Mjadala: Gharama na njia nafuu za kujenga nyumba ya kuishi Tanzania

Eti "baba mwenye nyumba"..? Unaweza kugharamia elimu ya mwanao akitaka kusoma course ya Off-shore Engineering chuo kizuri ULAYA..? Vp mkeo akpata tatzo linalohitaji kwenda India kwa matibabu utagharamia au "heshima ni nyumba" tu..?
Mkuu mbona povu? Ulitaka aitwe baba mwenye gari?
 
mkuu nasikia 500,000 per square metre ni ya zamani sana.

nimeambiwa na wataalamu (QS na contractors) kuwa haya ni makadirio ya TBA ambayo hayako realistic kwa wakati tulio nao.

hawa wataalamu wanadai eti siku hizi iko kwenye 700,000 kwenda juu.

tuendelee kuelimishana.
Kiwango cha chini cha makadirio ni viwanda na maghala ambapo makadirio yao ni 550,000@m
 
Khaa we kweli mwenzangu na mimi kwenye hesabu, yaani hapo nihivi
Anatakiwa aangalie katika raman ya nyumba yake kuna scale wengi hutumia m au wengine cm then kama wametumia cm uta convert to m mfano nyumba yako ina urefu 1600cm kwa upana 1300cm maana yae itakuwa ni mita 16 x mita 13 x 500000 = 104,000,000/= na hilo ndo jibu sahihi.

Ujenzi huu jamani duh. Na hela yenyewe ndo hii ya kimazabe mazabe. Nadhani ni mda muafaka kwa wenye hela (makampuni na watu binafsi) kuanza kujenga nyumba za low cost housing na kukopesha watu tulipe taratibu. Maana huu ujenzi unashawishi watu waibe! Nyumba million mia mbili?..hiyo ni income ya miaka mingapi kwa mtumishi wa umma?

mkuu nasikia 500,000 per square metre ni ya zamani sana.

nimeambiwa na wataalamu (QS na contractors) kuwa haya ni makadirio ya TBA ambayo hayako realistic kwa wakati tulio nao.

hawa wataalamu wanadai eti siku hizi iko kwenye 700,000 kwenda juu.

tuendelee kuelimishana.
Wakuu ieleweke kuwa haya makadirio ya ujenzi ya 550,000 kwa viwanda, 650,000/7500,000 na 850,000 kwa business apatimenti ni kwa ajili ya AQRB kukokotoa gharama za mradi na kwa kwa ajili ya ma Architect na QS kukokotoa gharama zao za u consultant. Hazina uhusiano sana na manunuzi ya ujenzi, ukiwa makini katika manunuzi wala hutakaribia makadirio hayo
 
kiongozi.kupaua nyumba ya kawaida yenye vyumba vya kulala 3 makadilio sh ngapi ufundi
 
Kiufup cost estimation ya nyumba haiitaj kubuni japokuwa inaitwa cost estimation. Among factors ni kujua squaremetre za jengo lenyewe, plan ya nyumba, aina ya finishing, umbali wa materials had eneo LA site nk. Kufanya baadh ya survey za materials costs. Kitu kingine n kwamba, kuongezeka au kushuka kwa cost inadepend pia na umakin ya supervisor wa site. Majibu ya mtandaon yanaweza yasimatch kwa swali lako. Cha msing ungemtumia mjenzi mwnywe kwa kazi hyo au kama Si hivyo bas umtumie expert yeyote ambaye ametembelea site na kuiona plan yako..kumbuka kuwa mahesab feki yanapelekea ugomvi bifu kwa mjenzi wako pale atakapo hitaj pesa nyngine nje ya hesab ulizopewa.
 
Mkuu wewe ni mjenzi au una uzoefu wa kutosha, umesema nilichowahi kukisema, nashangaa watu hapa wanapewa vipimo na kutoa gharama kimzaha.
Mjenzi makini hana msjibu ya juu juu, mwisho wake utaitwa mwizi matirio yasipotosha kama ulivyokadiria awali
 
ujenzi ni changamoto. Wengi bado hatujawa na uelewa sahihi umuhimu wa kutumia wataalamu wa ujenzi. Mwisho wa siku tunapenda nyumba nzuri lakini wengi tunaamini watalaam watatuibia.
 
ujenzi ni changamoto. Wengi bado hatujawa na uelewa sahihi umuhimu wa kutumia wataalamu wa ujenzi. Mwisho wa siku tunapenda nyumba nzuri lakini wengi tunaamini watalaam watatuibia.
 
Bongo kila mtu fundi, unahitaji ramani ya nyumba tafuta mtaalam, unatafuta kujua gharama za ujenzi tafuta mtaalam, unataka kujenga tafuta mtaalam lakini majibu ya mtandaoni hayana msaada wowote zaidi ya kutengeneza comflicts tu mathalan mimi kwenye finishing ya rangi nimetumia crystal paints siwezi kulingana na mtu mwingine alietumia rangi ya kawaida japo nyumba na designs ni ileile, vilevile kwenye milango nikitumia aluminum doors haitalingana sawa na alietumia timber doors kwa ramani ileile hivohivo kwa vitu vingine pia kwenye jengo hivo gharama za ujenzi zinategemea na
(1) Aina ya ramani husika
(2)Aina ya materials itakayotumika
(3) Pia site ilivyo(hatuwezi kulingana mimi niliejenga eneo ambalo liko flat na ambae eneo lake linamwinuko)
(4) Upatikanaji wa materials mpaka kufika site
(5) Aina ya udongo eneo la site pia lina determine aina ya foundation hivo kupelekea gharama ya foundation kupaa au la
Niishie hapo kwanza ila mambo ni mengi mno kwenye ujenzi huwa yanaibuka huwezi fanya makadirio kirahisi rahisi kama unavyofikiria
 
Nimeona leo niweke hapa uzi kuhusu mambo ya ujenzi,
Ili wale wenye ujuzi na mambo ya ujenzi watupe mawili matatu,
●Pia wakiweza watupe mipango jinsi ya kujenga nyumba za gharama nafuu,

●Pia kuweza kupata ramani kwa bei nafuu.

●Na jinsi gani unaweza kujenga kwa pesa ndogo na kesho ukajikuta upo katika nyumba yako.

●Na kukuelimisha ukitaka kujenga unatakiwa kujenga katika kiwanja cha aina gani.

●Je viwanja visivyopimwa vinafaa kujengwa?

●Kuelimishwa ujenzi wa ghorofa ni vitu gani vya muhimu vinahitajika.

●Hatua zipi za msingi kabla ya kununua kiwanja kwa mtu.

Mobile Traveller
 
Uzi mzuri sana huu mafundi njooni hapa kwa ufafanuzi mzuri utakaotoa usishangae ukaanza kupokea simu nyingi tu za kukutaka kazini sababu utashuhudia umahiri wako

Sent from my HUAWEI Y221-U22 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom