Mjadala: Gharama na njia nafuu za kujenga nyumba ya kuishi Tanzania

Kwa haraka haraka nitakupa makadirio maana ndizo kazi zangu hizo chukua square meter za ramani yako times 500,000 utapata garama ya morden house with everything you need.

Kama hujaelewa nina maana Urefu X Upana X 500,000=Construction cost

Hapo nina maana unatumia mkandarasi.
hii ilikuwa takwimu ya lini!? Kuna update ama bado iko vile vile!?
 
*NAMNA SAHIHI ZA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UJENZI*


*Habari Boss*

*Karibu Sana Tuelimishana Namna Sahihi Zaidi Kadhaa Za Kukusaidia Kupunguza Gharama Za Ujenzi Wa Mradi Wako*

Unaweza Ku-Share(Kushirikisha) Ujumbe Huu Kwa Watu Wako Wa Karibu, Unaweza Kuwasaidia Sasa Au Wakati Mwingine Kwa Namna Moja Au Nyingine

Ahsante

Kwanza kabisa kabla hujafikiria kupunguza gharama za ujenzi unatakiwa kufahamu gharama halisi za ujenzi, tatizo ni kwamba watu wengi huwa wanataka kupunguza gharama za ujenzi wakati hawana uelewa mzuri wa gharama halisi za ujenzi zilivyo. Ni vyema ukajua kwanza nyumba/jengo fulani la ukubwa fulani na ubora fulani katika mazingira fulani linagharimu kiasi gani cha fedha mpaka kukamilika ndio ufikirie uwezekano wa kupunguza hizo gharama ili ujue umeokoa kiasi gani cha fedha katika mradi huo.

*Sasa twende tuangalie mbinu mbalimbali za kupunguza gharama hizi za ujenzi;*

1. Namna ya kwanza na pengine sahihi zaidi ya kupunguza gharama za ujenzi ni kuwa makini na ukubwa wa jengo husika, kwa sababu ukubwa wa jengo unachangia kwa kiasi kikubwa sana ukubwa wa gharama za ujenzi wake, kwa hiyo kupunguza vile visivyo na umuhimu na kupunguza ukubwa wa functions za ndani ya jengo kama sio muhimu sana kwako ni njia ya kwanza sahihi sana. Huwa inashangaza mtu anaweza kukwambia nataka unitengenezee nyumba ndogo ya gharama nafuu ya vyumba vitano viwe vikubwa, mtu anataka nyumba ndogo ya bei nafuu lakini yenye vyumba vingi halafu viwe vikubwa. Weka vyumba ambavyo ni standard, kama ni nyumba ya kuishi unaweza kuchagua baadhi ya vyumba kama vile sebule na masterbedroom viwe vikubwa kiasi labda na jiko liwe na nafasi ya kutosha kupangilia vinavyohitajika na vyumba vingine viwe vya kawaida.
Kama ni majengo ya biashara au ofisi unaweza kupunguza "dead spaces"(maeneo yasiyotumika) kuondoa visivyo na ulazima na vingine vya namna hiyo.

2. Namna ya pili sahihi kupunguza gharama za ujenzi ni kutengeneza ramani halisi ya jengo lako. Ukiwa na michoro iliyofanywa kwa kuzingatia gharama unaweza kuepuka kutumia gharama zaidi kwa sababu utakuwa tayari umefanya makadirio ya ujenzi ambapo utaondoa uwezekano wa kuongezewa gharama zitakazoweza kuongezeka aidha kwa kuongeza jengo kiholela au kupunguza chochote kutokana na kukosa mwongozo au kwa wasimamizi wasiowaaminifu kudanganya kwa kuongezea chochote usichokifahamu.

3. Namna ya tatu sahihi ya kupunguza gharama za ujenzi ni wataalamu wa ujenzi kufanya kazi kwa pamoja kwa ushirikiano huku wakiweka kipaumbele katika kupunguza gharama. Kwa mfano structural engineer(mhandisi mihimili) anaweza kushauriana na architect(msanifu/mbunifu majengo) namna ya kupunguza idadi ya nguzo au upana wake kwenye baadhi ya maeneo ili kuepuka kutengeneza dead spaces zitakazolazimu kutengeneza spaces zaidi kufidia hizo spaces zilizochukuliwa na nguzo, bila kuleta madhara

4. Namna ya nne sahihi ya kupunguza gharama za ujenzi ni kufanya kazi na watu waaminifu. Hii itakusaidia kuepuka uwezekano wa kuibiwa au kuongezewa gharama (variations) ya kitu chochote kutokana na loopholes zinazoweza kuwepo kwenye makubaliano.

5. Namna ya tano sahihi ya kupunguza gharama za ujenzi ni kuufuatilia mradi kwa makini na kuuelewa vizuri, hii itakusaidia kujua ni kitu gani cha muhimu au kisicho cha muhimu kinachoweza kuondolewa ambacho kinasababisha gharama bila sababu za msingi baada ya kuzungumza na wataalam wako na kuelewana.

6. Namna ya sita sahihi ya kupunguza gharama za ujenzi ni kama una pesa yote ya mradi husika unaweza kukaa chini na wataalam wako mkapanga namna ya kusimamia ununuzi wa vifaa mkatafuta maeneo wanakouza vifaa vya ujenzi kwa bei nzuri ya jumla mkafanya manunuzi ya jumla. Jambo hili linahitaji umakini mkubwa sana kwa sababu unaweza kufika mbele ya safari katika huo ujenzi ukakuta ulichonunua hakifai au pengine kimeharibika na hakifai tena kwa sehemu iliyokusudiwa au ukawa umeamua kubadilisha baadhi ya vitu au mpangilio wa jengo lenyewe, ndio maana nasisitiza ni vyema kwanza kukaa chini na wataalam mkajadili kwa makini sana usije kujikuta unajiingiza kwenye hasara badala ya kupunguza gharama.


*NOTE; Kutaka kuepuka gharama kwa kufanya ujenzi kienyeji hasa kwa miradi mikubwa kunaweza kukusababishia aidha kujikuta kwenye gharama zaidi ya zile ulizokuwa unaepuka mwanzo au kusababisha maafa kwa watu kutokana na kuchakachuliwa kupita kiasi, au jengo kudumu kwa muda mfupi na kupelekea ukarabati wa mara kwa mara unaohusisha gharama nyingi ambazo zingeweza kuepukwa mwanzoni kwa kufanya maandalizi makini*

Kwa leo tuishie hapo
Ahsante na karibu sana

Please share
 
Ndugu kuna ksnuni gani ya kupata idadi ya bati na mbao za kupaulia nyumba?
Inakubidi ujue kwanza vipimo halisi vya jengo lako,angle ya mnyanyuo wa paa la nyumba yako,aina ya bati utakalopaulia nyumba. Baada ya hapo ndio unaweza kufanya mahesabu ya idadi ya bati na kiasi cha mbao zitakazohitajika kufanya kazi hiyo.

Kama unaweza kuwa na michoro ya jengo lako au vipimo halisi,naweza kukusaidia kutokea hapa.
 
Kwa ukubwa huo wa kiwanja izo tofali elfu mbili kasoro haziwezi hata kumaliza upande mmoja,labda ukubaliane nami kwamba umekosea maandishi ktk uwasilishaji i.e badaya ya kuandika square meter ukaandika square kilometer.

Pia natumai ulishapata fundi wa kukamilisha kazi hii na kama bado basi nakukaribisha nikusaidie kukutengenezea gharama za kumalizia ukuta uujengao.
Kama kichwa kinavyojieleza hapo juu, nina kiwanja cha square kilometer 400, nimeshazungusha ukuta upande mmoja bado pande tatu ni kama tofali elfu 2 kasoro hivi za nchi 5 na 6 jumla.
Nipeni gharama zake au fundi mzuri aende aone site then tuongee bei.
Contacts 0716282670.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mada imepamba moto; naombeni kujua, hivi kwa hapa Tanzania nikitaka prefabricated houses zinapatiakana? Kwa yeyote mwenye kufahamu naomba anisaidie kujua katika hilo kwa undani
Naam,prefab houses zinapatikana hapa tanzania. Kuna makampuni yanafanya kazi hizo kwa sasa.
 
Huwa inashangaza sana,mtu anakupa kipimo cha umbali kwa kutumia muda... wanatoa akilini umbali kupimwa kwa mita au kilomita...
Robo saa ndo umbali gani!!??
Robo saa kwa miguu au kwa gari? Kama ni kwa miguu vipi kwa mlemavu wa miguu naye atatumia robo saa kutembea!!? Tuwe serious.
Kwanini usiweke umbali halisi kwa KM?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri mzuri, lakini akiamua kwenda mdogomdogo kwa maana ya kuanza na msingi anatulia kwanza wakati anagunduliza ya hatua inayofuata
Mpaka finishing haiwezi kutosha mkuu,kwanza hapo ktk m.5 toa m.2 ya tofali.Ninahakika ktk ramani ya iyo lazima ziingie tofali 2000

Utakuta umebakiwa na m.3 sasa fundi mpk kuimaliza kujenga iyo nyumba atataka pengine laki nane mpka milioni moja.....

Utabakiwa na m.2 bado kupauwa ambapo hapo ndio pazito na hujachimba shimo la choo na ukatengeneza mwisho kabisa finishing pia pazito hapo mkuu ila anza ivyo usirudi nyuma ujenzi huwa hauwishi kwa siku moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi sana, kwakweli umenitia moyo,
Lakini kwa kuanza si inakubidi uanze msingi wote halafu ndipo unaanza kunyanyua chumba kimoja kimoja?
Upo sahihi sana ndugu mie nilikua na iyo hela nikaanza na chumba kimoja seble choo cha public na jiko nw nyumba yangu INA vyumba vitatu vya kulala kujenga n taratibu anza tu ivo 2

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naitaji nifyatue matofali naomba kuuliza mfuko mmoja wa cement naweza toa matofali imara mangapi?
 
Back
Top Bottom