Mjadala huru: Nini chanzo cha kukithiri kwa ajali za barabarani nchini Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjadala huru: Nini chanzo cha kukithiri kwa ajali za barabarani nchini Tanzania?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kibol, Oct 25, 2012.

 1. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,137
  Likes Received: 378
  Trophy Points: 180
  Ajali za barabarani nchini Tanzania zimekuwa zikisikika kila uchao, leo utasikia basi fulani limepata ajali mahali fulani na kuua watu kadhaa kesho napo hali kadhalika, imekuwa kama watanzania tumeanza kukubaliana na kuizoea hii hali, tumekuwa mara zote tunasema kazi ya Mungu haina makosa, tunamsingizia Mungu vitu ambavyo viko ndani ya uwezo wetu, makosa yetu wenyewe tunampakazia mtu mwingine.

  Ajali za barabarani nchini zimechukua nafasi kubwa ya 'Israel mtoa roho' kwa jinsi kila siku zinavyotoa roho za watu, najua kuna watu wengi watajiuliza kwa nini sijazungumzia ajili nyingine kama za majini nk lakini lengo langu ni kuanzia na hizi ambazo zimekua zikisikika mara kwa mara.

  Nafikiri ajali za barabarani kama zisipotafutiwa ufumbuzi mujarabu zitaendelea kuua kila uchao nasi ajabu mukaja kuziita janga la kitaifa, unapotaka kutafuta jawabu la kitu fulani ni lazima kwanza uwe na background information ya hicho kitu hali kadhalika tunapotaka kutafuta ufumbuzi wa hili tatizo hatuna budi kuangalia its root causes, nini chanzo chake? Bila hivyo tutaendelea kulia kila siku kwa kuwapoteza wapendwa wetu (dada,kaka,mama,baba zetu nk).

  Sina takwimu hasa lakini sisi wenyewe tumekuwa ni mashahidi wa haya tunayoyasikia kwenye vyombo mbali mbali vya habari.

  Karibuni jamani tushirikiane katika kutafuta ufumbuzi yakinifu wa tatizo hili.
   
 2. L

  Lyambasa Senior Member

  #2
  May 5, 2015
  Joined: Sep 24, 2013
  Messages: 104
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wadau huwezi amini kuwa kuna pepo watatu hapa Tanzania wanaongoza kusabisha ajali ambao huwatumia madereva nao ni pepo STRESS za maisha na pili pepo simu za mkononi na tatu pepo ulevi wa pombe.Hii ni kutokana na utafiti wangu kupitia slogan "Solution through nature&experience"
   
 3. Gazaniga

  Gazaniga JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2015
  Joined: Apr 12, 2015
  Messages: 1,053
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Umesahau mkuu wa mapepo hayo Chichiemu.
   
 4. L

  Lyambasa Senior Member

  #4
  May 5, 2015
  Joined: Sep 24, 2013
  Messages: 104
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hao ndio wamiliki au?
   
 5. Amaholo

  Amaholo Member

  #5
  May 5, 2015
  Joined: Apr 27, 2015
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani hivi tujiulize, mbona ajali zimezid tokea mwaka Jana? Ndo kusema hao madereva uzembe, stress vimeanza tokea mwaka Jana?
   
 6. Amaholo

  Amaholo Member

  #6
  May 5, 2015
  Joined: Apr 27, 2015
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mambo haya yapo ktk ulimwengu wa roho na tukipeleka kufikiri ktk ulimwengu wa mwili tutakesha pasi na kupata majibu ya kwanini ajali zimezid.
   
Loading...