lengo la kama 8000 USD nataka kuagiza Nisaan X-trail toka japan. Mwenye ujuzi wa hiz gari msaada tafadhali. Vipi ulaji wa mafuta, spea, ugumu kwa barabara za bonyokwa hukoooo...
Ni gari nzuri kwa bajeti yako tafuta NT-30 ya 2004 unaweza pata nzuri kabisa kwa $3,000
-4,000CIF.
Ina uvungu mkubwa sana hivyo hainasi kwnye magema ya barabara za bonyokwa, pia ina mfumo mzuri sana wa 4WD unapita mahali pengi patakapokushangaza hata wewe mwenyewe.
Kwa safari ndefu kale kadude ni roketi...prado nyingi na magari makubwa makubwa yatakuwa yanasoma namba na balansi yake ni nzuri.
Na nafasi ya abiria (haswa seat ya nyuma) na mizigo ni ya kutosha kqbisa.
Ila zingatia service, usivushe service ya oil...hakikish coolant ipo ya kutosha...hiyo gari injini yake ni QR 20, ikichemsha hasara yake ni kubwa..
Na epuka spear za kanjanja basi maisha yako na xtrail utaipenda sana.
 

Jozi 1

JF-Expert Member
Aug 16, 2015
6,559
2,000
Sio gari zuri kwa kua diffential zinakufa kihovyo hovyo, Pia ni gari delicate sana ingawa unaweza kufanyia safari Ila SIO gari ya kuaminika kwa sasa.
We utakuwa huzingatii service na pia utakuwa umeacha dial ya 4WD on kwenye barabara za kawaida.
Kosa kubwa sana hilo mwezi mmoja diff kwisha
 

blessings

JF-Expert Member
Jul 9, 2012
6,682
2,000
Daah sasa ikishindikana X-TRAIL itabid nirejee kwa Baby Walker (Vitz, Passo) maana nguvu ya kukwanyua RAV 4 sina halafu huku Bonyokwa wazee wa kazi wakikuona na RAV4 miezi mitatu mingi wanakujua kuichukua kama waliiweka. Range Rover (yale ya Zamani vipi wandugu) naona bei zake zipo chini japo najua wese la kutosha linahitajika. lakin najua wazee wa figisu figisu hawaangaiki nayo.
 

Ignorant

Member
Mar 9, 2008
27
45
Mimi niliagiza hilo gari miaka ya 2010 ila lilinitesa sana akaja jamaa kutoka Iringa nikambambika nalo baada ya kukaa nalo mwaka tu na kuona kiama chake

Ilikutesa vipi hasa? Funguka tafadhali kwani wengine tunaona kama 4WD yenye bei nafuu kidogo
 

Ignorant

Member
Mar 9, 2008
27
45
Ni kweli juzi.nimetoka jubilee ju renew yangu declared value 17m comprehensive insurance nimekata 595000 hii ni 3.5 percent ya 17m kabla ya hapo ilikua 3.0 percent kabla ya mabadiliko ya policy.

Thamani ya gari lako ni 17M? Je ndiyo gharama halisi uliyonunulia gari? Mie nimeangalia bei za kuitoa Japan CIF ni kama 7M na makadirio ya ushuru wa TRA ni 7M ambayo inaleta jumla ya 14M. Je la kwako uliliagiza nje? Kama ndiyo, ushuru ulilipa bei gani? Nifahamishe ili nisije liagiza nikashindwa kulitoa pale bandarini.
 

rushanju

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
2,900
2,000
Nina Xtrial na ni mwaka wa tano. Juzi nimekwenda Bujumbura na nimerudi bila tatizo. Nimepiga nayo safari ndefu maana nimeisha kwenda nalo Kampala mara tatu na hii ya juzi Bujumbura Sijaona tatizo lolote mbali ya kurekabisha ball joint mara mbili na stabilizer link tu. Na nadhani nitanunua xtrail nyingine wallah
 

platozoom

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
8,988
2,000
Daah sasa ikishindikana X-TRAIL itabid nirejee kwa Baby Walker (Vitz, Passo) maana nguvu ya kukwanyua RAV 4 sina halafu huku Bonyokwa wazee wa kazi wakikuona na RAV4 miezi mitatu mingi wanakujua kuichukua kama waliiweka. Range Rover (yale ya Zamani vipi wandugu) naona bei zake zipo chini japo najua wese la kutosha linahitajika. lakin najua wazee wa figisu figisu hawaangaiki nayo.

X-trail nakupenda kwa moyo wote.
Dugu moja. Huwa post zenu zinanifurahisha!!

Joshua_ok, blessings, soft g, andreakalima. Baba mmoja mama mbalimbali
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom