Mjadala: Gharama na njia nafuu za kujenga nyumba ya kuishi Tanzania

Naomba kufahamu, kujenga flat roof au Norma roof kipi ghali??
Flat Roof ni nafuu ila ina changamoto nyingi za kiufundi kuliko normal roof flat roof inakuwa na slop ndogo hivyo ni rahisi kuvuja katika misumari, pia flat roof ukuta unakuwa unaloa mno hivyo kupelekea ukungu katika kuta na some times maji kupenya ndani katika ceiling board
 
Wadau nilikuwa napenda kuwauliza nahitaji nondo za 16mm sijui ni kiasi gani kwa rolla
 
Habari za muda huuu wanajamvi
Naomba nina mdogo wangu wa kiume amemaliza degree ya ualim sayasi Biology & chemistry mwaka huu 2018 sasa amejibana bana amepata 50000(elfu hamsini) je ni biashara ngani au ni kitu gani anaweza kufanya hasa mazingira ya DAR HASA GONGO LA MBOTO NA MAENEO YA KARIBU AU HATA ENEO LOLOTE KATIKA JIJI LA DAR na kikamuingizia kipato huku anasubri hizi ajira za serikali maana tempo znasumbua

USHAURI TAFADHAR
 
Unaweza sana sana 50 ni nyingi sana ni mtaji wa kununua viatu(raba) pc5 kila moja utainunua 10 elfu zungusha kitaani kila moja utauza 25 elfu mwisho ishirini elfu kwa siku moja pambana mpaka uuze pc 2 mwisho wa mwezi utakuwa una sii chini ya laki tatu maisha yatasonga mbele karibu mjini ss tulishapazoea###umachingaunalipakuliko kufungua hata duka na mikodi kibaao##
 
Unaweza sana sana 50 ni nyingi sana ni mtaji wa kununua viatu(raba) pc5 kila moja utainunua 10 elfu zungusha kitaani kila moja utauza 25 elfu mwisho ishirini elfu kwa siku moja pambana mpaka uuze pc 2 mwisho wa mwezi utakuwa una sii chini ya laki tatu maisha yatasonga mbele karibu mjini ss tulishapazoea###umachingaunalipakuliko kufungua hata duka na mikodi kibaao##
Honegera mkuu kwa mawazo chanya. Hapo wengi watasema haitoshi
 
Ujenzi wa nyumba umekuwa changamoto kwa watu wengi kwa sababu ya kukosa taarifa sahihi juu ya ujenzi wa nyumba.

Ujenzi wa nyumba ni zaidi ya kuwa na tofali na kiwanja pekee. Ujenzi wa nyumba ni mchakato na sio tukio. Inabidi muhisika atathimini mambo mengi kabla ya kuanza kuwekeza kwenye nyumba. Maana ukikosea, utaishi na nyumba hiyo kwa maisha yako yote na utazidi ona hayo makosa kila siku.

Njia bora na sahihi kabisa ni kujua
1: kupata nakala zote za ujenzi kuanzia ramani na michoro ya ujenzi

2: Nani atajenga nyumba yako, awe kampuni au fundi wa kawaida

3:aina ya 'material ' utakayotaka kutumia kwemye ujenzi; kama mawe, mchanga, simenti na nondo. Mbao na bati/vigae

4: thamani ya nyumba ikiendana na muda. Nikimaanisha katika vifaa utakavyotumia. Je, Ni bora kununua bati na ukawa unabadilisha kila miaka mitano au kiweka vigae vya simenti ambavyo vinakaa zaidi ya miaka 30?

Lengo langu la leo ni kuzungumzia aina ya "material" yatumikayo hususani matofali.

AINA ZA TOFALI

1: Solid blocks

Hizi ni tofali za kawaida ambazo wengi wetu tumezizoea kutumia. Zinaanzia mara nyingi inchi 8,6 na 4. Inchi 5 sio kipimio halisia, ila tunatumia sana Tanzania kwa sababu ya kupunguza matumizi ya siment au kupata tofali nyingi zaidi.

Tofali hizi ni nzuri kwa maana ya uzito. Hivyo zinafaa sana kutumika msingi. Ila wengi wetu tunatengenezea hadi kufikia usawa wa kupaua.

Ukipata tofali lililo tengenezwa kwa vipimo husika, basi nyumba yako.itakuwa ngome ambayo itaishi muda mrefu sana.

Kwa gharama zake ni kubwa ukilinganisha na zingine nitazozitaja.

2: HOLLOW BLOCKS (tofali zenye uwazi)

Hizi ni tofali ambazo zinakuwa na uwazi katikati. Nazo hupatikana kuanzia ukubwa wa inchi 8,6, na 4. Inchi tano hazipo nyingi ila ukipata fundi makenika akatengenza mould utaipata tu.

Tofali hizi zina sifa ya kutumia kiasi kidogo sana cha mchanga na simenti ukilinganisha na pacha wake wa solid blocks. Mbali na hayo, sifa zingine za tofali hizi ni kuwa unapata tofali 4-6 za ziada kwa kila tofali 10 aina ya solidi. Nikimaanisha kwa kiwango kilekile cha simenti na mchanga unachopata tofali 10 za solid, utapata tofali 14 za hollow hadi sita. Hivyo kwa namna moja ama nyingine unapunguza gharama za ujenzi kwa wanaopenda tofali za hollow.

Pia tofali hzi zinasifa ya kuwa kuzuia mzunguko wa sauti/kelele ndani ya nyumba kati ya chumba na chumba. Pia zinazuia upotevu wa joto wa nyumba, ni nyepesi hivyo msingi wa nyumba utaishi miaka mingi sana. Mbali na hayo pia inakupa urahisi wa kupitisha huduma zingine kama.bomba za maji na umeme bila kutindua ukuta.

Ujenzi wa nyumba kwa tofali hizi unapunguza gharama kwa kiasi cha 30-50% ukilinganisha na ujenzi wa tofali za solid


3: INTERLOCKING BRICKS

hizi ni tofali za kuumana. Zinatengenezwa katika maumbo na vipimo tofauti tofauti kutokana na mahitaji. Utengenzwaji wake unahitaji mashine maalum. Ambazo zinapatika kwa gharama kati ya 17mil mpaka 34mil kutokana na uhitaji wake(automated machines) ila kuna zile za NHC wanazogawa zinaweza zisizidi 3mil.

Mara nyingi tofali hizi zinahitaji kiasi kidogo cha simenti katika mchanganyiko wa udongo uliokuwa na ufinyanzi kidogo na mchanga. Mara nyingi baada ya kuuzalisha tofali zinazohitajika kwa ujenzi. Basi ujenzi wake ni wa haraka sana na unachukua muda mfupi. Ujenzi wa tofali za kuumana baada ya nje ya mashine, gharama za ujezni zina pungua mpaka 50-65% wakati wote. Hivyo kufanya kuwa ujenzi wa bei nafuu kuliko wote kwa ujenzi wa tofali. Maana matumizi ya cement yamekatwa kwa kiwango hicho hicho.

4: BURNT CLAY BRICKS

Hizi ni tofali za kuchoma. Ambazo Zinatengenezwa kwà kutumia udongo mfinyanzi tu. Mara nyingi uzalishaji wake ni wakawaida kwa watu wa vijijini. Ila mijini tulikiwa na kiwanda kinaitwa kibrico ambacho kilikuwa kinazalisha tofali hizi. Kwa ujezni wa kienyeji yaani kununua tofali zake kienyeji basi unaweza kupunguza gharama.ila tafiti hazijaonesha kwa kiasi gani. Shida ya ujenzi huu ni kuwa aina ya utengenezaji unafajya tofali zisiwe na mwonekano mzuri hivyo kumlazimu mjenzi kurekebisha mara kwa mara na kuwa na tofali mbovu nyingi. Japo kama zikipatikana vizuri ujenzi unafaa.

Nakaribisha maswali juu ya ujenzi kwa ujumla na ushauri
Ungeweka picha ya kila aina ya tofali ingefaa sana hasa hizo hollow blocks.bei za interlocking au hollow blocks zikoje
 
Mhh,najaribu kujiuliza,nimenunua mbao za kenchi,bati,na kuezeka,grill kutengenezwa na kuwekwa,kumwaga jamvi na gharama za mafundi vyote kwa ujumla vimenigharimu zaidi ya 12M,nimesimamia mwenyewe na vyote nimenunua mwenyewe....!!hiyo 15m kujenga nyumba hadi inaisha,itakuwa ni nyumba aina gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama hii hapa Chini,vyumba 2 vyote self contained jiko/chumba sebule na public toilet ya nje
 

Attachments

  • IMG_20180809_134712.jpg
    IMG_20180809_134712.jpg
    54.9 KB · Views: 252
Hio nyumba ya kujengwa kwa 15 milioni labda ulijenga banda la KUKU sio nyumba ya kuishi. Paa tu, linakomba hio 15milion
Kwa dimensions alizozitaja huyo jamaa hapo huo ni uongo unless amelipua na haina finishing yeyote ya maana ila kwa nyumba ya dimension ya 8.2mx7.45m inamalizika kwa finishing ya wastani but inayoridhisha
 
Nakataa kabisa Mkuu. Nimejenga nyumba kama hiyo hadi kupaua na madirisha plus milangu imekula 12,000,000. Bado mziki wa finishing hapo
Inategemea sehemu uliko na choice yako ya materials pia bargain yako na Fundi unaowatumia na msimu wa kujenga.Mikoa ya nyanda za juu huhitaji cement kujengea isipokua rental na plaster,kenchi ni milingoti isipokuwa papi na branderings,nondo u just need za 10mm instead of 12mm and 8mm,hata plaster nje inafanyika around foundation,kuanzia usawa wa madirisha kwenda juu na kuweka mkanda wa plasta/koplo kuzungusha madirisha yote etc na namna nyingi tu za kufanya economy building bila kuathiri ubora na muonekano.
Kwa kufuata hichinachokwambia kwa nini usimalize nyumba,pia tafuta wataalam wawasaidieni kwenye ratio na paa ambazo ni economy with good impression otherwise local fundi wamewatia watu wengi hasara
 
Hii imekaa sawa kweli? ina maana kwa nyumba ya vyumba 5 alioulizia mkuu inaweza kuwa around Tzsh 25 - 30 Million?.

Hii ukikadiria kwamba kila chumba kitakuwa na ukubwa wa 10 square meters. ((10 x 5) x 500,000) = 25,000,000.

Kwa utaratibu huu mbona gharama zitakuwa ni ndogo ukilinganisha na gharama tunazozisikia kila siku?
hujamuelewa, amesema unatafuta eneo la nyumba mara 500,000. Eneo la nyumba halitafutwi kwa idadi ya vyumba
 
Kwa haraka haraka nitakupa makadirio maana ndizo kazi zangu hizo chukua square meter za ramani yako times 500,000 utapata garama ya morden house with everything you need.

Kama hujaelewa nina maana Urefu X Upana X 500,000=Construction cost

Hapo nina maana unatumia mkandarasi.
Kama hautumii mkandarasi????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom