Geeque
JF-Expert Member
- Aug 17, 2007
- 936
- 317
Nchi yetu ni ya Wadanganyika ambao wanakubali kila kitu kutoka kwa viongozi MAFISADI. Hakuna tumaini lolote nchini Tanzania kwa sasa litakaloletwa na CCM au wanachama wake, tusitegemee chochote kipya kutoka kwa MAFISADI na washirika wao ambao wanapindisha mizengwe na uongo wa kila aina kuwahadaa Watanzania. Nadhani siri pekee wanayoijua ni kuwa watanzania ni waoga, wajinga na ni watu wa kuitikia ndio kila kitu ambacho MAFISADI watakachosema. Hakuna tumaini lolote na kilichobaki hivi sasa ni mabadiliko makubwa katika uongozi pale nchini. Dr. Slaa ndio mtu anaetufaa kutuongoza mwaka 2010, jamani wakati ndio huu na hakuna ngoja ngoja, tumuombe sana Dr. Slaa agombee hii nafasi. Ningeomba Invisible uifungulie ile topic yangu ya Dr. Slaa for President ili tuendelee kuichangia. Hakuna Tumaini kutoka CCM. Hakuna tumaini lolote pale ambapo Mizengwe Inapindishwa Mchana Kweupe ili kuwahadaa wananchi. Tusitegemee MAFISADI kuchukuliwa hatua zozote kwenye suala la EPA, Richmond, BOT,Kiwira, TTCL na uchafu mwingine wowote.
Wakati mwingine demokrasia haiji kwa amani, haiji kwa kujaribu kutumia vyombo sahihi vya umma, haiji kwa kufuata utaratibu unaotakiwa, haiji kwa kutegemea CCM watabadilika, haiji kwa kukaa kusubiri mwingine afanye mabadiliko. Sasa ni muda muafaka wa kuanza kutumia njia mbadala ambazo zinaweza kuwa si za kidemokrasia lakini dhumuni lake kubwa ni kuleta demokrasia nchini kwetu.