MJADALA: Je, ni kwa namna gani YouTube humlipa mmiliki wa account?

Ipo hivi, Pesa zinalipwa huko youtube kwa sababu ya matangazo, Narudia tena "MATANGAZO", mimi, wewe na makampuni makubwa iwapo tuna huduma au bidhaa tunazotaka zitangazwe tunaweza kutangaza kupitia Youtube ili bidhaa zetu zijulikane na watumiaji wa youtube.

Tukipeleka Tangazo letu youtube, Itabidi youtube tumlipe ili tangazo letu liwafikie watumiaji wa youtube.

Youtube yeye kama yeye ni kampuni tu inayoturuhusu kupandisha video, Video zinazowekwa youtube sio za youtube bali ni za wasanii, waandishi wahabari, n.k youtube hawezi kufanya chochote kwenye hizo video.

Sasa youtube tunapompa fedha atutangazie biashara zetu mimi na wewe kwa watumiaji wa youtube ina maana ya kwamba watumiaji wayaone matangazo hayo wanapotizama video za youtube

Youtube hawezi kuweka tu tangazo kwenye video za watu, Inabidi aombe ruksa ya kufanya hicho kitu kwa wasanii kama kina Diamond platnumz.

Sasa tuchukulie kwamba ndio youtube na diamond wanongea, mawasiliano yapo hivi (ni mfano tu, Diamond katumika kama mfano):,

Youtube: " Bwana diamond, kuna kampuni inaitwa jamiiforums wametengeneza app yao, wametupa tangazo lao tuwatangazie youtube liwafikie watanzania, sasa bwana Diamond tunaomba ruksa yako tuweke tangazo la jamiiforums liwe linaonekana kabla video yako haijaanza kucheza ama pembezoni, We unasemaje?"

Daimond: "Sawa, nimekuelewa Bwana youtube, matanmgazo yao nikiyaruhusu yaonekane kwenye video zangu basi itabidi na mimi mnilipe kiasi kadhaa kwenye hio pesa mliopewa,"

Youtube: "Ondoa shaka, wala usihofu kijana, wewe utachukua asilimia 55 na mimi ntabaki na asilimia 45, kwa hio kama jamiiforums walitulipa kwa kigezo cha elf 5 kwa kila watu elf 1 wataoliona tangazo wakicheki video yako wewe utachukua 2,750 na sisi tutabaki na 2,250"

Basi ndio mkataba huo unaanza kutekelezwa hapo ndipo unapoendaga kutazama video za wasanii huko youtube unakumbana na aina ya matangazo yale ambayo yanaanza kucheza kabla video uliyotaka kuicheki haijaanza na kuna kitufe cha kuruka tangazo (skip ad) ama aina nyingine ni matangazo yale ambayo yanakuaga pembeni mwa video, n.k

Jambo lingine ni kwamba watu wanaotaka kutangaziwa biashara zao kwa youtube huwa wanaseti kabisa tangazo lao liwafikie watu wa tanzania ama nchi flani, sisi watazamaji wa bongo tunayaonaga matangazo mengi ya kina vidacom ama tigo, Nao wenye biashara marekani huwa wamelenga watazamaji wa huko na ulaya.

Sasa endapo video za msanii zikitazamwa Marekani, Ulaya, Canada, n.k basi msanii anaweza kulipwa hata elfu 10 akipata views elf 1 kutoka majuu, hii ni kwasababu makampuni ya huko yanayotaka kutangaziwa biashara yana ni makubwa na pesa nyingi tu, wanaweza kulipa hata elf 20 kwa views elf 1 youtube wakachukua elf 9 msanii akabaki na elf 11, views za wabongo elf 1 msanii anaweza akabaki hata na buku tu kwasababu tangazo tutaloliona mimi na wewe tukiwa hapo buza litakua labda ni la kampuni ya ufugaji wa kuku ambayo bado ni changa
 
So location ya mwenye channel inategemea uwepo wa matangazo ili apige hela du!
 
Kwamba Youtube wanamuomba content creator wamuwekee tangazo?

Ninachofahamu youtuber(mmiliki wa channel) kama anahitaji video za channel yake ziwe monetized anapaswa kuomba akaunti ya adsense yaani kuomba YouTube Partner Program baada ya kutimiza vigezo adsense ikikubaliwa matangazo ndio yataonekana kwenye videos.

YouTube baada ya kuona malipo yao sio makubwa kiivyo hasa kwa wasanii ukilinganisha na idadi ya watazamaji, wameamua waanzishe mfumo wa Channel Membership(member hulipa kila mwezi) ambapo member wanaolipa wanaona vitu vingine na videos ambazo hazionekani kwa wasiolipia. Japo hii feature kwa Tanzania haipo ila Uganda ipo.

Kwa hiyo siku hizi sio lazima kutegemea matangazo kupata pesa youtube kwa baadhi ya nchi.
 
Mkuu sijui kama wamebadilisha sasa hivi ila nilikuwa naangalia sana hizo video na wanachoangalia ni confirmation ya umri wako
Kwamba Youtube wanamuomba content creator wamuwekee tangazo?

Ninachofahamu youtuber(mmiliki wa channel) kama anahitaji video za channel yake ziwe monetized anapaswa kuomba akaunti ya adsense yaani kuomba YouTube Partner Program baada ya kutimiza vigezo adsense ikikubaliwa matangazo ndio yataonekana kwenye videos.

YouTube baada ya kuona malipo yao sio makubwa kiivyo hasa kwa wasanii ukilinganisha na idadi ya watazamaji, wameamua waanzishe mfumo wa Channel Membership(member hulipa kila mwezi) ambapo member wanaolipa wanaona vitu vingine na videos ambazo hazionekani kwa wasiolipia. Japo hii feature kwa Tanzania haipo ila Uganda ipo.

Kwa hiyo siku hizi sio lazima kutegemea matangazo kupata pesa youtube kwa baadhi ya nchi.
 
Kama umefungua video na Tangazo limeanza kuonekana then ukaskip add kabla hujaona Au hujalimaliza. Je Bado huyo msanii etc atalipwa ?
 
Kama umefungua video na ukaskip analipwa kama kawaida ila pesa inakua ndogo atalipwa kwa mfumo wa PPM (pay per impressions) ila ili donge liwe kubwa unatakiwa uCLICK tangazo uksitazame ndo atapewa pesa nyng yaan PPC(pay per click). Ndio maana weng waTz wanaofanya blogging au affiliate marketing wanatarget sana viewers wa nje.
 
Kwamba video ikiwa na viewers wengi kama haina tangazo hakuna faida anayofaidika Mwenye video?
mwenye video hatapata kitu kama hajaruhusu matangazo, ila anaweza kujiongeza, mfano unaweza kuweka video ukichambua sifa za simu flani alafu ukaelekeza duka la kununua, hapo ikiwa duka ni lako utafaidika ila hata ukiwa dalali waweza pewa commision na mwenye duka
 
Kama umefungua video na ukaskip analipwa kama kawaida ila pesa inakua ndogo atalipwa kwa mfumo wa PPM (pay per impressions) ila ili donge liwe kubwa unatakiwa uCLICK tangazo uksitazame ndo atapewa pesa nyng yaan PPC(pay per click). Ndio maana weng waTz wanaofanya blogging au affiliate marketing wanatarget sana viewers wa nje.
ni kweli kabisa
 
Hiyo ni njia ndogo sana ambayo YouTube anaingiza hela ila kikubwa anachofanya anaongea na makampuni Mama ya mitandao ya simu kama Vodafone, Bharti Airtel, At&T yale giants mobile operator then wanauza bundle mfano umenunua bundle ya 1,000 ume stream YouTube katika 1,000 yako YouTube wana percent yao pale
 
Uongo

Maelezo hayajitoshelezi..
Mgogoro wa WCB na harmonize .. milioni 600 Kwa ajili ya kugombea matangazo tu?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom