Mizengo Pinda: Ni sawa kwa wakuu wa wilaya kuinadi CCM mikutanoni! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mizengo Pinda: Ni sawa kwa wakuu wa wilaya kuinadi CCM mikutanoni!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Makala Jr, Aug 16, 2012.

 1. Makala Jr

  Makala Jr JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Ni siku chache tokea wakuu wa wilaya walipokula kiapo cha uaminifu wa kuwatumia wananchi wote pasipokujali itikadi za wananchi husika. Cha kushangaza, leo hii Waziri mkuu, mhe.Mizengo Pinda a.k.a mtoto wa mkulima (asiye na shamba) amesema ni sahihi kwa wakuu wa wilaya kuinadi ccm (kama makatibu wenezi) wanapokuwa wilayani haswa katika mikutano ya hadhara.

  Alipokuwa anajibu swali la Mb.Ezekiel Wenje kuhusu uhalali wa wakuu wa wilaya kukinadi chama wakati wanatumia kodi za watanzania wote kupitia mishahara,usafiri na posho wanazopewa Wakuu hao. Kwa mtazamo wa mtendaji mkuu wa serikali Mhe.Pinda aliyedai ni sawa kunadi chama na kuelezea utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi kinachokimbiwa na wanachama kila kukicha.

  Baadhi ya wananchi niliowahoji mjini Mbeya...wamesema hawana imani na wakuu wa wilaya wakiwa kama Wakuu wa ulinzi na usalama wilayani kwani hawawezi kusimamia haki panapo matatizo kwa kuwa wanafungamana na chama cha (zamani).Katiba mpya itutatulie utata huu.
   
 2. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2012
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kwa mwendo huu wataendelea kufanya utawala wao kuwa mgumu, kwani wananchi waliowengi watakasa imani nao na kutoshiriki katika miito pamoja na majukumu yatakayokuwa chini ya usimamizi wao.

  Ni bora wakaliangali pia kwa jicho la pili, sio kudhani kuwa itawaokoa katika kipindi hiki wanaposhika kwa mwendo kasi mtoroko!
   
 3. M

  Mzee Kabwanga Member

  #3
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 68
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tatizo lipo ktk katiba ya nchi hakuna inapoeleza majukumu ya mkuu wa wilaya au mkoa wapo wapo tuu . Mara mjumbe wa kamati ya siasa mara mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama . Tutoe maoni yetu ktk tume ya katiba.
   
 4. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Huu ni ushenzi kabisa. Yaani Mkuu wa Wilaya na Mkoa wanawakilisha SSM wakati wanawakilisha wananchi wote na vyama vyao? They are supposed to be neutral katika siasa. Katiba mpya ifikirie suala hili kwa makini sana. Just a little brain to issues about this sensibly!!!
   
 5. c

  chuwaalbert JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 3,062
  Likes Received: 1,450
  Trophy Points: 280
  Maumivu ya Kichwa huanza pooolepoole, maumivu si mchezo...........
   
 6. Makala Jr

  Makala Jr JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hivi ni kwanini nchi imetumia rasilimali nyingi kuwalipa wakuu wa mikoa na wilaya pasipo kuandikwa kwa kueleweka majukumu yao tangu 1992 baada ya vyama vingi? Ama kweli Raila Odinga aliona mbali aliposema UTULIVU unatokana na satisfaction au kutojitambua.
   
 7. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #7
  Aug 17, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,458
  Trophy Points: 280
  Rafiki, mchakato wa sasa wa Katiba Mpya umeshachakachuliwa na hao hao ma-RCs na ma-DCs. Lazima baada ya 2015 tutengeneze mchakato mpya wenye kukubalika na halali ili tupate Katiba ya Ukweli. Mchakato wa sasa ni kiini macho.
   
 8. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo wameshaingizwa rasmi katika kundi la mafisadi. Tutapambana nao mpaka kieleweke, kilio na kusaga meni ni 2015. Pinda keshawafukuza kazi in advance, wasimlaumu mtu.
   
 9. Adharusi

  Adharusi JF-Expert Member

  #9
  Aug 17, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 10,635
  Likes Received: 3,017
  Trophy Points: 280
  :nerd:Amelewa madaraka pinda....alishawahi ulizwa hilo swali kipindi kile ndo anaanza uwazir mkuu,alijibu kwa nidhamu sana
   
 10. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #10
  Aug 17, 2012
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Hilo jicho la pili wanalo? wangekua nalo mbona wangeona mauchafu yao mengi tu. Nadhani wanalo moja tu tena linaloishiaishia maana inabidi watumie lensi yenye nguvu sana. Na kwa kutumia hiyo lensi kitu chenye ukubwa kama tembo wanakionakama punjeya mtama!! Hebu fikiria ufisadi unaouona; unafikiri wao wanauona?!
   
 11. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #11
  Aug 17, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,992
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Kama kumbukumbu zangu zipo sawa hawa wakuu wa wilaya walitakiwa kusimamia mchakato wa katiba mpya wakitetewa kuwa hawafungamani na CHAMA CHA MAPINDUZI!imekuwaje ghafla mtoto wa mkulima (anayelima) anatangaza hadharani kuwa wanatikiwa kufanya kazi za ukada kama NAPE na MUKAMA
   
 12. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #12
  Aug 17, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Na hili ni udhaifu mkubwa wa kuweza kuwaelimisha wananchi ili kulifanyia mabadiliko katika katiba. Sijaona umuhimu wa wakuu wa mikoa zaidi ya kujiongezea gharama za kuendesha serikali na kutoa nafasi za zawadi kwa Rais kuwapa watu wake wengi waliokosa Ubunge. Ukuu wa wilaya kazi zake zinatakiwa ziainishwe katika katiba na zisiwe za kiitikadi.
   
 13. t

  thatha JF-Expert Member

  #13
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  waziri mkuu hakumumunya maneno.ameitoa black and white.
   
 14. t

  thatha JF-Expert Member

  #14
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  wakuu wa wilaya ndio wawakilishi wa rais katika wilaya zao na ndio wasimamizi wa amani na utulivu katika maeneo yao.
   
 15. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #15
  Aug 17, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Mizengo Pinda mimi huwa namfananisha na Masanja Mkandamizaji!
   
 16. m

  magohe JF-Expert Member

  #16
  Aug 17, 2012
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  huu ni upuuzi tu alioujibu pinda kwani kila anaelipwa na serikali kama mfanyakazi ni budi kueneza sera za chama tawala? Au lengo kuu ni kuhudumia jamii yote bila kujali tofauti za itikadi zao kama taifa!! Ifahamike kuwa itafikia kipindi watu watashindwa kujitokeza ktk shughuli za maendeleo kwa kuhofia kwenda kuhubiriwa siasa za chama ambacho kwao ni kero kubwa na chenye kuwatia kichefuchefu.kuna hatari pia ya hata baadhi ya wanafanyakazi wa umma mathalani madaktari,walimu na wengineo kuhudumia watu baadhi kwa kujali msimamo wao wa kiitikadi kwa kisa cha kukubaliana na sera za chama tawala.jamani tunalipeleka wapi taifa hili? nijuavyo mimi public servant yeyote awaye yule hapaswi kujishughulisha na mambo ya kisiasa bali kutekeleza majukumu ya serikali inayoongoza watu wa itikadi zote vinginevyo wasije laumiwa watu wakijitokeza kwa kusema hawaitambui serikali iliyoko madarakani kwa kuwaita wahaini au wanataka nchi isitawalike kama watawala wengi wanaopingwa wakiwashutumu watu wenye kuwapinga...Pinda tafakari kabla hujaropoka!!
   
 17. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #17
  Aug 17, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Bora Masanja Mkandamizaji anatufanya tunacheka. Huyu mzee ametufanya tumebaki kulia tu. Anatudanganya masuala ya mkulima wakati kundi la wachache linazidi kuneemeka na nchi hii. Siku ya siku inakuja, hata ikichelewa but yaja.
   
 18. B

  BigMan JF-Expert Member

  #18
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,097
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Kwenye katika ya sasa majukumu ya mikuu wa mkoa yapo kaka soma vizuri katika no Kama tulivyo watz kukurupukia Hoja hate Kama hatujafanya utafiti
   
 19. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #19
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Ninamheshimu sana PM lakini ananikwaza maana ukweli ameonyesha udhaifu mkubwa katika kujibu maswali ya papo kwa papo bungeni, kutekeleza ilani ya chama sio siasa, siasa hukoma kwenye kuiandaa, lakini utekelezaji huhusisha taaluma, rasilimali na kodi za wananchi wote pasipo kujali itikadi zao.

  Mkuu wa mkoa/wilaya huhusika kwa kiwango kikubwa kusimamia utekelezaji wa ilani na sio kupiga siasa jambo ambalo wakuu wengi hulifanya na cha kushangaza hata PM anaunga mkono, maendeleo yatajia wapi kama wasimamizi wa maendeleo badala ya kuelekeza akili zao na nguvu kwenye maendeleo huelekeza akili hizo na nguvu kwenye siasa?

  Inabidi swala la wakuu hao lijadiliwe kwa kina ikibidi waondolewe la sivyo wachaguliwe na wananchi badala ya uteuzi au gharama zao zibebwe na vyama maana wapo kisiasa zaidi na si kiserikali.
   
 20. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #20
  Aug 17, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,193
  Trophy Points: 280
  Tatizo tunaiga kila kitu.

  Bunge tumeiga Westminster, mpaka majibu ya hapo kwa papo nayo tumeiga.

  Wakati Waziri Mkuu wetu hata kumung'unya boilerplate iliyopakwa koti la ukweli kama PM wa UK hawezi.

  Hapo kwenye maswali ya hapo kwa papo hamna desa wala personal assistant kusaidia kupata desa, ndipo unajua nani fahali na nani ndama.
   
Loading...