Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,715
- 729,882
Ni kwenye kiza hiki ndio tunakutana na nafsi zetu sisi wenyewe, hatuoni kingine chochote bali hujiona wenyewe katika uhalisia wetu
Unapokodoa macho gizani na ukaona umbo la ajabu ambalo ukitaka kutazama tena kwa makini hupotea... Lile umbo ni lako ni wewe, mawazo yako ndio uhalisia wako... Wengi hupiga kelele na kukimbia kisichombilika yani unajikimbia kwakuwa huoni chochote bali unajiona wewe mwenyewe na unataka kujikimbia... Haiwezekani abadan..
Nachukulia Biblia takatifu kama chanzo muhimu kwenye mada hii kwamba katika uumbaji hakuna mahali popote inapotajwa kwamba Mungu aliumba MAPEPO hakuna... Kinachoonekana kufanana na pepo ni shetani na malaika wengine ambao Inasemekana waliasi toka mbinguni na kutimuliwa hata kabla ya sakata la Adam na Eva.... Lakini shetani sio pepo... Sasa ninini asili ya mapepo yalitokea wapi na kwanini leo yapo duniani na tutaona watu wakiombewa na kutolewa mapepo?
Lakini vilevile katikati mjadala huu tusije kuchanganya mapepo na roho za kuzimu
Kingine cha muhimu je haya mapicha ndio halisi ya mapepo kama sio basi waliyoyachora ndio mapepo wenyewe yani walijichora ama kujitengeneza.... Huwezi kutengeneza kitu usichokijua.... Juu ya yote nahoji pepo ni uumbaji toka wapi?
Mimi sio pepo