Mjadala: Gharama na njia nafuu za kujenga nyumba ya kuishi Tanzania

Wanajamii nina swali/maswali
Mosi: naomba kujuzwa makadirio ya idadi na gharama za mbao kwa nyumba yenye urefu mita 10 na upana mita 9

PIli:makadirio ya idadi ya bati migongo mipana.
 
Kwa haraka haraka nitakupa makadirio maana ndizo kazi zangu hizo chukua square meter za ramani yako times 500,000 utapata garama ya morden house with everything you need.

Kama hujaelewa nina maana Urefu X Upana X 500,000=Construction cost

Hapo nina maana unatumia mkandarasi.
Hii hesabu kakufundisha mwalimu nani, maana sio mchezo umejiongeza...butwhy 500,000 is fixed why not 200,000
 
Kinachopishanisha gharama za ujenzi kwa experience yangu niliyoipata ni gharama za material ya ujenzi bei zina cheza sana kulingana na wakati, utakachopata ni bei elekezi tu kwa wadau lakini ukiingia sokoni vitu bei vipo juu unaweza kukata tamaa kujenga,
 
Hapo kiongoz inategemea unaezeka kwa mtindo gan either flat roof (eg hidden roof) au pitched roof na hapa ukisema unaitaj bat liende juu Sana yaan (45°) au kawaida(30-35°) naweza kupa jubu sahii kiongoz
Naomba makadirio ya 45 na ya 30-35
 
Saiv wstaalam wengi na wengi wao wameingilia soko la ujenzi bila kuelewa ujenzi wenyewe mwishowe wanapewa kazi wanakimbia.so client kuweni makini na hilo.
 
Nipo moshi pia kuna kaeneo nataka kujenga.... Tuwasiliane.... Unipe hii experience yako aisee......

0718321418
Mm nlijenga nyumba yangu huku kijijini kwetu moshi
Kiwanja ni cha uridhi
Nyumba ya vyumba vitatu na choo ndani +sebule na baraza mbele

Kupandisha boma nilitumia 3ml tofali za new land za kuchoma na mawe ya chupa lorry
Mchanga lorry 2@180000
Mawe lorry 4@90000
Cement 25@14500
Funding 350000
Nondo20ml12@18000
Tofali lorry2 @47000
Saidia fundi nkawa mwenywe mwanzo mwisho kitambi yote ikaisha

Baada ya hapo nkatulia kwa muda

Mwezi wa pili nkatumia 2.7ml kupauwa na nkahamia
Mbao 3×4 150@6000
Bati za kawaida 60×18500
Misumar kg25(sikumbuki being
Funding 500000
Dirisha 4@90000 za chuma
Nkaziweka vioo zote( sikumbuki ni ela ngap)

Nkahamia na watoto na wife na sasa hivi wife mjamzito

Haina plaster vyumbani wala tiles choo na bafu natumia vya nje na jiko langu LA kuni maisha yanaendelea namalizia nkiwa humo humo ndani

So ww jenga tu ukifuata maneno ya watu huku ndani utaishia kusugua pymbu kwenye vijumba vya kupanga tu
 
Ndugu wanaforum,

Naomba Ushauri wenu juu ya ujenzi wa nyumba Dar.

Kutokana na uwezo mdogo, nimeshauliwa nitumie system inyoitwa interlocking blocks, amabyo inatumia tofari zinazotokana na mchanganyiko waudongo wa kisuguu na cement.

Swali:
Je, hii teknolojia ipo Dar?
Je inasaidia kupunguza gharama za ujenzi na kwa % ngapi ukilinganisha na nyumba ya tofali za Cement za kawaida?
Je, nyumba hiyo inaweza kudumu mda mrefu kama ya cement?

Nipeni ushauri ndugu zangu.
Hiyo nyumba hsina tofauti na ya cement.
Ina umaridadi pia.
Technologies Dar ilianza siku nyingi kuna Mashine special ya kupiga tofali hizo inaitwa Hydraform inatoka South Africa.
 
Ndugu wanaforum,

Naomba Ushauri wenu juu ya ujenzi wa nyumba Dar.

Kutokana na uwezo mdogo, nimeshauliwa nitumie system inyoitwa interlocking blocks, amabyo inatumia tofari zinazotokana na mchanganyiko waudongo wa kisuguu na cement.

Swali:
Je, hii teknolojia ipo Dar?
Je inasaidia kupunguza gharama za ujenzi na kwa % ngapi ukilinganisha na nyumba ya tofali za Cement za kawaida?
Je, nyumba hiyo inaweza kudumu mda mrefu kama ya cement?

Nipeni ushauri ndugu zangu.
Hiyo nyumba haina tofauti na ya cement.
Ina umaridadi pia.
Technology hiyo Dar ilianza siku nyingi kuna Mashine special ya kupiga tofali hizo inaitwa Hydrafom inatoka South Africa
 
Kwa raman hii nikitumia tofali za kuchoma..... Itani cost bei ngap?
Kama upo sehemu ambazo msingi /foundation wanatumia mawe, basi andaa:
TRIP =12-15 za mawe.
TOFALI= 2800-3000-BLOCKS
MCHANGA =TRIP 10
CEMENT =70
NONDO=( MM12=26 & MM10=22)
NOTE; GHARAMA ZA BOMA
 
This was really great Chief
Si kweli mkuu, maisha mazuri ni mipango mizuri, bidii na kujinyima tu. Halafu vilevile usitishwe na hesabu za wadau humu ndani, unaweza kuwa na altenative ukajenga kwa gharama nafuu tu.

Kuna kajengo ambako nimefanya kama kijihotel flani uchwara mkuu, ramani yake ni balaa haswa, nikiweka hapa nitakuwa naexspose ID, lakn nilichofanya ni kuchukua ramani yangu, nikatafuta constructor wa kkusuka foundation, kkunyanyua beams na kazi zote za zege, mkataba wake ukaishia hapo. Nikanunua tofali za kuchoma,Nikatafuta mason mzuri akapandisha kuta kwa bei nafuu sana, nikatafuta vijana wengine wa roofing kwa robo tu ya bei ya constructor, Jengo likawa limesimama, Nikatafuta interior designer kwa ajili ya ushauri tu lakini kazi halisi nikachukkua vijana wa wanaofanya kazi kwenye makampuni ya ujenzi wakafanya kazi zote zilizobaki.

Mpaka nafungua sehem hiyo nimeweka mpaka vitanda na gadgets zingine daftari linasoma chini ya M650! (10 executive rooms+a descent restaurant, bar & kitchen !).

Ninachotaka kusema ni kwamba, kazi ukiizoea kiasi unaweza kujua fundi mzuri nampata wapi na kwa bei gani, pia unapunguza kuibiwa na mafundi ukkiwa karibu nao wakati wote wa ujenzi.

Ukigawa project yako katika smaller projects unapunguza gharama hapa kwetu bongo.
 
Kwanza kwa wote mliochangia hii post nawaomba niwagongee senksi,kwa sababu ile kitufe cha kubofya senksi hakionekani kwangu.

Pili kuna nyumba (flat) ni mpya vya vyumba vitatu inauzwa kwa milioni 53 hapa Tanga.

Naomba wadau mniambie ni deal nzuri kununua au ni vizuri kujenga mwenyewe kwa hapa Tanga?

Asanteni.
Nyumba za kununua jau mkuu
 
Kwa haraka haraka nitakupa makadirio maana ndizo kazi zangu hizo chukua square meter za ramani yako times 500,000 utapata garama ya morden house with everything you need.

Kama hujaelewa nina maana Urefu X Upana X 500,000=Construction cost

Hapo nina maana unatumia mkandarasi.
Ina maana nyumba ya sqm 414 ni 207 million? tutakuwa hatujengi
 
NINASHUKURU KWA HESABU, NINAHAKIKA NEXT EASTER I WILL BE IN MY HOUSE AT MASAKI AREA SQUARE YA NYUMBA KATIKA RAMANI NI 455m SQUARE. KWELI BONGO LAINI
So 455 x 500000 haya bwana ngoja niwahi zangu mihogo kwa Lulenge
 
Back
Top Bottom