TODAYS
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 13,730
- 21,130
Amani kwako.
Wakati dunia imegubikwa na mjadala mkubwa wa kupigwa na janga la ugonjwa wa corona virus wa mwaka 2019 ambao kiukweli ugonjwa huu hauchagui umpige nani tajiri au masikini na unaugulia hapa hapa hakuna India wala Afrika kusini.
Wakati mjadara mkubwa ni covid-19, jamii kama wasomi, viongozi, wenye hekima na wananchi wa kawaida kila mtu anaongea lake na wengine wanaomwamini Mungu na Allah leo wanapinga kama Mungu hawezi kufanya maajabu kwenye covid-19!.
TWENDE KWENYE MADA.
Viongozi wengi duniani mara baada ya kuapishwa, wamekuwa wakienda nchi za nje kwa nia ya kujitambulisha, kujenga urafiki kiuongozi, kidipromasia nk.
Wanaokwenda huko nje kuna wanaokwenda na malengo binafsi, kiserikali na wengine kutembea kuangalia kukoje huko kwa wakoloni au kusaini mikataba fake, kufungua account huko visiwani nk.
Tulejee kwa issue ya rais wa nchi kwenda ulaya kujitambulisha ambapo tunaweza kujiuliza mpaka sasa JPM hajapanda ndege kwenda popote kwa lengo hilo ila kwa issue za kiserikali tena hapa hapa afrika.
Ukivuta picha ya viongozi wengine na JPM utagundua tofauti kubwa kati yao na uwenda nasema uwenda JPM atakuwa ni kiongozi wa nchi ambaye amefahamika na kutajwa sana kuliko kiongozi mwingine wa nchi yetu bila kupanda ndege kwenda kujitambulisha.
Hilo linaweza kuwa ni jambo la kipekee hata kama linaweza lisiwe na impact kwake lakini anachokifanya kwa taifa tutaliona kesho, leo ni vigumu kuona analofanya.
Hali hiyo imenipelekea kutaka tuwe na mjadara huru kwetu wanajf na wale wanaopita kusoma pia wapate nafasi kujiuliza.
Unaruhusiwa kutoa povu.
Nawasilisha.