Mjadala: Anaestahili kugharamia pesa ya kutolea ni mtumaji au mpokeaji?

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,273
21,386
"Tuma na ya kutolea" ni moja ya kauli maarufu sana kwa watumiaji wa pesa kwa njia ya simu!

Kabla ya teknolojia hii ya pesa mtandaoni kuingia; pesa zilikuwa zinatumwa kwa TMO na EMS, etc.

Watu walipanda bus kufuatilia madeni ya pesa zao mkono kwa mkono na kukabidhiana pesa zikiwa cash pasipo kupungua.

Utata ulipo sasa! Nani anaestahili haswa kukatwa au kulipia pesa ya kutolea kati ya mtumaji au mpokeaji?

Mtumaji: Je ni sahihi kutuma pesa bila kuweka ya ziada kwa mpokeaji?

Na wewe mpokeaji: Kwanini uombe ya pesa ya ziada tofauti na mapatano?

TIRIRIKA HAPA
 
Inategemea unamtumia nani ya kwenye matumizi gani...
Kama ni biashara tuma na ya kutolea
Kama umemtuma mtu akufanyie Manunuzi tuma na ziada
Kama ni mzazi tuma na ya kutolea
Kama ni mhitaji tuma na ya kutolea
ILA KAMA NI MCHEPUKO TUMA KAMILI

Jr
 
Sasa kama ya kutolea ni mhimu basi iwe kwa wote! Iweje mchepuko usiuwekee ya kutolea?
 
MTUMAJI NDIO MWANZISHAJI WA MUAMALA,YEYE NDIO SOURCE OF MONETARY TRANSACTION,KWAHIYO KAMA NDIO CHANZO TUNA ASSUME KWAMBA ANAYEMTUMIA HANA CENT NDIO MAANA AKATUMIWA..SASA UTAMKATA MTU ANAYETUMIWA!LOGIC HAIWEZEKANI
 
Binafsi situmi pesa ya kutolea. Nikikutumia pesa na ikaingia kwenye simu yenye jina lako naamini hiyo pesa tayari ni yako. Ukiamua kuitoa iwe cash ni maamuzi yako hivyo unawajibika kwa maamuzi hayo. Otherwise endelea kuiacha kwenye simu maana ni yako.
 
MTUMAJI NDIO MWANZISHAJI WA MUAMALA,YEYE NDIO SOURCE OF MONETARY TRANSACTION,KWAHIYO KAMA NDIO CHANZO TUNA ASSUME KWAMBA ANAYEMTUMIA HANA CENT NDIO MAANA AKATUMIWA..SASA UTAMKATA MTU ANAYETUMIWA!LOGIC HAIWEZEKANI
Kama Mtumaji angekuwa hana simu akakuomba Ufuate kwake pesa yako JE NAULI YA KUFUA PESA HIYO NANI ANGELIPIA KAMA SIYO WEWE?
Sasa iweje kwenye miamahala umuombe na ya ziada wakati kakuepushia adha ya nauli ?
 
Kama Mtumaji angekuwa hana simu akakuomba Ufuate kwake pesa yako JE NAULI YA KUFUA PESA HIYO NANI ANGELIPIA KAMA SIYO WEWE?
Sasa iweje kwenye miamahala umuombe na ya ziada wakati kakurahisisha ?
Tunapozungumzia miamala ya kielektronic, kuna baadhi ya vitu huwa exclusive kulingana na terms,na mifumo wenyewe.
 
Nikikuomb 10000 ukatuma kumi, je nikienda kuitoa itakuwa kumi tena?

Mtumaji ndio unapaswa kutuma na ya kutolea maana ungetuma hata kwa basi ungelipa gharama ya kuituma wewe sio mimi mpokeaji.
 
Inategemea unamtumia nani ya kwenye matumizi gani...
Kama ni biashara tuma na ya kutolea
Kama umemtuma mtu akufanyie Manunuzi tuma na ziada
Kama ni mzazi tuma na ya kutolea
Kama ni mhitaji tuma na ya kutolea
ILA KAMA NI MCHEPUKO TUMA KAMILI

Jr

Mmesikia awali wakisema kama ni mchepuko tuma kamili, lakini mimi nawaambia usichepuke kabisa.
 
Back
Top Bottom