Mjadala: Gharama na njia nafuu za kujenga nyumba ya kuishi Tanzania

Habari Wakuu!! Nina kiwanja changu ukubwa 30-20. Udongo wake ni Mfinyanzi nipo nje kidogo ya mji kama Km 4 hv na nina mdoto ya kujenga nyumba ya kawaida ila iwe angalau na kigorofa cha chumba kimoja

Ni nini napaswa kuzingatia kabla sijaanza chochote? na je kwa ukubwa huu naweza kufanya ujenzi huo?
 
Upo sahihi mkuu, mimi nyumba yangu ina sq 100 na hadi sasa imecost around 50mln.
Kwa haraka haraka nitakupa makadirio maana ndizo kazi zangu hizo chukua square meter za ramani yako times 500,000 utapata garama ya morden house with everything you need.

Kama hujaelewa nina maana Urefu X Upana X 500,000=Construction cost

Hapo nina maana unatumia mkandarasi.
 
Wewe @ bwegebwege: kwanini usi convert hizo $ kabisa into Tsh. Badala ya kuleta mazima, unatusumbua au wewe wewe unaishi USA
Kwa kukupa picha kidogo:

Mimi nina ongoing project, imefika kwenye linter, (Nyumba ya kawaida): 1 Masterbedroom moja, 1 Guest Room with attached toilet, 2 other Bedrooms, Study room 1, Laundry, Kitchen, Public Toilet & Bath, Dinning Room na Sitting Room...hadi sasa tayari $65,000 zimekatika!

I just received estimates ya kupauwa (Kwa bati pana) ni kama $18,000..hapo ni mbao, mabati na ufundi etc. Sasa nikianza kufikiria finishing nahaisi nitapaswa kuwa na kama $30,000 nyingine (total kuanzia kuezeka)! Hapo sijaweka hesabu ya fence.....

Kwa mantiki hiyo bosi waliosema uwe na kama 100,000,000/= kwa uchache hawajakosea (ingawa mimi nashauri uwe na kama 160,000,000/=
 
Kwa kukupa picha kidogo:

Mimi nina ongoing project, imefika kwenye linter, (Nyumba ya kawaida): 1 Masterbedroom moja, 1 Guest Room with attached toilet, 2 other Bedrooms, Study room 1, Laundry, Kitchen, Public Toilet & Bath, Dinning Room na Sitting Room...hadi sasa tayari $65,000 zimekatika!

I just received estimates ya kupauwa (Kwa bati pana) ni kama $18,000..hapo ni mbao, mabati na ufundi etc. Sasa nikianza kufikiria finishing nahaisi nitapaswa kuwa na kama $30,000 nyingine (total kuanzia kuezeka)! Hapo sijaweka hesabu ya fence.....

Kwa mantiki hiyo bosi waliosema uwe na kama 100,000,000/= kwa uchache hawajakosea (ingawa mimi nashauri uwe na kama 160,000,000/=
Kiongozi umepigwa pakubwa mno,ndio shida ya kujenga kwa simu,kwa 130M unapata nyumba ya ghorofa moja chini vyumba vinne na juu vitatu,other wise hiyo130M uibreak down tuone umetumia tofari ngapi,mifuko ya cement mingapi na mchanga na kokoto kiasi gani,hata hiyo roofing ya usd 18,000 karibia 40M nayo ivunje vunje tuone zinatakiwa bati ngapi na mbao kiasi gani ndio utafunguka macho kujua umepigwa kiasi gani,mfano kwa ukubwa wa myumba hiyo haiwezi tumia bati zaidi ya bati 120,tufanye unatumia bati za ALAF za migongo mipaka ile futi 10 wanauza 45,000 kwa bati moja mara 120 unapata only 5.4M hope umepata mwanga huyo mtu wako anavyokupiga live
 
Jamani naomba niulize kwa wana JF ambao ni wataalamu wa ujenzi.

Naomba wanipatie bajeti ya kujenga nyumba ya kawaida yenye vyumba 5, sebule, kitchen, dinning na sitting room ina cost kwa makisio shilingi ngapi?

Naomba nielimishwe,

Asanteni.

======
SIMILAR CASES:
Soil stabilized bricks... Adobe stabilized bricks... kutegemea mazingira uliyopo na fining unayohitaji kufanya je uezekaji ni bati, nyasi au vigae...
 
tupieni vi raman simple vya kisasa na bei affordable kwa mtu wa kawaida,nawasilisha ombi wakuu
bagamoyo_2#0.jpg

kama hii ina 12m*10m, ni 52 bati za kawaida. though tofali ni nyingi kidogo
 
Habari Wakuu!! Nina kiwanja changu ukubwa 30-20. Udongo wake ni Mfinyanzi nipo nje kidogo ya mji kama Km 4 hv na nina mdoto ya kujenga nyumba ya kawaida ila iwe angalau na kigorofa cha chumba kimoja

Ni nini napaswa kuzingatia kabla sijaanza chochote? na je kwa ukubwa huu naweza kufanya ujenzi huo?
Panajengeka vizuri tu,kitakachofanyika ni udongo kubadilisha
 
Yes kama ni gorofa unazidisha mara mbili au unachukua square meter za juu times 500,000 plus sqm za chini times 500,000 sum up the two values u will and get the roughly approximation.

Tatizo wabongo hampendi kutumia wataalam wa kazi hizo unajikuta mafundi wanawaibia wanafanya vitu vya low quality,jifunzeni kutumia wataalam katika kazi ambazo hamna utaalamu wake.

Kwa mfano unaweza ukamtumia quantity surveyor akakupa quantity ya material na garama yake hapo unapata picha halisi ya garama ya nyumba yako na ni kwa garama nafuu tu pale UCLAS wapo vijana wazuri tu hata mtaani. Ukihitaji contact za hao watu ni PM
Ahsante sana Ndg manyusi.Mimi binafsi ni Mtanzania na napenda kuwatumia wataalamu, lakini gharama zao wakati mwingine si rafiki ndio maana mtu anajikuta kaingia mitaani.Mimi ninaomba kuuliza kama nataka kujenga chumba kimoja standard master bedroom Mbagala ina maana gharama yake itakuwa wastani 7 square metres X 500,000= TZS 3,500,000? Je hii ni bei ukimpa mkandarasi anakupa chumba kimekamilika? Ahsante sana kwa mahesabu ya kitaalamu.
 
Mm nlijenga nyumba yangu huku kijijini kwetu moshi
Kiwanja ni cha uridhi
Nyumba ya vyumba vitatu na choo ndani +sebule na baraza mbele

Kupandisha boma nilitumia 3ml tofali za new land za kuchoma na mawe ya chupa lorry
Mchanga lorry 2@180000
Mawe lorry 4@90000
Cement 25@14500
Funding 350000
Nondo20ml12@18000
Tofali lorry2 @47000
Saidia fundi nkawa mwenywe mwanzo mwisho kitambi yote ikaisha

Baada ya hapo nkatulia kwa muda

Mwezi wa pili nkatumia 2.7ml kupauwa na nkahamia
Mbao 3×4 150@6000
Bati za kawaida 60×18500
Misumar kg25(sikumbuki being
Funding 500000
Dirisha 4@90000 za chuma
Nkaziweka vioo zote( sikumbuki ni ela ngap)

Nkahamia na watoto na wife na sasa hivi wife mjamzito

Haina plaster vyumbani wala tiles choo na bafu natumia vya nje na jiko langu LA kuni maisha yanaendelea namalizia nkiwa humo humo ndani

So ww jenga tu ukifuata maneno ya watu huku ndani utaishia kusugua pymbu kwenye vijumba vya kupanga tu
 
Nakubaliana na SMU huo mjumba balaa, yaani mkubwa kweli kweli.

Ukijenga mjumba wa size hiyo jee watoto wako wakishaondoka wamemaliza shule utaufanya nini? Vile vile ni kujihakikishia idadi kubwa ya wageni kwa muda wote kwani kuna nafasi ya kutosha.

Maintenance costs ndio hazisemeki, unaweza kufaidi for the first four to five years, baadae ndio harakati za maintenance zinapoanza hapo.

Halafu TRA watakapokupiga hiyo property tax ndio utakoma ubishi.

Majumba ya aina hiyo yalikuwa yanajengwa mnamo miaka ya tisini sio sasa hivi.
Jibu zuri sana hili tena inabidi liangaliwe kwa makini sana na kila mtu anayeplani kujenga au kununua nyumba kwa matumzi ya familia. Nilikuwa na nyumba ya vyumba vinne Marekani ikiwa na vyoo vinne, sebule ya familia (family room), sebule ya wageni (living room), Jiko kubwa tu, Breakfast area, dining room, laundry room, bar, movie theater, na home office mbili. Nyumba ilitutosha sana mimi, mama watoto na watoto wetu wawili kwa matumzi yetu ya kila siku ambapo watoto walikuwa wanaweza kuwaleta marafiki zao kwenye sleepover au hata kuangalia movie na kucheza video games, kufanya homework bila bugudha na wakichoka wanaweza kulala. Baada ya miaka 15 tangu tujenge jumba hilo, watoto wamekomaa na wameondoka nyumbani na kutuachia sehemu kubwa sana ambayo haitumiki tena. Property Tax ya nyumba inaongezeka kila mwaka!

Ninataka kuliuza lakini sasa nostalgia ya watoto inakuwa ni kikwazo! Plan with care!!
 
Hii imekaa sawa kweli? ina maana kwa nyumba ya vyumba 5 alioulizia mkuu inaweza kuwa around Tzsh 25 - 30 Million?.

Hii ukikadiria kwamba kila chumba kitakuwa na ukubwa wa 10 square meters. ((10 x 5) x 500,000) = 25,000,000.

Kwa utaratibu huu mbona gharama zitakuwa ni ndogo ukilinganisha na gharama tunazozisikia kila siku?
Ulikuwa mtoro kwny darasa la namba, eeh??
 
Back
Top Bottom