Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,987
- 20,271
Wengi tumekuwa tukistaajabu kwa umasikini unavyozidi kulisulubu taifa letu, unaweza kuwadhani baadhi ya Watanzania kama vile walikuwa uhamishoni kwa jinsi wanavyo lalamika kwa ugumu wa maisha, lakini hilo si wao tu bali ni kila mmoja, hata Jakaya ukimuuliza kuwa kwanini Tanzania ni masikini atakuambia SIJUI.
Mimi narejea nyuma baada ya uhuru, Tanzania ilikuwa na uchumi endelevu na wastani mzuri wa idadi ya watu, Unaweza usiamini lakini ni ukweli uliowazi kuwa enzi hizo Taifa lilitegemea Tumbaku, Pamba na Mkonge kupata pesa za kigeni, na ilimudu kwa kiwango kikubwa kuwapa wanachi wake hudumu muhimu kama hospitali na shule.
Chini ya vita ya ujinga, maradhi na umasikini, Tanzania ilianza kukua kiuchumi hasa ikiabudu na kuakisi mifumo ya uchumi wa kijamaa sanjari na kuchagiza uzalendo halisi kwa wakaazi wa Tanzania bila shuruti,
Machipuko mema na ndoto imara za Mtakatifu Julius K. Nyerere zilianza kuzaa matunda hasa baada ya Tanzania kuzaliwa na kuitwa nchi ya viwanda vidogovidogo vyenye kuwalisha watanzania uhalisia wao.
Lakini ndoto na machipuko hayo yalikabiliana na upinzani wa mabeberu wa ndani waliofanikiwa kupenyeza sera zao na zikafanikiwa kuingia nakuliangusha rasmi taifa na ndoto huru za mtakatifu J.k. Nyerere zikatutoka na leo hatujui kwanini sisi ni masikini.
Miaka ya 1980+ paliibuka sera iliyoitwa Economy Recovering Program (ERP), mpango huo ulipendekeza viwanda ambavyo wao waliviita havina tija vifungwe. Hakika hili lilipelekea idadi kubwa ya viwanda vyetu kufungwa na hata vile vilivyobaki serikali ilivitelekeza kasha wakaibua dili lingine walilolipa jina la uwekezaji lakini mimi nasema WIZI.
Mimi najaribu kutafakari huku nikistaajabu ya Musa, hawa waliokuja nasera hii ya ERP ndio leo wanaojiita wawekezaji kwa mwamvuli wa nje.
Jambo lakushangaza kama taifa, bado hatujajua wapi tulikosea ili tujisahihishe.
Wadau naomba tusaidiane kujibu huenda jibu langu ni tofauti na lako, Kwanini watanzania ni masikini? Tumlaumu nani?