MJADALA: Baada ya Spika kujiuzulu ni hatua gani hufuata?

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,618
2,000
Habari WanaJF,

Wote tumeona taarifa ya Kujiuzulu kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naomba kujuzwa yafuatayo;

Je, Hatua gani hufuata kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya Nchi?

Je, Naibu Spika anachukua madaraka Moja kwa Moja?


Karibuni Wajuvi

======

KWA MUJIBU WA KATIBA ya Tanzania (🇹🇿)

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amejiuzulu nafasi hiyo kuanzia leo Januari 6, 2022 kwa hiari yake mwenyewe kwa kulinda maslahi ya Taifa, serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania (84) ibara ndogo ya 8 kinaeleza kwamba, pindi kiti cha spika itakapokuwa wazi, hakuna shughuli yoyote itakayotekelezwa katika Bunge (isipokuwa uchaguzi wa Spika) wakati wowote ambao kiti cha Spika kitakuwa wazi.

Hii inamaanisha kwamba, ili shunguli za bunge linalotarajiwa kuanza Februari 1, 2022 ziweze kuendelea, ni lazima kwanza limchague Spika.

Kwa mujibu wa katiba, (84)(1), spika atachaguliwa na wabunge kutoka miongoni mwa watu ambao ni Wabunge au wenye sifa za kuwa Wabunge; atakuwa ndiye kiongozi wa Bunge na atawakilisha Bunge katika vyombo na vikao vingine vyote nje ya Bunge.
 

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
30,546
2,000
Utulivu atachukua kiti cha uspika, na kisha kijana mpendwa (wa mchongo) atapendekezwa kua naibu.
Baada ya hapo Mgogo ataanza kuugua na kabla ya 2025 atang'ata shuka wakati chama chao kikiwa kime pata ombwe la mpasuko.
NAHISI NIMELEWA...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom