Mizengo Pinda: Natamani Katiba ya Tanzania ibadilishwe, ili Rais Magufuli aongezewe muda zaidi

Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda amesema isingekuwa katiba ipo “tight” kidogo, basi angetamani kuona Rais Magufuli akiongeza miaka mingine mitano baada ya muda wake kuisha.
Huyu mzee mnafiki huyu!!!

Si ndiye alimkataza Magufuli asiwe strict kwenye uharibifu wa barabara!!!!
Si ndiye huyu alimkemea Magufuli alifikirie kudondosha jengo la Tanesco!!!

Katiba isingekuwa tight huyu alitakiwa kukamatwa na kuwekwa ndani
 
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda amesema isingekuwa katiba ipo “tight” kidogo, basi angetamani kuona Rais Magufuli akiongeza miaka mingine mitano baada ya muda wake kuisha.

"Ni kwakuwa tu katiba zenyewe kidogo ziko taiti lakini kama si kwa sababu hiyo, Walahi ningesema mzee piga mingine mitano tu''

Pia Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu ameongeza kuwa:

“Ni matumaini yetu kwamba katika kipindi hiki hata kama utatugomea kabisa kuongeza kidogo, lakini utahakikisha basi umetupa kiongozi mwingine mzuri kwa kusaidiana na NEC, atakayeweza kusukuma mawazo haya na maamuzi haya magumu ambayo unayafanya”

Mzee Pinda ametoa kauli hiyo leo hii wakati wa Semina ya Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) iliyofunguliwa na Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, inayofanyika Jijini Mwanza.

]Hawa ni wale wale wa "mtumikie kafiri upate mradi wako" baada ya kugundua maneno aliyokuwa anategemea kusikia toka kwa vimbelembele wake.
 
Badala ya kuangalia ni vipi tunajenga mifumo na taasisi zenye kuweza kutupa uongozi bora endelevu bila kujali kiongozi ni nani, tunapigia chapuo na jaramba habari za kubadili mifumo na taasisi ili zimruhusu mtu mmoja kutawala zaidi.

Hii ni moja ya sababu kubwa bado tupo masikini.

Hatufikirii sera, mifumo, taasisi, dhana.

Tunafikiria watu, matukio na mambo madogomadogo.

Mtu kama Pinda huyo naye kasoma sheria, kafanya kazi usalama, kafanya kazi Ikulu, kawa mbunge, kawa mpaka Waziri Mkuu.

Lakini bado anaongea mambo kama vile mtu asiyejua misingi ya utawala bora na uongozi endelevu.

Huyo mtu wanayetaka kumuongezea muda akianguka na kufariki kesho itakuwaje?
Uliuliza swali la msingi kabisa hapo mwisho.
 
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda amesema isingekuwa katiba ipo “tight” kidogo, basi angetamani kuona Rais Magufuli akiongeza miaka mingine mitano baada ya muda wake kuisha.

"Ni kwakuwa tu katiba zenyewe kidogo ziko taiti lakini kama si kwa sababu hiyo, Walahi ningesema mzee piga mingine mitano tu''

Pia Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu ameongeza kuwa:

“Ni matumaini yetu kwamba katika kipindi hiki hata kama utatugomea kabisa kuongeza kidogo, lakini utahakikisha basi umetupa kiongozi mwingine mzuri kwa kusaidiana na NEC, atakayeweza kusukuma mawazo haya na maamuzi haya magumu ambayo unayafanya”

Mzee Pinda ametoa kauli hiyo leo hii wakati wa Semina ya Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) iliyofunguliwa na Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, inayofanyika Jijini Mwanza.

Ayarudie Tena
 
Mzee Mwinyi na Pinda fix zao zililipa maana walizipiga vyema. Calculated Fix.
Ona wamefanikiwa walichotaka, Mwinyi mwanae katunukiw Urais Zenji na Pinda mwanae uwaziri Bara.
Yaani jamaa alikuwa akipenda sifa sana, hata Angetokea mtu akamsifu "Jiwe ana sura nzuri kuliko Cleopatra" angemuuliza unahitaji cheo gani?
 
Back
Top Bottom