MJADALA: Baada ya Spika kujiuzulu ni hatua gani hufuata?

econonist

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,345
2,000
Ni wakati wa nchimbi kuwekwa ili amsafishie Njia mama hapo 2025?na yeye alipwe fadhila ya umakamu wa Raisi kama mgombea mwenza??Tuone sasa hatma ya maamuzi haya!! Je The State wameridhia maamuzi ya kumuondoa spika kisa maono yake???je Mama atatengenezewa kashfa ya rushwa kisa kulazimishwa na wenye dola kujiuzulu uraisi wake???ngoja tuone!!

Hivi hii nchi haina watu wengine zaidi ya hao hao wasiokuwa na jipya. Huyu nchimbi uwaziri ulimshinda akajiuzulu kipindi Cha kikwete.
 

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
10,389
2,000
Leo unamtetea Ngugai? Ni maajabu
Kuna jambo la kutetea hapo mkuu, siyo mtu bali mhimili, so tujifunze kitu hapa.

Hata akiwa Lissu ndiye spika likitokea kama hili tutaisemea nafasi siyo Lissu, maana nguvu iliyopo pale inatokana na cheo siyo mtu, so mtu akikosea tunamshutumu kwa kuidhalilisha nafasi.
 

This is...

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
3,458
2,000
Hakuna shughuli yoyote itakayotekelezwa na Bunge isipokua uchaguzi wa spika wakati ambao kiti cha spika ki wazi.
 

Babe la mji

JF-Expert Member
Dec 14, 2019
818
1,000
Mkutano ujao wa bunge ukiketi tu mchakatoa wa kumtafuta spika mpya utaanza.Ataptikna mpya.
 

Mwanga Mkali

JF-Expert Member
Jul 8, 2018
756
1,000
Ndiyo Mara ya kwanza speaker kujiuzulu Tanzania
Kama ilivyo mara ya kwanza Rais kufa, mara ya kwanza kuwa na rais mwanamke na itakavyokuwa mara ya kwanza rais kushika wadhifa huo kwa kipindi kimoja.... yote yanaendelea kutokea kwa mara ya kwanza.
 

Panctual Fwenga Boy

JF-Expert Member
Jun 11, 2019
307
500
V8 yenye kibao cha SB na bendera vimeshakua historia.
1.V8 itabaki kuwa yake
2. Ataendelea kulipwa 80% ya mshahara wa spika atakayekalia kiti kwa maisha yake yote.
3. Ataendelea kutibiwa kwa gharama za serikali mpaka kufa kwake.
4. ..,...,.......,..!
 

fimboyaasali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
5,142
2,000
Habari WanaJF,

Wote tumeona taarifa ya Kujiuzulu kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naomba kujuzwa yafuatayo;

Je, Hatua gani hufuata kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya Nchi?

Je, Naibu Spika anachukua madaraka Moja kwa Moja?


Karibuni Wajuvi

======

KWA MUJIBU WA KATIBA ya Tanzania ()

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amejiuzulu nafasi hiyo kuanzia leo Januari 6, 2022 kwa hiari yake mwenyewe kwa kulinda maslahi ya Taifa, serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania (84) ibara ndogo ya 8 kinaeleza kwamba, pindi kiti cha spika itakapokuwa wazi, hakuna shughuli yoyote itakayotekelezwa katika Bunge (isipokuwa uchaguzi wa Spika) wakati wowote ambao kiti cha Spika kitakuwa wazi.

Hii inamaanisha kwamba, ili shunguli za bunge linalotarajiwa kuanza Februari 1, 2022 ziweze kuendelea, ni lazima kwanza limchague Spika.

Kwa mujibu wa katiba, (84)(1), spika atachaguliwa na wabunge kutoka miongoni mwa watu ambao ni Wabunge au wenye sifa za kuwa Wabunge; atakuwa ndiye kiongozi wa Bunge na atawakilisha Bunge katika vyombo na vikao vingine vyote nje ya Bunge.
Nafasi inatangazwa,na watu wenye nia wataomba,wale watajaopitia vyama vyao,hivyo vyama vitateua wagombea na watapigiwa kura,atakayeshinda ndio spika

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
56,547
2,000
Kama ilivyo mara ya kwanza Rais kufa, mara ya kwanza kuwa na rais mwanamke na itakavyokuwa mara ya kwanza rais kushika wadhifa huo kwa kipindi kimoja.... yote yanaendelea kutokea kwa mara ya kwanza.
Na itakua mara ya kwanza Tanzania kuongozwa na chama ambacho si CCM.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom