Mjadala: Chadema mjipange kuwaenzi mashujaa hawa wanaoangamia katika harakati | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjadala: Chadema mjipange kuwaenzi mashujaa hawa wanaoangamia katika harakati

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by USTAADHI, Sep 4, 2012.

 1. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #1
  Sep 4, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  katika hali inayoonesha kuwa ni mkakati wa polisi na serikali kuidhooofisha CHADEMA na kwa kuwa ni dhahiri kuwa kwa sasa swala la polisi kuuwa ni la mwendelezo ombi langu kwa CDM kama mtakuwa na kikao chochote cha kujadili mauaji haya ni vyema pia mkakubuka kuanzisha utaratibu wa kusaidia wajane na yatima wa watu wanaouwawa na polisi kama ishara ya kuwaenzi HAYATI wote waliouwawa
  namaanisha uanzishwe mfuko wa mashujaa wote waliouwawa tangu TARIME ,IGUNGA,MOROGORO,ARUSHA,IRINGA, na kwingineko wakiwa katika harakati za kuleta mabadiliko ili kuzipa moyo familia zingine zijue pia kuwa CHADEMA kama msemaji wa wanyonge yuko tayari kuhakikisha usalama wa yatima katika elimu na katika afya na mambo muhimu yote ie ALL SOCIAL SERVICES
  na mfuko huu utangazwe vyema hata humu jf tushiriki barabara TIZAMA NDUGU ZANGU WANA JF HATA HAWA WATOTO WA HAYATI MWANGOSI WATAISHIJE? tunaamini chadema you can do initiation we are ready to provide you a support NAOMBA MAWAZO HAYA YACHUKULIWE SERIOUS AHSANTENI nimeandika lakini siko vizuri moyo wangu unauma kwa haya polisi wanayofanya
   
 2. M

  Makyomwango JF-Expert Member

  #2
  Sep 4, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 323
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Well said, naunga mkono hoja hii.
   
 3. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #3
  Sep 4, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  ni wazo toka kwa great thinker, na hasa huo mfuko ni vema ukaanza mapema hata kabla ya kuchukua dolla kwani vifo huko mbele kuanzia mwakani ni vingi sana kulingana na mpango mzima wa magamba.Hata hivyo sura ya mwangozi imetia majonzi sana watanzania, nahisi haIGP mwema naye kasononeka hata yule muuwaji pia .Ni matumaini yetu mungu ataepusha.
  Yawezekana pia Mwangosi ni mfano wa PAULO NA SILA wa Tanzania
   
 4. Varbo

  Varbo JF-Expert Member

  #4
  Sep 4, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 1,025
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  naunga mkono hoja na nipo tayari kuchangia kama hili wazo litafanyiwa kazi
   
 5. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #5
  Sep 4, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,731
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Dokta slaa afikishiwe haya maneno, nliumia sana nlivofiwa na baba japo nlikua mkubwa nlivona yule kijana kakumbatiwa na slaa nimekumbuka nami nlipofiwa na baba,. Pole sana watoto wa mwangosi
   
 6. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  mpaka sasa ndugu wanajf ccm hawajatulia mpango wao ni zaidi ya mauaji sasa yatakuja maangamizi nape alichozungumza na wenzake ni ishara ikikumbukwa kuwa nchi haina mkuu
   
 7. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Nashauri tuanzishe daftari maalum la kuweka kumbukumbu za wanaouwawa na kuteswa. Binafsi nimeanza na majina haya ya mashujaa wetu.
  1. Dr Steven Ulimboka
  2. Daudi Mwangosi
  3. Ali Arizona

  Naomba tuwe tunarekodi tarehe zao na miezi, tukishachukua nchi tufanye assessment ya michango yao waingie katika siku ya mashujaa, naamini tutaifanyia marekebisho siku hiyo ili iweze ku-accomodate mahujaa wa kizazi chetu dhidi ya CCM na serikali yake.

  Tafadhali naomba majina ya waliouwawa Mbeya, Arusha, Tarime, Igunga ili niongeze kwenye kumbukumbu za chama najua yatatumika siku moja.
   
Loading...