Mizengwe na rushwa vinatawala kwenye chaguzi za vyama vya ushirika hapa kagera.

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
chaguzi zinazoendelea hivi sasa hapa Kagera katika vyama vya ushirika vya msingi vinavyounda KCU 1900 LTD. Zimegubikwa na mizengwe na rushwa kiasi cha kufanya chaguzi hizo kuwa mpakazo husio na maudhui yeyote.

Hali hiyo inasababishwa na kuwepo njama kati ya uongozi na watendaji wakuu wa KCU1900 LTD Kwa upande mwingine ,ili kuakikisha watu wanaowapenda wao ndio wanaoshinda katika chaguzi.

Katika kuhakikisha njama zao hizo zinafanikiwa , wamekuwa wakipindisha kanuni zinazosimamia chaguzi hizo,KWA MFANO kutegemea kama mgombea ni rafiki au adui, katika baadhi ya vyama. Mtu aliyejiudhuru kukidhi matakwa ya thelusi amekuwa akiruhusiwa kugombea tena lakini katika vyama vingine anakatazwa.

Mbali na hayo kumekuwepo pia matumizi makubwa ya rushwa .KWA MFANO katika chama cha msingi cha MARUKU mgombea wa nafasi ya uwakilishi ambaye pia ni mkurugenzi wa KCU.alikodi haice mbili za kupeleka wajumbe kwenye mkutano na kila mjumbe aliyekuwa akipanda hiace hizo alipewa sh 10000.

Kutokana na hayo natoa rai kwa mrajis wa vyama vya ushirika nchini kuingilia kati na kurekebisha hali hiyo. Vinginevyo majigambo kuwa atua zitachukuliwa kuimarisha ushirika nchini zitakuwa ni maneno matupu.
 
Back
Top Bottom