'Mizigo' hii ilikuwa haikutajwa na Kinana na Nape

Kawambwa, Ghasia na Maghembe si ndio mizigo ya Kinana??

Wameguswa??

Punguza kukurupuka

Mkuu I beg to differ, we ndo umekurupuka hujasoma alichoandika mwenye post bali umejikita kwenye heading, in a figure of speech tunaita alichoandika mwenye post kuwa ni irony
 
Sakata lao bado linakuja, hao waliotoka ni baada ya ripoti ya kamati, hope kamati nyingine nazo zitakuja na ripoti zao covering kashfa za hao waliobaki
 
Wale wa jana haipo katika orodha ya MIZIGO SABA ambapo kawambwa ni wa kwanza ila walikuwa zaidi ya mizigo.Akina nchimbi wapo katika kundi la KIPINDUPINDU

Teh teh teh,Mkuu Kawa-mbwa na Mulugo ni zaidi ya KIPINDUPINDU,sitashangaa hii Wizara akipewa yule mlamba miguu na kilaza Mkuu Said Bagaile a.k.a Kingwengwee.
 
Huyu hafukuziki ni wa kwetu pale bagamoyo. Kama kuna mbunge hajipendi amguse. Same to philipo
 
Jamani, tusiwe wavivu wa kufikiri, wagumu wa kuelewa na wepesi wa kusahau!

Hili tukio la Kagasheki na mizigo mienzake lisitusahaulishe ile 'mizigo ya Kinana' iliyotakiwa kuachia ngazi lakini ikaingia mitini.

Baada ya kuwa mizigo hii ya Operesheni Tokomeza imetuliwa, turudi nyuma hatua moja tukaitue ile 'mizigo ya Nape na Kinana' (Kawambwa, Ghasia, Chiza, Malima, Mgimwa, et al). Bila mizigo hii kung'olewa, kamwe tusitegemee unafuu wowote wa kimaisha.

Na tukitoka hapo, tushuke chini hadi kule halmashauri tukatokomeze mchwa wa wakurugenzi wanaotafuna pesa za maendeleo ya wananchi bila huruma.

Lakini pamoja na hayo tusisahau kwamba ile mizigo ya mwanzo kabisa (Mkulo, Ngeleja, Maige, Chami, Karamagi, Mponda, Nkya, et al) bado haijachukuliwa hatua za kisheria kama ilivyopendekezwa wakati inatuliwa chini.

Haiwezekani kabisa tukawa wepesi wa kusahau kiasi hicho. Lazima sasa tujifunze kurudisha kumbukumbu nyuma na kudai utekelezaji kwa nguvu zetu zote bila kumuonea haya fisadi yeyote yule awaye.
 
Tukumbuke waliojizulu na kutenguliwa sio pekee waliokuwa wakilalamikiwa

Spika na naibu-Kuburuza na kuendesha bunge kibabe,kuzima hoja za wapinzani zenye maslahi,kulinda mawaziri MIZIGO

Waziri wa Maji-Maji hamna,visima vilivyochimbwa havina maji,pesa zinaliwa,bill hewa

Waziri wa Fedha-Ucheleweshaji wa fedha za miradi na utoaji misamaha ya kodi na kutobadili sheria ya Tax holiday huku makampuni yakibadili majina kila siku.Usimamizi mbovu wa TRA na kuruhusu RUSHWA.Kuacha vyanzo vingi vya kodi na kudumaza tax collections

Waziri wa TAMISEMI-Ubadhirifu wa fedha kwenye Hamashauri na wizara yenyewe,Usumbufu kwa walimu na kuwalinda watumishi wezi kwa kuwahamisha vituo badala ya kuwafikisha mahakamani.Ikumbukwe eizara hii mama na ni kubwa chini yake ikiwa na idara za Elimu,Afya,Kilimo,Maji,Ujenzi,Mipango na Ardhi,Maliasili,Mifugo,Uvuvi na huko ndiko kwenye wananchi wengi wa tz wanaohitaji huduma hizo lakini ni uozo mtupu,Mishahara kwa watumishi hewa nk

Wizara ya Elimu-kutuletea div 5,walimu hawapandishwi madaraja,wizi wa mitihani,kukosekana kwa mitaala na malimbikizo ya madai
Waziri wa elimu ya juu-kutoa mikopo bila kufuata ukweli wa vigezo vya uwezo wa wanavyuo

Wizara ya Utawala bora-TISS haoinekani,Takukuru haina meno na kesi zote inashindwa!

Wizara ya Nishati na Madini-Umeme wa mgao na kushindwa kununua mitambo yake na kuendelea kulipa makampuni ya Symbion na Agreko wakati nishati ya kuendeshea(gas) ni yetu
Kukumbatia wageni kwenye vitalu wakati zoezi kama hilo kwenye migodi ni maumivu

Wizara ya Ardhi-kisima cha rushwa na migogoro ya ardhi..kupata hati ni kazi kuliko hata kupata kiwanja chenyewe
Waziri wa nyumba na makazi-hakuna mipango miji wala kujenga nyumba nafuu.zilizopo kutumiwa vibaya

Wizara ya Ujenzi-kuuza nyumba za serikali,kupendelea ujenzi wa barabara kwa baadhi ya maeneo ya nchi na kushindwa kusimamia malori yanayoharibu barabara-refer issue ya malori ya mizigo na mizani iliyoingiliwa na Pinda na kutengua sheria

Waziri wa Afya-Dawa hazifiki kwenye hospitali.kushindwa kutatua madai ya Madaktari.kukosekana huduma za vipimo muhimu na kuwa wagumu kutoa refferal kwa wagonjwa wananchi wa kawaida lakini kusaini vibali kwa wanasiasa ni kitendo cha masaa tu

Waziri wa Uvuvi-pamoja na mita za mraba nyingi za bahari,maziwa na mito lakini hakuna MAPATO

Waziri wa mawasiliano-gharama za mawasiliano hazijashuka licha ya kuunganisha Mkongo.TCRA kutokuwa na monitoring equipment kwa makampuni ya simu kujua mapato na kushindwa zoezi la usajili wa simu na kumlinda mtumiaji anapopata matatizo ya kuibiwa simu,kuibiwa fedha nk

Wizara ya Habari,Michezo-Kushindwa kuwa na sports academy,kufungia magazeti hasa yale yanayoikosoa serikali na kuacha uozo kwenye TV zinazotoa vipindi hovyo na filamu zisizo na maadili..Radio zenye vipindi hovyo na matumizi mabovu ya lugha,magazeti ya full udaku from front page to last page.kutovibana vyombo hivi kuwa na vipindi na makala za kuelimisha na kuviacha kuwa kama vilabu vya starehe yaani mchana kutwa hadi usiku ni burudani wakati vyombo hivi vina athari kwa vizazi vijavyo

Waziri wa viwanda na biashara-kuachia Tanzania kuwa dampo la bidhaa mbovu na kuruhusu viwanda vinavyodhalisha bidhaa hafifu.kwa kifupi kushindwa kusimamia QUALITY & STANDARDS

Wizara ya jumuia ya Afrika Mashariki-haipo ishakufa

Waziri Mkuu-kushindwa kusimamia mawaziri mizigo na kuamuru wananchi WAPIGWE TU

ANGALIZO:
hata watakaochaguliwa kuziba mapengo ya Mizigo na wao soon watakuwa Mizigo wasipozingatia mambo muhimu kama haya machache

  • -kurithi mifumo ya utendaji ya kizamani bila ubunufu kuendana na kasi ya dunia ya sasa
  • -Kurithi watendaji wabovu na wanaolalamikiwa kukwamisha maendeleo,rushwa na urasimu
  • -Kutowatembelea wananchi na kusikia kero zao
  • -Kupendelea miradi ya wizara zao kwenye majimbo yao
  • -kuhodhi habari,kutokuwa na uwazi na kujenga ukuta mnene kati ya waziri na watu wengine
  • -kuingilia kazi za watendaji kwa kutumia hoja za kisiasa
  • -Kusafiri kila siku na mikutano ambayo ingehusu wataalamu zaidi lakini mawaziri kujipeleka wao
  • -kuwa na MAJIBU MEPESI na hayohayo KILA SIKU bungeni
 
usiendeshwe kwa matukio kagasheki sio mzigo na wewe humjui. na hujui nyuma ya pazia kuna nini.hategemei uwaziri waka ubunge kuendesha maisha.yake.ujangirii sio vita ya kitoto

aaakh--kumbe uwaziri ni 'ulaji' sio utumishi wa umma? sasa kama alijua hana njaa kwanini hakuwaachia wenye njaa nao wale? acha akili zako mgando ndugu yangu.
 
Serikali ya JK ni ya kwanza Tz kuwa na mizigo mingi.
 
CCM ina mizigo mingi sana. David Mathayo ndio pekee yake aliyekuwepo kwenye mizigo ya kwanza ya CCM.

Kina Kinana na Nape hakuwahi kuwataja kina Nchimbi, Nahodha na Kagasheki kuwa ni mizigo.

Sasa nina amini kuna mawaziri wengi mizigo katika serikali hii ya CCM.

Nasubiri JK siku ya kushughulikia mizigo ya awali. Baba Jk pakua mizigo meli inazama.
Hapo tafsiri yake ni kuwa almost Cabinet nzima ni mizigo aka mapakacha!

Hata hivyo kuna msemo unaosema kuwa kuvuja kwa pakacha, nafuu kwa mchukuzi!

Hiyo tafsiri yake ni kuwa kwa JK kuyatua chini mapakacha hayo, imekuwa nafuu kwa watanzania, tuliokuwa tunayabeba mapakacha hayo, kwa kuwalipa mishahara minono na marupurupu kibao kwa kodi zetu, kumbe mawaziri wetu walikuwa wanafanya kazi ya kutesa na kuangamiza maisha ya waTz!
 
Nimefurahishwa sana na Kufukuzwa ama kujihudhuru kwa mawaziri mizigo

LAKINI NIMESHTUSHWA KWA HUYU MZIGO MKUU PINDO KUTOKUFUKUZWA AMA KUJIUDHURU
TATIZO LIPO WAPI?
 
Tukumbuke waliojizulu na kutenguliwa sio pekee waliokuwa wakilalamikiwa

Spika na naibu-Kuburuza na kuendesha bunge kibabe,kuzima hoja za wapinzani zenye maslahi,kulinda mawaziri MIZIGO

Waziri wa Maji-Maji hamna,visima vilivyochimbwa havina maji,pesa zinaliwa,bill hewa

Waziri wa Fedha-Ucheleweshaji wa fedha za miradi na utoaji misamaha ya kodi na kutobadili sheria ya Tax holiday huku makampuni yakibadili majina kila siku.Usimamizi mbovu wa TRA na kuruhusu RUSHWA.Kuacha vyanzo vingi vya kodi na kudumaza tax collections

Waziri wa TAMISEMI-Ubadhirifu wa fedha kwenye Hamashauri na wizara yenyewe,Usumbufu kwa walimu na kuwalinda watumishi wezi kwa kuwahamisha vituo badala ya kuwafikisha mahakamani.Ikumbukwe eizara hii mama na ni kubwa chini yake ikiwa na idara za Elimu,Afya,Kilimo,Maji,Ujenzi,Mipango na Ardhi,Maliasili,Mifugo,Uvuvi na huko ndiko kwenye wananchi wengi wa tz wanaohitaji huduma hizo lakini ni uozo mtupu,Mishahara kwa watumishi hewa nk

Wizara ya Elimu-kutuletea div 5,walimu hawapandishwi madaraja,wizi wa mitihani,kukosekana kwa mitaala na malimbikizo ya madai
Waziri wa elimu ya juu-kutoa mikopo bila kufuata ukweli wa vigezo vya uwezo wa wanavyuo

Wizara ya Utawala bora-TISS haoinekani,Takukuru haina meno na kesi zote inashindwa!

Wizara ya Nishati na Madini-Umeme wa mgao na kushindwa kununua mitambo yake na kuendelea kulipa makampuni ya Symbion na Agreko wakati nishati ya kuendeshea(gas) ni yetu
Kukumbatia wageni kwenye vitalu wakati zoezi kama hilo kwenye migodi ni maumivu

Wizara ya Ardhi-kisima cha rushwa na migogoro ya ardhi..kupata hati ni kazi kuliko hata kupata kiwanja chenyewe
Waziri wa nyumba na makazi-hakuna mipango miji wala kujenga nyumba nafuu.zilizopo kutumiwa vibaya

Wizara ya Ujenzi-kuuza nyumba za serikali,kupendelea ujenzi wa barabara kwa baadhi ya maeneo ya nchi na kushindwa kusimamia malori yanayoharibu barabara-refer issue ya malori ya mizigo na mizani iliyoingiliwa na Pinda na kutengua sheria

Waziri wa Afya-Dawa hazifiki kwenye hospitali.kushindwa kutatua madai ya Madaktari.kukosekana huduma za vipimo muhimu na kuwa wagumu kutoa refferal kwa wagonjwa wananchi wa kawaida lakini kusaini vibali kwa wanasiasa ni kitendo cha masaa tu

Waziri wa Uvuvi-pamoja na mita za mraba nyingi za bahari,maziwa na mito lakini hakuna MAPATO

Waziri wa mawasiliano-gharama za mawasiliano hazijashuka licha ya kuunganisha Mkongo.TCRA kutokuwa na monitoring equipment kwa makampuni ya simu kujua mapato na kushindwa zoezi la usajili wa simu na kumlinda mtumiaji anapopata matatizo ya kuibiwa simu,kuibiwa fedha nk

Wizara ya Habari,Michezo-Kushindwa kuwa na sports academy,kufungia magazeti hasa yale yanayoikosoa serikali na kuacha uozo kwenye TV zinazotoa vipindi hovyo na filamu zisizo na maadili..Radio zenye vipindi hovyo na matumizi mabovu ya lugha,magazeti ya full udaku from front page to last page.kutovibana vyombo hivi kuwa na vipindi na makala za kuelimisha na kuviacha kuwa kama vilabu vya starehe yaani mchana kutwa hadi usiku ni burudani wakati vyombo hivi vina athari kwa vizazi vijavyo

Waziri wa viwanda na biashara-kuachia Tanzania kuwa dampo la bidhaa mbovu na kuruhusu viwanda vinavyodhalisha bidhaa hafifu.kwa kifupi kushindwa kusimamia QUALITY & STANDARDS

Wizara ya jumuia ya Afrika Mashariki-haipo ishakufa

Waziri Mkuu-kushindwa kusimamia mawaziri mizigo na kuamuru wananchi WAPIGWE TU

ANGALIZO:
hata watakaochaguliwa kuziba mapengo ya Mizigo na wao soon watakuwa Mizigo wasipozingatia mambo muhimu kama haya machache

  • -kurithi mifumo ya utendaji ya kizamani bila ubunufu kuendana na kasi ya dunia ya sasa
  • -Kurithi watendaji wabovu na wanaolalamikiwa kukwamisha maendeleo,rushwa na urasimu
  • -Kutowatembelea wananchi na kusikia kero zao
  • -Kupendelea miradi ya wizara zao kwenye majimbo yao
  • -kuhodhi habari,kutokuwa na uwazi na kujenga ukuta mnene kati ya waziri na watu wengine
  • -kuingilia kazi za watendaji kwa kutumia hoja za kisiasa
  • -Kusafiri kila siku na mikutano ambayo ingehusu wataalamu zaidi lakini mawaziri kujipeleka wao
  • -kuwa na MAJIBU MEPESI na hayohayo KILA SIKU bungeni

MBONA UMEMALIZA WIZARA ZOTE. Hapo imebaki Wizara ya Popo tu, Muda huu yupo Anga la Amerika
 
Back
Top Bottom