'Mizigo' hii ilikuwa haikutajwa na Kinana na Nape

mkuu wewe ni mstaarabu.ni hivi chini ya kagasheki kuna maofisa wa wizara wakuu wa polisi wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya na wengine kibao.waziri hakuusika diretly kuuwa watu.na kubaka watu ila kwakua yeye ndo waziri imemlazimu ajiuzulu na ni jambo la kawaida.sijasoma repoti ila predictions ni mbili zoezi limefanyika bila umakini Au limehujumiwa na majangiri.kwa vyovyote vile waziri lazima awajibike.mfumo ni mbovu

Rushwa imetajwa kuhusika kikamilifu sasa jiulize rushwa imehusika katika lipi.


mawaziri mizigo wanajulikana.
naungana na wewe, dhamira ya kagasheki ni safi kabisa lakini kuna mijitu milafi na haina mwiko katika kuhujumu waliasili ndio wako front kuendesha hili zoezi na nuda si mrefu maliasili tutaishiwa na tutamkumbuka kagasheki
 
Kumbe mijamaa inafaidi aisee. Namna hii utasitisha ziara mikoani kweli? Hata hivyo kazi ya Kinana na Nape ilikuwa ni kumtambulisha mgombea wa CCm 2015 Asha Migiro kwa wananchi. Kero za wananchi ni za kimfumo na huwezi kuziondoa kwa ku-isolate episodes kama wafanyavyo Kinana na Nape. Mfumo mzima wa utawala umeoza kabisa labda wafumue wote. Hivi ile dossier ya Prof. Mihanjo na Mukama imetupwa wapi? Ile ilikuwa ni dawa mjarabu kwani ilitoa very concrete and tangible solutions to the inherent crisis in the body-politic. Kikwete na waafidhina wake akiwemo kingunge wakaigwaya na kuitupilia mbali. Mukama kaamua kuachia ngazi baada ya kuona anafanya kazi na waswahili maneno mengi vitendo kidogo. Jumba bovu kasukumiwa Kinana naye anajaribu kunyofoa vipengele anavyoona anaweza kuwa-impress mbulula ma-ccm kwamba anafanya kazi isiyo tija.. Ukitaka kutekeleza ile dossier sharti uitekeleze nzimanzima maana imesukwa dialectically interconnected (mavitu ya Hegelian na Marxian world outlook).
 
Nape na Kinana wote pia nimizigo, nadhani wajipime hasa kwa kashfa ma Tembo wa bwana katibu mkuu...Nadhani yeye ni mzigo namba moja katika nchi hiii..Nape mchumia tumbo
 
Huyu kaja kule Iringa kijini kwetu anadai wananchi tumevamia eneo la serikali.
Mwaka 1974-75 serikali ya CCM kupitia TANU ilituhamisha kutoka kwenye maeneo yetu asilia katika kile kilichoitwa Operesheni Sogeza. Eneo lililoachwa wazi serikali ikachukua na kulifanya la serikali. Sasa karne hii ya 21 akina Kagasheki wanakuja na kudai wananchi tumevamia eneo la serikali. Napata uchungu tena uchungu mkali.
Akija kujipendekeza tena kiongozi mwingine historia ya Iringa itarudiwa tena. Mwamwindi alionewa jna kudhurumiwa ardhi na Mafisadi wa CCM( TANU), wanafikiri tumesahau.

Swela bee!

Mkuu umenichekesha. Kagasheki tena mzigo ulijiangusha wenyewe.
 
Kama mizigo bado JK mawaziri wa serikali yake atawatoa wapi? Last time ilimrazimu kuteua wabunge nje ya mfumo wa kiccm ambao kwa kiasi nao wame-prof failure (Mhuongo).

Dhambi zitawatafuna, dawa ni kurudisha mlivyoiba...jk naye kuachia ngazi...kuna madudu mengi nyuma yake.

Kinana ataponaje ktk ili?
 
Walimu bado wana masikitiko makubwa kwani waziri mzigo shukuru kawa-mbwa kwa nini hajajiuzuru.kashindwa kazi.madai ya walimu,walimu hawapandishwi madaraja.uafisa elimu wanapeana kwa upendeleo.maisha ya walimu yako duni sana mishahara kiduchu.
 
Wale wa jana haipo katika orodha ya MIZIGO SABA ambapo kawambwa ni wa kwanza ila walikuwa zaidi ya mizigo.Akina nchimbi wapo katika kundi la KIPINDUPINDU
 
Ha ha ha ha haaaa! huyo mzee wa division 5 sijui anasubiri nn me hata simwelewi na yule mwenzake aliyeshindwa kufanya presentation huko nje! aibu sana hawa mawaziri mizigo kwelikweli. umemsahau na yule mama wa tamisemi aliyeshindwa kupambana na ubadhirifu katika halmashauri.
 
Walimu bado wana masikitiko makubwa kwani waziri mzigo shukuru kawa-mbwa kwa nini hajajiuzuru.kashindwa kazi.madai ya walimu,walimu hawapandishwi madaraja.uafisa elimu wanapeana kwa upendeleo.maisha ya walimu yako duni sana mishahara kiduchu.

Na wewe umeandika eeh!
 
Hakika nasubiri kuona Ata amishiwa Wizara Gani safari hii maana Jamaa anashikiria Rekodi ya Kuhama hama Wizara, Yani ukiona CV yake ya kushika Wizara Tofauti unaweza kufikiri ni waziri aliyepo serekalini toka Enzi za mwalimu, Kumbe Hata miaaka 10 hana, Lakini kashashika wizara karibia Tano sasa.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom