Mjadala; Je hizi ndio zama za mwisho za CCM...??

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
18,894
36,211
Habari za wakati huu wapendwa...natumaini kila mmoja ni mzima wa afya na wale wenye kadhia mbali mbali za kimaisha Mungu yu pamoja nasi....

Kila macho na mioyo ya wapenda demokrasia na mabadiliko yalikuwa kwenye uchaguzi uliopita...ambapo mshindi amepatikana kimiujiza au niseme kwa njia wanazozijua wao maana kwenye box la kura kila mtu anaju kuwa nani ni mshindi.....

Lakini pia tumeshuhudia nguvu nyingi ikitumiwa na chama tawala katika harakati za kuwaaminisha wapiga kura kuwa bado wanastahili kuendelea kutawala......katika harakati hizo tumeshuhudia wale wale waliokuwa wakiaminika kuwa ni vigogo wa CCM na wengine kwa kauli zao wakijinadi kuwa kamwe hawawezi kuondoka CCM lakini mwisho wa siku tumeshuhudia wakitiririka mithiri ya maji kuelekea upinzani.....Hakika vita ilikuwa kali na ndio hali iliyopelekea chama tawala kutumia nguvu nyingi kwenye harakati zao za kuelekea ikulu.....

Uchaguzi ulikwisha na matokeo yalishatoka na kupitia matokeo hayo yameonyesha na jinsi gani CCM kilivyo chokwa na kila mwenye akili timamu na utashi wa kutambua baya na zuri....CCM imepoteza manispaa nyingi maeneo ya mijini na hata huko walikoshinda ni kwa njia za kihuni na wala sio kwa njia za kidemokrasia.....

Sasa swali la msingi ni kuwa ni kwanini CCM WANATUMIA NGUVU NYINGI KUENDELEA KUBAKI MADARAKANI....???
JE KWAMBA WATU WAMESHAWAJUA KUWA NI WALAGHAI NA HIVYO KUONA KUWA HAWANA HAKI YA KUENDELEA KUTAWALIWA NAO.....

JE HAIWEZEKANI HIZI ZIKAWA NI DALILI ZA MWANZO ZA ANGUKO KUU LA CCM HAPA NCHINI.....

Karibuni wadau....
 
Back
Top Bottom