Mizizi inyonyayo rutuba ya uzalendo Tanzania

LUCAS KISIMIR

Member
Sep 11, 2012
29
4
View attachment 72941View attachment 72941View attachment 72941

Nakubaliana na maudhui yaliyopo kwenye Makala ya Maggid Mjengwa ya kichwa kisemacho CCM NA NJIA YA KINANA iliyokuwa posted kwenye JAMII FORUMS ikitokea kwenye Gazeti la RAIA MWEMA. Uchambuzi wa aina hii ndio pia unaotakiwa katika mitandao ya kijamii. Inaonekana michango mingi kwenye magazeti inatoka kwa watu makini na wenye upeo kuliko ilivyo katika mitandao ya kijamii ingawa nayo magazeti mara zingine hukumbwa na kiharusi! Mjengwa amelenga katika kututazamisha masuala muhimu ya jamii yetu kwa kuonesha mfano wa aina ya uchambuzi wenye tija tunaouhitaji kwa sasa. HONGERA SANA. Huo ndi uzalendo unaotakiwa hapa Tanzania. Ni makala ya thamani kubwa. Baba wa Taifa alisema, “Kukosoa, kukosoana na kukosolewa ni silaha ya kimapinduzi” Kukubali kukosolewa sio umbumbumbu bali ni kuboreka kifikra na kimtazamo. Huwezi kuwa shujaa kwa sababu hukosoleki! Makala hii ni ya kujadiliwa kwa kuwa ndani mwake, humo, kuna uchambuzi wa kina unaoweza kuitibu Tanzania ambayo imevamiwa na uoza wa kimaadili. Tusiache kuujadili hoja hii kwa kuwa umeandikwa na Maggid Mjengwa tunayemfahamu na katika hili, tutenganishe baina ya yeye Maggid kama mtu na hoja aliyoiwasilisha. Tuanzie hapo.

Uoza huo unajiimarisha kila kukicha ndani ya sekta zote za kijamii kuanzia mila, AZISE, Asasi za kidini, utendaji Serikalini na katika ngazi ya kaya! Maggid Mjengwa kaandika maneno yafuatayo na hivyo kusema ; “Ni kwenye ‘siasa za mafungu’ ndipo utawakuta wana-CCM wenye kudhani wao ni wasafi, na wenzao ni wachafu. Wakati, kimsingi, jamii nzima kwa sasa ni kama imeoza kimaadili. Leo utawakuta wala rushwa CCM, na hata kwenye vyama vya upinzani. Utawakuta makanisani, misikitini na hata kwenye sekta ya michezo.”

Kasema tena yafuatayo; “mradi wa kujivua magamba haukulenga kwenye kubadili mfumo uliosababisha tatizo, bali , ulichukua sura ya mbio za Urais wa 2015, na hivyo, ukabeba sura ya kuwindana kisiasa ( Political Witch Hunting) zaidi miongoni mwa wana-CCM wenyewe kuliko kukijenga na kukiimarisha chama chao”.

Mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla wake, vipo katika kuhangaika na kutapatapa kutafuta mbadala popote, hata ikiwa kwamba mbadala wenyewe hausimami kwa miguu yake. Kutapatapa huku kunafanana na mtu aliye kwenye mawimbi yatokanayo na mafuriko. Mtu aliyeko ndani ya kadhia kama hiyo, fikra yake haimsadii kufikia katika maamuzi yenye tija kwake yeye na wale wanamzunguka. Kutapatapa ni kiashiria cha hatari inayomkabili mhusika kwani katika kutapatapa huweka matumaini yake kunako mazingira yasiyofanyiwa uchambuzi, jambo ambalo ni nadra kupata matokeo bora. Mara nyingi katika hali hii, mambo hutekelezwa kama yanavyokuja na kama matukio na matokeo yake ndiyo yenye kupata wasaa wa kutathminiwa kwa mfumo ufananao na ule wa kutafuta chanzo cha kifo!
Nataka niwatanabaishe WaTanzania wenzangu kwamba, ni vema kujadiliana kwa uangalifu, kwa kina na katika wakati, faida na hasara ya kufanya uamuzi kwa suala zito. Unaweza kuliuza gari lako kwa kuwa unazo sababu za msingi. Huwezi kuliuza gari lako kwa kuwa ni chakavu na kununua gari jingine chakavu kwa hoja kwamba lina usajili wa namba nyingine! Huwezi kuliuza gari lako kwa kuwa unataka fedha za nauli ya kusafiria kwenye daladala na humo ukadai haki ya kuketi kwa nafasi ya kujiachia! Ukisha-kuuza gari ukanunua baiskeli, basi, ujiandae pia kurekebisha ratiba ya safari zako!

Maadili ya kijamii tuliyomo hayajipambanui kwa msingi wa dini, kabila wala chama. Ni kizazi!

CCM ndicho chama chenye kutawala hivi sasa kwa maana ya Sera na Ilani. Tulikubaliana na uamuzi wa kuachana na CHAMA-DOLA na kuingia kwenye siasa ya vyama vingi vyenye CHAMA TAWALA. Sina hakika kama tulijiandaa kufikia uamuzi huo, lakini haidhuru kwa JINA la DEMOKRASIA tumefikia hapa tulipo. Demokrasia yetu imetuzalia DOMO-KILA SAA! Nasema haidhuru, Twende nayo!

Kwa DOMO–KILA SAA nyuma ya DEMOKRASIA, tunataka kuliuza gari kwa mifano niliyosimulia hapo juu! Ikumbukwe wakati wote kwamba huko nyuma na au hapo awali, hali ilikuwa kwamba “majuto ni mjukuu”, lakini kwa sasa majuto ni mwana na au mwenza.

Naungana moja kwa moja na hoja ya Mjengwa na Ndugu Kibanda kwamba kupuuza kazi inayofanywa na Ndugu Kinana ni matokeo ya fikra zilizojengwa katika hoja zilizokosa uchambuzi makini. CCM hivi sasa kinafanya maboresho ya ndani kwa dhati ya uzalendo kwa nchi hii. Katika miongoni mwa mada nilizotuma Jamii forums, niliwahi kusema kwamba tunao watu wenye hamu ya kuongoza kwa hoja ya kuiondoa CCM madarakani na wala sio kwa hoja ya agenda ya maendeleo ya umma. Watu hawa, wanalalamika dhidi ya maadili ndani ya CCM kama kwamba ndiyo inayojipambanua kuwa chemchemi ya wahalifu na kwamba wapinzani ndio wenye ubora. Kabla ya kuingia katika mtego wa ghilba za wenye hamu ya uongozi, yatupasa tujitosheleze na historia binafsi ya viongozi wa upinzani wanaotaka kuwa mbadala wa ujenzi wa mustakabali wa nchi hii. Uongozi hautoki nje ya historia binafsi. Siasa potofu zimewafikisha watu wetu kuamua mambo hata yaliyo muhimu kwa msingi kwa HISIA tu. Ikumbukwe kwamba UIGIZAJI nao huibua na kusisimua hisia za watazamaji na wasikilizaji! Nionavyo mimi, kuwaamini wapinzani ni sawa na kuziba kwa mikono sehemu iliyochanika nyuma ya suruali. Siasa za upotoshaji katika kutafuta uongozi, zimeigeuza nchi yetu kuwa uwanja wa michezo ya kitoto.

Kwa busara na upeo wa mkubwa wa kichambuzi alionao Ndugu Maggid Mjengwa alitupatia nukuu ifuatayo;-
MWANAFALSAFA Benjamin Disraeli anasema; “Mamlaka zote msingi wake ni imani, tunawajibika katika kuyatekeleza yaliyo kwenye mamlaka zetu, na kwamba, mamlaka yatatokana na watu, kwa ajili ya watu, na chemchem zote za fikra ziachwe hai”- Benjamin Disraeli.

Haya aliyoyasema Benjamin Disraeli kama Ndugu Maggid Mjengwa anavyomtaja, ndiyo hasa yanayopata hivi sasa tafsiri ya kivitendo kupitia Makamanda wa CCM wakiongozwa na Ndugu Abrahamani Kinana. WanaCCM wote popote tulipo, tunatakiwa tuyaunge mkono maboresho yanayofanyika ndani ya CCM kwa vitendo dhahiri, bidii inayopimika, uaminifu usiotiliwa shaka, kujali wakati, kutambua mabadiliko ndani ya kizazi chetu na kuzingatia mahitaji halisi ya watu wetu tukiongozwa na kuzifuata ALAMA ZA NYAKATI. Majid Mjengwa anasema; “Maana, leo Kinana na wenzake wanazunguka mikoani wakijenga hoja zaidi za kisiasa zenye kuwagusa wananchi. Mathalan, Kinana na wenzake wameonyesha wanavyofanya kazi ya kuisimamia Serikali kwa kuwabana watendaji wa Serikali hadharani. Kufanya hivyo ni moja ya kutekeleza wajibu wa chama cha siasa kinachoongoza nchi; kuisimamia Serikali”.

Kwa rejea ya simulizi yangu hapo juu, nashawishi watu kutambua umuhimu wa kushirikiana kwa imani, matumaini na uaminifu kufanya maboresho ya dhati ndani ya CCM kama mfumo rasmi wa kuaminika katika kuunda uongozi wa nchi yetu. WanaCCM tunatakiwa hivi sasa kuchukua hatua dhabiti za kujiboresha kimaadili na kiuwajibikaji bila shuruti. Maboresho ya dhati ni yale yanayotambua mahitaji ya msingi ya jamii bila kutazama gharama ya kutekeleza wajibu huo kama kikwazo bali changamoto. Kuwatumikia watu ni kumtumikia MUNGU na ama kutumikia kwa niaba ya MUNGU mwenyewe. CCM ikiteleza majukumu yake kwa kujibu mahitaji halisi ya watanzania, kitakuwa kinafanya hivyo kama mamlaka inayotoka kwa Mungu na hilo linashadidiwa na Historia yake.

WaTanzania wanayo matumaini makubwa kwa CCM nasi wanaCCM tunalo jukumu la kuhuisha matumaini hayo tukijitambua kuwa mamlaka itokayo kwa Mungu. Mungu hashiki beleshi wala kusimamia ujenzi wa barabara, ni Magufuli wa CCM. Ikiwa wanaCCM tukijumuisha wanachama, wapenzi, washabiki na viongozi, hatutaisimamia kikamilifu Serikali tuliyoiunda sisi wenyewe, tukasingizia wajibu huo kwa upinzani, tutakuwa tumeisaliti IMANI ya Watanzania na Mungu atatuhukumu. Kinana ameanza, tumuunge mkono. Tuhuishe imani ya umma kwa CCM tukikubaliana na hoja kwamba MATUMAINI NI KIUNGO KATI YA WATU, MUNGU NA UHALISIA. WaTanzania wanaijua CCM na CCM iendelee kuwajua WaTanzania. WaTanzania wakiiacha CCM kwa kufiwa na matumaini na wakupajipatia mbadala usioaminika, watailaani CCM kwa tukio la kujikuta wakiwa. Watajikuta katika nyika isiyokuwa na tone la maji ya kupooza ndimi zao zilizokaushwa na ukame nyikani. Maggid Mjengwa Kasema; “Umma unahitaji kutoka kwa wanasiasa, kauli zenye kuwatia matumaini ya baadaye. Kauli zenye kuashiria kwamba mwenye kuzitoa, amedhamiria kutatua matatizo yao ya kimsingi. Nikaweka wazi, kuwa hata kwa maslahi ya nchi yetu, ni heri kuwa na CCM yenye makundi yenye kuwania urais 2015 kuliko CCM yenye magenge yenye kuendesha biashara ya ‘siasa za rejareja na au ‘siasa za mafungu’ (retail politics).”

Kutoka sasa na miaka mingine 50 ijayo, hakuna mbadala wa CCM unaohimiliwa na mantiki ya dhati kuhusu mustakabali wa Tanzania, bali mbadala wenye kuhimiliwa na hitaji la kuganga njaa na kutuliza kiu ya kukalia viti vya mamlaka hata kama vimenakshiwa kwa damu isiyo hatia. Dhambi hii itatutafuna kwa vizazi vingi vijavyo kwa kustahili. Sote tujue kwamba Presidential material inapatikana CCM tunapodhamiria kutoa huduma ya uongozi wa dhati kwa nchi hii.

Hoja yangu kwa Watanzania wenzangu ni kuwaomba tukumbuke daima kwamba UKWELI hauna rangi, tabaka, dini, kabila na wala jinsia bali una zana na nyenzo zinazouwezesha kuonekana bayana. Hatutakiwi kujiuliza kwamba ukweli umetoka wapi, bali, UKWELI NI NINI?

Maggid Mjengwa anahitimisha hoja yake kwa kusema; “Kinachohitajika ni mkakati wa kitaifa utakaohakikisha kwamba huko tuendako, tunapunguza idadi ya viongozi wa kisiasa, wa kijamii na hata kimichezo watakaoingia kwa nguvu za fedha, hivyo basi, nguvu ya rushwa. Kama alivyopata kutamka Mwalimu kwenye Kitabu Chake; Uongozi Wetu na Hatma ya Tanzania, rushwa ni kama kansa kwenye jamii yetu. Kwa hiyo, ni tatizo la kimfumo zaidi kuliko la baadhi kwenye jamii”. Kazi hii manju wake ni CCM iliyoboreka na inayotembea katika KANUNI na KATIBA yake. Hii itapatikana kupitia usimamizi madhubiti wenye mizizi inyonyayo RUTUBA YA UZALENDO.

NIMEKUHESHIMU SANA MAGGID MJENGWA.
SHIME TUWEKEZE KWENYE SAYANSI NA TEKNOLOJIA SIO KWENYE SIASA ZA GHILBA…………………….!!!!!!!!!!!
…TUSIENDESHE SIASA YA MAANGAMIZI BALI SIASA ITUANDALIE MAZINGIRA YA KUENDESHA SAYANSI...​
 
Njaa zenu zitawamaliza ninyi na familia zenu...shame on you!​
 
Back
Top Bottom